MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA
MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA
A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO,
ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA
MASOMO
Somo I: Ex. 34: 4b-6, 8-9
Somo
II:
2Cor. 13: 11-14
Injili: John/Jean 3:
16-18
SALA: Ee
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja, mwenye Upendo na Uzima, tunakuja mbele yako leo
kukusifu na kukushukuru kwa ajili ya Uwepo wako katika Maisha yetu, basi
tunakuomba uwajalie upendo, amani na masikilizano familia zote, ndoa zote na
jamii zote ambayo zinaishi katika shida, vita, ungovi, wivu, migogoro na
ubaguzi…tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao anayeishi na
kutawala nawe na Roho Mtakatifu, Mungu
daima na milele. Amen.
UTANGULIZI
Wapendwa
Taifa la Mungu: SHALOOM. Baada ya
kusherekeya msimu mzima ya mafumbo ya wokovu wetu yaani Pasaka na pia baada ya
kupokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, leo Mama Kanisa utupa nafasi ya
kumtukuza na kumshukuru Mungu ambaye kwa imani yetu ni Mmoja katika Nafsi Tatu.
Sherehe ya Utatu Mtakatifu kwetu sisi wakristu ni kiini cha imani yetu na
inachukua nafasi ya pekee katika historia ya uumbaji na wokovu wa ulimwengu
mzima ambaye ulijengwa katika Neema yaani Upendo wa Mungu kwetu sisi. Basi
tunao sababu ya kumpa Mungu sifa ambaye ni Mmoja katika Nafsi Tatu(3). Tumwombe Mungu atupe Uwezo katika adhimisho ya siku ya leo kusudi tuweze kutambuwa mafumbo matakatifu ya imani na matumaini yetu. Pia tuwaombea wote ambao kwa namna moja ao nyingine ushindwa kuelewa na kusadiki mafundisho ya Mama yetu Kanisa ili Mungu awaongoze katika fikra zao kusudi waweze kuonja upendo na umoja wa Mungu katika maisha yao.
UFAFANUZI
Bila
shaka Sherehe ya leo uwa nawapa watu wengi changamoto kwanza kwa kuelewa na
pili kwa kutowa ufafanuzi sahihi ambayo unaweza kufasiria wazi izi Nafsi tatu
katika Mungu Mmoja. Wengine kwa sababu ya mchanganiko wa makanisa na dini,
wanashawishika na kuhisi kwamba sisi wakatoliki tunaabudu miungu mitatu(3).
Jibu ni kwamba APANA. Sisi kama wakristu
wakatoliki tunakiri imani kwa Mungu Mmoja TU katika Nafsi Tatu: Umoja usiopimika wa nafsi hizi
utuonesha wazi UMOJA NA UPENDO wa Mungu wetu. Basi kwa uweza wa Mungu
Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, nakwalika wewe ambaye utasoma
homelia hii ujaliwe faraja, amani na baraka katika maisha yako ya imani,
familia yako, kazi na shuguli zako mbalimbali kusudi kwa msaada wa Mungu Mmoja
ujaliwe neema ya kuelewa vizuri mafumbo haya matakatifu ya imani yetu.
Wapendwa
katika Barua ya Mtakatifu Paulo Mtume kwa Warumi(Romain) sura(chapitre) ya 10:
17-18 tunasoma kamaifatavyo: Basi imani, chanzo
chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema: Je, wao
hawakusikia? Naam, wamesikia, sauti yao imeenea dunia mwote, na maneno yao na
fahamu nitawaghadhibisha. Wapendwa Paulo Mtume anatufunza kwamba
imani yetu chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo: maana
yake bila kusikiliza neno la Kristo sisi leo atuwezi kushuhudia Uzima, Upendo
na Huruma wa Utatu Mtakatifu kwetu. Kila mmoja wetu lazima aipe neno la Mungu
nafasi katika maisha yake kusudi aweze kupewa neema ya kuimarisha imani yake. Tutambuwe kwamba wengi kati yetu uwa najiuliza kuwa Utatu
Mtakatifu unamsingi gani katika Biblia? Tunaweza kupata ufafanuzi wa kibiblia
ambao unaweza kutusaidia kuelewa huyu Utatu Mtakatifu? Na kwa nini Utatu
Mtakatifu?
Kabla
ya kujibu maswali hizi, lazima kufahamu kwamba Utatu Mtakatifu ni Fumbo la
imani. Ndio maana Waebrania(Hebreux) sura(chapitre) ya 11: 1 usema hivi: Basi imani ni kuwa na hakika
ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyookekana. Kwa hiyo
tunaitaji ufunuo zaidi wa Mungu Mwenyewe kusudi tuweze kuelewa mafumbo yake.
Kwanza
katika
lugha ya Agano la Kale(Ancien Testament), inafamika kuwa Mungu yaani Yahweh ni
Mmoja na wa Upekee Kabisa. Tusome Kitabu cha Kumbukumbu la Torati(ama Deutéronome)
6: 4: Sikia, ee Israeli: Bwana, Mungu wetu, Bwana
ndiye Mmoja. Ni Mungu wenye Wivu wala hakubali miungu mingine.
Tusome kitabu cha Kutoka(Exode) 20: 3-5: Usiwe na
miungu mingine ila mimi. Usifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu
chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini dunia, wala kilicho majini
chini ya dunia. usivisujudie wala kuvitumikia. Kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu
wako, ni Mungu mwenye Wivu... Basi wapendwa,
tukibaki katika mtazamo ma maneno haya tunaweza kusema kuwa neno Utatu
Mtakatifu aipo katika Agano la Kale. Lakini tukiendelea kusoma Biblia
yaani Agano la Kale tutaona kwamba licha neno Utatu Mtakatifu aipo katika Agano
la Kale lakini mawazo ambao yanaweza kutoa ufafanuzi wa neno Utatu Mtakatifu yapo.
Ndio maana Kanisa katoliki lina tumia Biblia, Mapokeo( Tradition) na
Viongozi wake(Papa na Maaskofu wezanke) kwa kuimarisha imani ya waamini.
Basi wa baba wa kanisa katika Mapokeo (ya kanisa) walitafsiri baadhi ya
vipengele vya Agano la Kale na kuunda wazo kuusu Utatu Mtakatifu ambao ni kiini
cha imani yetu sisi wakristu. Kwanza walitambuwa kwamba kuna baadhi ya
vipengele vya Agano la Kale ambao vinaonesha wazi Mungu akiongea katika UWINGI: kwa hiyo wakatoa wazo kwamba katika Mungu
kuna nafsi zaidi ya Mmoja:
Basi tusome Kitabu Cha
Mwanzo(Genesis) 1: 26: Mungu akasema, “Natufanye mtu
kwa mfano wetu, kwa sura yetu... tena katika Gen.3: 22 tunasoma
hivyo: Bwana Mungu akasema, “Basi, huyu mtu amekuwa
kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya, na sasa asije akanyosha mkono wake
akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele.” Tena
ukiendelea kusoma Gen.11: 6-7 utasikia kama ifatavyo: Bwana akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao
ni moja, na hayo ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno
wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachufulie usemi wao ili
wasisikilizane maneno wao kwa wao.” Pia katika kitabu cha nabii
Isaya 6: 8 utupa pia ufafanuzi: Kisha nikaisikia
sauti ya Bwana, akisema, “Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili
yetu?” Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nitume mimi.” Basi wapendwa
hizi ni baadhi(yaani versets ni nyingi) ya vipengele katika Agano la Kale ambao
utupa picture ya wazo la Utatu Mtakatifu.
Pili katika mafundisho ya Kanisa letu utimilifu wa Agano la Kale ni Agano Jipya.(Nouveau
Testament). Ndio maana Katika Agano Jipya tunao sababu ya kutosha kuusu wazo
la Utatu Mtakatifu. Agano Jipya utufundisha wazi habari ya Yesu Kristo ambaye
ufunua katika kazi, matendo na maisha yake Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu.
Kristo anakuwa kwetu kio ambao tunaona Umoja na Upendo wa Mungu katika Nafsi
Tatu(3). Biblia yaani Agano Jipya ujaa na mawazo ya Utatu Mtakatifu. Kwanza tukianza
na Injili ya Mathayo3: 13-17, Marko1: 9-11 na Luka3: 21-22 tunaona Ubatizo wa
Yesu ambao umetupa ufunuo wa Utatu Mtakatifu: Ikawa,
watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu
zilifunuka, Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua,
sauti ikatoka mbinguni, “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu, nimependezwa nawe.
Na katika ushuhuda wa Utatu Mtakatifu katika injili hizi tatu( synoptic) upo
zaidi katika Injili ya Mathayo 28: 19: ambao tulipewa siku ya Kupaa(Ascension) Yesu
mbinguni mamlaka ya kuwabatiza watu wote katika Utatu Mtakatifu: Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,
mkiwabatiza kwa jila la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Basi
wapendwa katika injili hizi tatu sakramenti ya Ubatizo utuonesha wazi Ufunuo wa
wokovu wetu ambao unaanza kwa kuzaliwa mara ya pili katika maisha yetu. Kwa
hiyo Utatu Mtakatifu ni Uzima na kwa sakramenti ya ubatizo mimi na wewe
tulipewa Uzima wa Mungu. Ndio maana Yesu alimwambia Nicodemo: “Amin, amin, nakuambia: mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,
hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.”(Jean/John3: 5) Lakini, Injili ya Mtume Yohane
utuonesha zaidi kuusu Utatu Mtakatifu. Mwanzoni kabisa wa Injili hii tunaona
wazo kuusu Utatu Mtakatifu. Ndio maana katika sura ya 1 hadi ile ya 12, Yohane
utuonesha wazi usiano wa Mungu Mwana na Mungu Baba. Na katika sehemu ya pili ya
injili hii yaani kuanzia sura ya 13-17, Yohane ufasiria wazi ujio wa Roho
Mtakatifu.(Jn14: 16) ambaye ametoka kwa Baba. (Jn15: 26), anatumwa na Yesu
Kristo(Jn16: 7) ambaye Kazi yake ni kutufundisha yote, na kutukumbusha yote
tulioambiwa na Yesu. (Jn14: 26). Ni Roho wa Ukweli ambaye anakuja kumshuhudia
Kristo.( Jn15: 26 na 16: 13). Kwa hiyo Yohane 14: 26 kwa kifupi utupa picture
kamili ya Mungu Roho Mtakatifu: Lakini ni huyu
Mzaidizi, huyu Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu,
atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote nilivyowaambia.
Tena sura ya 17 ya Injili ya
Yohane utuonesha utukufu wa Baba na Mwana. Na utukufu huyu ni wokovu ambao
Yohane ufundisha kama Uzima. Ndio Yohane 17: 3 utufundisha kama ifatavyo: Na uzima wa milele ndio huu: wakujuwe wewe, Mungu wa pekee wa
Kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Basi wapendwa Katika Injili ya
Yohane tunafunzwa kuwa Utatu Mtakatifu ni Upokeayaji wa Uzima katika Maisha
Yetu. Kwa hiyo Uzima wetu upo katika kumjuwa Yesu ambaye ni Uzima kwa sababu
Uzima wake umetoka katika Uzima, Mungu katika Mungu, Mwanga katika Mwanga. (Jn17:
7). Na hio uonesha Upendo na Umoja wa Utatu Mtakatifu Kwetu. Ndio maana katika
waraka wa Kwanza wa Yohane 4: 2: katika hili mwamjua
Roho wa Mungu: kila Roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili
yatokana na Mungu. Pia katika 1Jn5: 8 tunasoma: kwa maana wako watatu washuhudiao: Roho, na Maji na Damu, na
watatu hawa hupatana kwa habari moja.
Basi Yohane utuonesha wazi kwamba
Nafsi hizi tatu katika Mungu Mmoja hufanya kazi pamoja na katika upendo
usiopimika ao kutenganishwa na mtu yeyote. Kwa hiyo Utatu Mtakaatifu ni mfano wa
Upendo, Umoja na Masikilizano usiokuwa na mipika katika ulimwengu wetu. Na hio
ndio Sakramenti ya Eukaristi ambayo kwetu sisi ni Alama ya Upendo na Umoja wa
Mungu kwetu: Mungu kwa upendo wake umtowa Mwanae Mpendwa kuwa sadaka ya wokovu
wetu kusudi tusafishwe na kurudishwa katika umoja wa kimungu. Ndio maana Paulo
anakasia na kuonesha Upendo huo kwetu katika waraka wake kwa Wagalatia 4: 4: Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe
ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao
waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate hali ya kuwa wana.(
Tusome pia Rom1: 3-7, Rom8: 3-17, 1Cor12: 4-6, 1Cor8: 2, 2Cor3: 17, Col 2:
9...)
Basi wapendwa, Paulo pia utufunza
wazi katika Barua zaka kwamba Utatu Mtakatifu, kwanza unaonesha kazi ya Mungu
katika historia ya wokovu ya Mwanadamu na pili mwendelezo wa kazi hii ya wokovu
wa Mungu katika Kanisa letu Katoliki la Mitume ambalo msingi wake ni Utatu
Mtakatifu. Ndio maana 1Cor 12: 4-6 utujuza hivi: Basi
pana tofauti za Karama, bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na
Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule
azitendaye kazi zote katika wote. Basi wapendwa kwa kumailzia, Mitume katika
kitabu cha Matendo ya Mitume, utuonesha wazi kwamba Utatu Mtakatifu ndio msingi
wa Mahubiri yao.(Acts2: 14-36ff) ambao katika kitabu cha Ufunuo wa Yohane ama
Apocalypse tunakiri kwamba Mungu ana mwanzo wala Mwisho: Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, asema Bwana Mungu,
aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. (Apocalypse1:8)
Tunajifunza nini
katika Biblia na Mapokeo ya Kanisa?
Kwanza tutambuwe kuwa, tunapo
sherekeya Utatu Mtakatifu, tunasherekeya Utukufu, Upendo na Umoja wa Mungu
katika kazi yake ya Uumbaji na wokovu ambaye Yesu Kristo ni kio, ni Njia, Uzima
na Ukweli kwani kupitia Yeye Ulimwengu mzima hushuhudia kazi hio ya Utatu
Mtakatifu. Pili Utatu Mtakatifu ni kielelezo kwetu cha Uzima, ambao
tunashirikishwa na Yesu kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu katika upokeaji wa
Sakramenti ya Ubatizo ambao mimi na wewe tulipewa nafasi ya kushiriki tena
pamoja Na Mungu na kuonja tena Neema yake. Tatu Utatu Mtakatifu ni kielelezo
cha Upendo-Umoja, wa kimungu katika Maisha, familia, shughulu, wokovu
wetu(Maisha yetu nzima), ambao katika sakramenti ya Eukaristi tunafundishwa
kupendana kama vile Kristo alivyo tupenda, kuishi umoja kama vile Kristo uwa
katika Umoja na Baba na Roho Mtakatifu. Basi wapendwa kwa kubatiwza kwetu na kwa
ushiriki wetu katika meza ya Bwana, sisi kama wakristu tunapewa Uzima wa milele
na Upendo ambao utokalo kwa Utatu Mtakatifu. Kwa hio katika Sakramenti hizi tunaonja
kazi ya Utatu Mtakatifu katika Maisha yetu. Ndio maana Juma ijao tutasherekeya
sherehe ya MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU
KRISTO.
Tufanye nini kusudi Tushiriki katika Uzima, Umoja na Upendo huo wa Utatu
Mtakatifu? Jibu lipo katika masomo yetu ya leo: Masomo yetu ya leo
usisitizia zaidi kuusu neno UPENDO, neno UMOJA, neno AMANI.
Katika somo la kwanza katika kitabu cha Kutoka 34 Musa anakutana na Mungu, na katika
tokeo la Bwana, Musa alitakaswa na akalitangaza jina la Bwana... pia Musa
anatambuwa kuwa watu aliopewa na Mungu wa na shingo ngumu kwa hiyo Musa
anamwomba Mungu aende kati yao, awasamehe uovu na dhambi zao kusudi wakuwe
warithi wa Mungu. Wapendwa, ni wangapi leo wanamwomba Mungu kusudi awasamehe
wale ambao kwa namna moja ao nyingine wamepotea kiimani licha tu ya maisha
magumu, shida, njaa, umaskini, kutopata ndoa, watoto, kazi, amani... Musa
utufundisha leo kupitia wana wa Israeli kwamba hata sisi leo tunaishi katika
shingo ngumu, tunamioyo migumu kwa hiyo tumwombe Mungu aliye Upendo, Uzima,
Amani kusudi tupate faraja na neema ya kuitwa wana wa Mungu.
Ndio maana katika Injili Yesu
anamwambia Nicodemo kwamba Mungu ni Upendo na Kwa Upendo huo alimtuma Yeye
kusudi alinusuru ulimwangu lakini sio kulihukumu. Yesu anataka kutuambia leo kwamba,
tusiwe sababu ya kutoa hukumu kwa wezentu kwa ajili ya maisha yao: tupo wengi
ambao tunaona tu mabaya na matatizo ya wenzetu huku tukijifanya kuwa
watangazaji wa maisha ya wenzetu popote tulipo. Yesu anakwambia leo: tangaza
neno la Mungu, neno la upendo, amani na umoja kwa watu, kwa wezentu,
majirani... kusudi wapate kuonja upendo na uzima wa Utatu Mtakatifu, pia tuwe
mfano bora wa Uzima na Upendo huo, tusiwe chanzo cha kukatisha wengine tamaa ya
kumfuate Yesu. Basi tutafanya haya yote kama tu tunaishi katika upendo, amani,
umoja, tukifarijiana, tukisalimiana kwa busu takatifu na mwishoni neema ya
Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu na ushiriki wa Roho Mtakatifu utakaa ndani
yetu nyote. Huu ni ujumbe mahususi ambao tunaoupata katika somo la pili.(2Cor.
13: 11-41)
Wapendwa, Yesu kupitia Mtume
Paulo utusihi tuzingatie sifa hizo kusudi tupate neema ya Utatu Mtakatifu. Wewe
baba, wewe mama leo unaisha katika kuzingatia sifa hizo ndani ya familia yako?
Kama sivyo, kwa nini? Mbona unamdanganya mpezi wako na kuishi maisha isio ya
ukweli mbele yake? Leo hii ndoa mbali mbali zinapata changamoto nyingi licha tu
ya kutokuwa waaminifu katika mambo madogo madogo, waaminifu katika agano letu
ya ndoa: na madhara ya hizo tabia mbaya ni ugonvi, talaka, migogoro, utekelezaji
wa watoto katika ulimwengu wetu wa kisasa...uzima, upendo na umoja ambao
tunashirikishwa na Utata Mtakatifu katika sakramenti ya Ubatizo na Ekerasti
vipo wapi? Tupo wengi leo katika kazi zetu tunashindwa kuonesha umoja na upendo
sababu tu wale ambao tunafanya nao kazi sio wa kabila letu, sio wa province ama
mkoa wetu, sio ndungu zetu... madhara ya tabia kama hizo mbaya ni ubakuguzi,
ukabila na unyanyazaji katika maisha yetu ya kibinadamu... leo hii kuna baadhi
ya watoto ambao wanashindwa kuwaheshimu wazazi wao kwa sababu ni maskini na sio
wasomi... tambuwa kwamba Mzazi anabaki kuwa mzazi wala hauwezi kubadilishwa,
wala upendo wake kwako hawezi pimika kwa sababu ya umaskini: madhara ya hizi
tabia ni kupiga wazazi, kuwashika uchawi, na kugawanyana katika familia... kwa
kifupi familia zetu zote zinaishi katika shida kubwa kwa sababu ya kutokuwa na
upendo, amani na umoja... Basi wapendwa tunapo sherekeya sherehe ya Utatu
Mtakatifu tujifunze kuishi Umoja na Upendo ambao utuonesha asili ya Mungu kwetu
ambaye ni Mmoja katika Nafsi Tatu.
SHALOOM: MUNGU
AWABARIKI KATIKA MAISHA, KAZI NA FAMILIA ZENU
SHEMASI
BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS
Commentaires