MAHUBIRI YA SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A WAKANISA: ROHO MTAKATIFU HULITAKATIFUZA KANISA MASOMO Somo I : Acts 2:1-11 Somo II: 1Cor 12:3b-7, 12-13 Injili: John/Jean 20:19-23 SALA: Ee Mungu Baba Mwenyezi, kwa ushirika wa Yesu Mkombozi wetu na kwa uwepo na nguvu ya Roho Mtakatifu, Kanisa lako lilitakatifuzwa, basi ee Baba tunakuomba, utusaidie sisi viungo vya Kanisa lako kusudi tubaki waaminifu kwa kulishika Neno na Amri yako. Uwatakase na kuwalinda Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen. UTANGULIZI Taifa la Mungu, SHALOOM: wapendwa leo tunao furaha ya kuhitimisha mahadhisho ya sherehe ya Pasaka ambalo kiliturgia leo tunahesabu siku 50 tangu tulipoanza kusherekea mafumbo ya wokovu wetu yaani: Kuteswa, Kufa, Kufufuka na Kupaa Mbinguni Bwana wetu Yesu: Ndio sababu leo ni Sherehe ya Pentekoste maana yake ni “ siku ya hamsini ”.(50 th ) Ni siku ya hamsini tangu tulipo sherehekea Jumapili ya Pasaka yaani Jumapili ya Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo: B...
MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA MASOMO Somo I: Ex. 34: 4b-6, 8-9 Somo II: 2Cor. 13: 11-14 Injili: John/Jean 3: 16-18 SALA: Ee Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja, mwenye Upendo na Uzima, tunakuja mbele yako leo kukusifu na kukushukuru kwa ajili ya Uwepo wako katika Maisha yetu, basi tunakuomba uwajalie upendo, amani na masikilizano familia zote, ndoa zote na jamii zote ambayo zinaishi katika shida, vita, ungovi, wivu, migogoro na ubaguzi…tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu, Mungu daima na milele. Amen. UTANGULIZI Wapendwa Taifa la Mungu: SHALOOM . Baada ya kusherekeya msimu mzima ya mafumbo ya wokovu wetu yaani Pasaka na pia baada ya kupokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, leo Mama Kanisa utupa nafasi ya kumtukuza na kumshukuru Mungu ambaye kwa imani yetu ni Mmoja katika ...
DOMINIKA YA MATAWI AO DOMINIKA YA MATESO MWAKA A MASOMO Somo I: Isa . 50:4-7. Somo II: Flp . 2:6-11. Injili: Mt . 26:14-27:66 SALA : Ee Bwana tunakushukuru kwa wema na upendo wako mkuu kwa kumtoa Mwanao Mpendwa Yesu Kristu kuwa sadaka kwa ajili ya wokovu wetu basi e Bwana tunakukabidhi watu wanaoteseka na ugonjwa wa virusi vya Korona: Ee Mungu Baba yetu pokea marehemu wote kaika ufalme wako. UFAFANUZI WA DOMINIKA YA MATAWI Ndugu zangu katika Kristo, tangu jumatano ya majivu tulianza kipindi cha Kwaresima kipindi ambacho Mama Kanisa anatualika kututafakari kwa kina mafumbo ya wokovu wetu. Katika kipindi hiki tunaungana na Yesu katika safari yake ya ukombozi, kwa kufunga, kusali na kutenda matendo ya huruma kwa maskini, wanyonge na jirani zetu. Basi leo Mama Kanisa anahadhimisha Dominika ya Matawi dominika amboyo inatuingiza taratibu katika kilele cha imani na matumaini yetu kusudi tukumbuke na kutafakari pamoja lile fumbo la Pasaka la Bwana wetu Yesu Kr...
Commentaires