MAHUBIRI YA SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A WAKANISA: ROHO MTAKATIFU HULITAKATIFUZA KANISA MASOMO Somo I : Acts 2:1-11 Somo II: 1Cor 12:3b-7, 12-13 Injili: John/Jean 20:19-23 SALA: Ee Mungu Baba Mwenyezi, kwa ushirika wa Yesu Mkombozi wetu na kwa uwepo na nguvu ya Roho Mtakatifu, Kanisa lako lilitakatifuzwa, basi ee Baba tunakuomba, utusaidie sisi viungo vya Kanisa lako kusudi tubaki waaminifu kwa kulishika Neno na Amri yako. Uwatakase na kuwalinda Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen. UTANGULIZI Taifa la Mungu, SHALOOM: wapendwa leo tunao furaha ya kuhitimisha mahadhisho ya sherehe ya Pasaka ambalo kiliturgia leo tunahesabu siku 50 tangu tulipoanza kusherekea mafumbo ya wokovu wetu yaani: Kuteswa, Kufa, Kufufuka na Kupaa Mbinguni Bwana wetu Yesu: Ndio sababu leo ni Sherehe ya Pentekoste maana yake ni “ siku ya hamsini ”.(50 th ) Ni siku ya hamsini tangu tulipo sherehekea Jumapili ya Pasaka yaani Jumapili ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo: B...
MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA MASOMO Somo I: Ex. 34: 4b-6, 8-9 Somo II: 2Cor. 13: 11-14 Injili: John/Jean 3: 16-18 SALA: Ee Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja, mwenye Upendo na Uzima, tunakuja mbele yako leo kukusifu na kukushukuru kwa ajili ya Uwepo wako katika Maisha yetu, basi tunakuomba uwajalie upendo, amani na masikilizano familia zote, ndoa zote na jamii zote ambayo zinaishi katika shida, vita, ungovi, wivu, migogoro na ubaguzi…tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu, Mungu daima na milele. Amen. UTANGULIZI Wapendwa Taifa la Mungu: SHALOOM . Baada ya kusherekeya msimu mzima ya mafumbo ya wokovu wetu yaani Pasaka na pia baada ya kupokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, leo Mama Kanisa utupa nafasi ya kumtukuza na kumshukuru Mungu ambaye kwa imani yetu ni Mmoja katika ...
MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA Somo I : Kut 12 : 1-8, 11-14 Somo II : 1Kor 11 :23-26 SomoIII: Yohane 13:1-15 SALA: Tuwaombee mapadre wote ili Mungu awajalie juhudi na ujasiri wa kuwahudumia Taifa lake lote bila ubaguzi wa rangi ao wa taifa tena wabaki imara katika wito wao kila siku ya maisha yao. UTANGULIZI Leo Mama Kanisa anaadhimisha Alhamisi Kuu , mmja kati ya siku kuu tatu kabla ya kusherekeya mafumbo ya imani na matumaini ya wokovu wetu sisi wakristu: ndiyo Pasaka ya Kikristo yaani kuteswa, kufa na kufufuka Bwana wetu Yesu Kristu . Katika ukumbusho wa siku ya leo Bwana wetu Yesu Kristo pamoja na wanafunzi wake, saa chache kabla ya kukamatwa na kuhukumiwa kifo, alikula karamu ya mwisho. Katika karamu ya mwisho, alionyesha mfano wa kuishi Amri ya Mapendo na akaweka Sakramenti mbili muhimu kabisa ndizo: Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Sakramenti ya Daraja Takatifu (...
Commentaires