MAHUBIRI YA SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTO: MWAKA A WA KANISA 2020
MAHUBIRI YA SHEREHE YA MWILI NA DAMU
TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTO: MWAKA A WA KANISA 2020
MASOMO
SOMO I: Deut.8: 2-4, 14-16a
SOMO II: 1Cor.1: 16-17
INJILI: John/Jean 6: 51-58
SALA: Tumuombe Mungu, kusudi kwa Mwili na Damu Takatifu ya Bwana Wetu Yesu
Kristo Mwanaye Mpendwa, Mungu na Mwokozi wetu na kwa utakaso wa Roho Mtakatifu,
mimi na wewe leo tutambuwe upendo utakalo kwa Ekaristi Takatifu katika jumuiya
yetu, Maisha na familia zetu pia katika nchi na taifa zetu.
UTANGULIZI
Wapendwa, baada ya kusherekeya sherehe ya
Utatu Mtakatifu Dominika iliopita yaani tulisherekeya Umoja na Upendo usiogawanyika katika Mungu Mmoja, leo tena kwa namna ya pekee tunasherekeya
sherehe ya Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo: Maana yake leo
tunataka kumshukuru tena Mungu kwa ajili ya upendo wake kwetu kupitia kazi yake
ya uumbaji na wokovu wetu. Tukiwa na dhamira hiyo tumuombe Mungu atusaidia
tutambuwe uwepo wa Yesu Kristo kila siku katika adhimisho ya Ekaristi kama kielelezo cha umoja na upenda kati yetu na Mungu pia kati yetu sisi kwa sisi wanadamu.
UFAFANUZI
Wapendwa Taifa la Mungu: SHALOOM /
TUMSIFU YESU KRISTO: Wapendwa tunaweza kujiuliza kwa nini leo tunasherekeya
tena sherehe ya Mwili na Damu Takatifu ya Bwana Wetu Yesu Kristo wakati
Alhamisi Kuu (Jeudi Saint) tulisherekeya kuwekwa rasmi kwa sakramenti Ekaristi pia sakramenti ya Upadre? Wapendwa jibu ni
kwamba, Alhamisi Kuu, ni kweli tulisherekeya kuwekwa rasmi kwa sakramenti ya
Ekaristi na Bwana wetu Yesu Kristu na pia kuwekwa rasmi kwa sakramenti ya
Upadirisho. Kwa hiyo Kanisa utufundisha kwamba: Mwokozi wetu, katika karamu ya
mwisho, usiku alipotolewa, aliweka sadaka ya Ekaristi ya Mwili wake na Damu
yake. Alifanya hivyo ili kuendeleza sadaka ya msalaba siku zote mpaka
atakaporudi, kusudi amwachie Bibiarusi Mpendwa yaani Kanisa, ukumbusho wa kifo
chake na ufufuko wake: Sakramenti Takatifu, ishara ya Umoja na kifungo cha
Upendo.
Lakini leo kwa namna ya pekee
baada ya kusherekeya mafumbo ya wokovu wetu yaani Pasaka: tunaadhimisha sherehe
hii kwanza kama shukrani kwa Utatu Mtakatifu kwa kuwa kwa njia ya Mateso, Kifo
na Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo ulimwengu mzima ulikombolewa na binadamu
kupewa tena neema ya kushiriki katika upendo na umoja wa Mungu. Pili Kanisa
katika sherehe hii utupa tena nafasi ya kutafakari nguvu na umuhimu wa Ekaristi
Takatifu katika Maisha yetu ya Imani na wokovu. Tatu sherehe hii utukumbusha
mafundisho ifatavyo kuusu Ekaristi Takatifu: Mosi Ekaristi Takatifu
hukamilisha kuingizwa katika ukristo. Wale walioinuliwa katika heshima ya
ukohani wa kifalme kwa Ubatizo na kufananishwa kwa ndani Zaidi na Kristo kwa
Kipaimara, hushiriki Pamoja na jumuiya yote katika sadaka moja ya Bwana. Pili
Ekaristi ni chemchemi na kilele cha Maisha yote ya Kikristo. Sakramenti
nyingine, kama zilivyo pia huduma zote za kanisa na kazi za utume, zaungana na
Ekaristi na zaelekezwa kwake. Kwani katika Ekaristi Takatifu mna kila hazina ya
kiroho ya kanisa, yaani Kristo Mwenyewe, Pasaka wetu. Tatu Ekaristi ndio ishara
thabiti na sababu ya hali ya juu kabisa ya ushirika katika uzima wa kimungu na
umoja ule wa taifa la Mungu ambao unalifanya Kanisa liwepo. Maana yake
Ekaristi ni kilele cha tendo la Mungu la kuutakatifuza ulimwengu katika Kristo,
na kilele cha tendo la kumwabudu Mungu wampalo watu Kristo, na kwa njia yake
wampalo Baba katika Roho Mtakatifu. Mwishowe, kwa njia ya adhimisho la Ekaristi
tunaungana tayari sisi wenyewe na liturjia ya mbinguni na tunaanza kutangulia
kushiriki uzima wa milele Mungu atakapokuwa yote katika wote.
Basi wependwa tunao sababu ya
kutosha kusudi leo kwa namna ya pekee tutafakari kuusu Ekaristi ambao kwetu
sisi leo ni shukrani kwa Mungu ambaye yupo nasi kila siku asa pale ambapo
tunashiriki katika Misa Takatifu. Ndio maana masomo yote tatu ya leo utualika
kutambuwa Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo kama mafumbo ya
wokovu na Imani Yetu. Katika agano la Kale mkate na divai vilitolewa sadaka
kati ya mazao ya kwanza ya nchi, ishara ya kumkiri Muumba. Lakini vinapata pia
maana mpya katika tendo lote la Kutoka yaani ukombozi wa israeli kutoka utumwani Misri: mikate isiyotiwa chachu ambayo Israeli hula kila mwaka wakati
wa Pasaka hukumbusha ukombozi wao kwamba aliishi kwa mkate wa neno la
Mungu.(Rejea Deut.8:3) Ndio maana katika somo la kwanza, Musa aliwaambia
makutano: utaikumbuka njia ile yote ya Bwana, Mungu
wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwani… akakuacha uone njaa,
akakulisha kwa mana, usiyaijua wewe wala baba zako hawakuijua, apate
kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu bali huishi kwa kila litakalo
katika kinywa cha Bwana.
Wapendwa Neno la Mungu ni Kristo
ambaye katika Injili ujidhihirisha kwa wayahudi na kwetu leo nakusema: Mimi ni Chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni,
mtu akila Chakula hiki, ataishi milele…. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu
yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake… Basi wapendwa atuna budi
kutafuta neema apa na pale, yatupasa kutambua kwamba Ekaristi ni Yesu Mwenyewe.
Na kila mara Padre anapo adhimisha misa ni Yesu Mwenyewe anaadhimisha, ni Yesu
Mwenyewe hutoa neema na nguvu za kutuwezesha kuishi Imani yetu. Sasa wakati
unapoanza kujitenga kushiriki Ekaristi ao unaposhiriki Ekaristi bila Imani na
kwa mazoea tambuwa kwamba ni mwanzo wa mateso na maanguko yako. Sasa wewe na mimi
leo tutambuwe kwamba Ekaristi ni Shukrani pia ni sala na kilele cha sala zote. Hakuna njia nyingine ya kukutana na Mungu yenye undani na ukuu zaidi isipokuwa
Ekaristi Takatifu ndio maana Yesu anasema: Kama vile
Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba, kadhalika naye mwenye
kunila atakuwa hai kwa mimi.
Tena Kanisa inatufundisha kwamba
kwa njia ya Liturjia, hasa sadaka takatifu ya Ekaristi, latimizwa tendo la
ukombozi wetu. Liturjia inasaidia kikamilifu waamini waonyeshe katika maisha
yao na kuwadhirishia wengine fumbo la Kristo na pia maumbile halisi ya Kanisa
la kweli. Kusudi kutimiza tendo kubwa namna hii, Kristo yupo daima katika
Kanisa lake, kwa jinssi ya pekee katika maadimisho ya kiliturjia. Yupo kwenye
Sadaka ya Misa katika nafsi ya Kasisi, Yeye ambaye, akijitoa mara moja
msalabani, anajitoa tena mwenyewe kwa huduma ya mapadre. Yupo hasa chini ya
maumbo ya Ekaristi. Baasi wapendwa, Kama Ekaristi ni Karamu basi inatupasa
kabla ya kesherekeya karamu hiyo fufanya matayarisho ao maandalizi ya kiroho na
kimwili kusudi tujaliwe neema itakalo kwa Kristo Kohani Mkuu. Tuwe katika hali gani
tunapoijongea meza ya Bwana? Leo hii tuna kumbushwa kuwa tunapo ijongea meza ya
Bwana, tuijongee tukiwa katika mapenzi mema. Yaani tusiijongee kwasababu ya
mazoea, majivuno, wala kwa kuwapendeza watu, bali kwa nia ya kumpendeza Kristo,
kuunganika naye na kupata dawa ya kuushinda udhaifu. Kusudi tuhudumishe upendo
na umoja kati yetu na Mungu na pia kati yetu sisi kwa sisi kama wakristo. Kupokea
Ekaristi kwasababu ya mazoea, majivuno, kujionyesha ni kufuru kwa Ekaristi
Takatifu. Kupokea Ekaristi ukijua kuwa unadhambi ya mauti moyoni ni kufuru.
Basi tunaposherekea sherehe
Ekaristi Takatifu tunakumbushwa kuwa sisi sote tumealikwa kushiriki Ekaristi
Takatifu ambayo Bwana wetu Yesu Kristu anasema kuwa ni mwili wake na damu yake.
Chakula hiki kinatolewa kwa ajili yetu kinatupatia uzima wa milele. Kwa hiyo
kila mmoja wet ni mshiriki wa sherehe hii: kwa kusoma, kuimba, kiitikia wakati
unatuhusu kutikia na kukaa kimia wakati tunaitajika kukaa kimia: basi wapendwa
yatupasa kufanya mandalizi kabla ya kuja kushiriki katika Karamu hii ya wokovu
wetu: tambua kuwa unaposoma ni Kristo Mwenyewe anasema kupitia wewe, mtu
anapobatiza, ni Kristo mwenyewe anayebatiza, wakati padre anaadhimisha Misa ni
Kristo mwenyewe alie Kohani Mkuu huadhimisha misa kupitia padre basi maandalizi
ni ya muhimu sana kwa kuboresha misa na liturijia nzima ya Kanisa letu. Ndio
maana Paulo katika somo la pili utuonesha wazi kwaamba: kwa kuwa mkate ni mmoja,
sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule
mkate mmoja. Basi tumwombe Mwenyezi Mungu atujalie kwa njia ya Mwanaye Yesu
Kristo Bwana na Mwokozi wetu na katika Umoja wa Roho Mtakatifu tujaliwe neema
na baraka katika sherehe hii ya leo.
SHALOOM
SHEMASI
BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS
Commentaires