MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 13 YA MWAKA A WA KANISA WAKATI WA KAWAIDA: UKARIMU WAKO UTAKUFANYA WEWE UZIDI KUBARIKIWA NA MUNGU
MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 13 YA MWAKA A WA
KANISA WAKATI WA KAWAIDA: UKARIMU WAKO
UTAKUFANYA WEWE UZIDI KUBARIKIWA NA MUNGU
MASOMO
SOMO I: 1Fal. 4:8-11, 14-16
SOMO II: 2Rom: 6:3-4, 8-11
INJILI: Mt. 10:37-42
SALA: Ee Baba yetu Mwema, ulituumba kwa
sura na mfano wako kusudi tushiriki katika upendo na utukufu wako pia Mwanao
Yesu Kristo Mungu na Mkombozi wetu kwa kufa na kufufuka kwake sisi tulijaliwa
maisha mapya ambao kwa nguvu na msaada wa Roho Mtakatifu Kanisa inaendelea
kuwakirimia watoto wake kwa njia ya sakramenti na huduma mbali mbali. Basi Ee
Mungu wetu utusaidie kwanza kukupenda Wewe na Yesu Kristu kusudi tujifunze
kuboresha upendo huu katika familia, taifa na dunia nzima hasa zaidi wakati huu
ambao tunapambana na janga hii ya vimelea vya Corona. Tunaomba hayo kwa njia ya
Kristu Bwana wetu. Amen.
UTANGULIZI
Wapendwa Taifa la Mungu SHALOOM, TUMSIFU YESU KRISTO: leo tunaadhimisha
Dominika ya 13 ya Mwaka A wa Kanisa (Kanisa letu Katoliki) katika kipindi cha
kawaida. Katika Dominika hii ya leo: Yesu anatukumbusha kwamba bila Yeye katika
maisha yetu sisi hatuwezi kupata mafanyikiyo na Ufalme wa Mbinguni. Yohane 17:
3 utufundisha kwamba: na uzima wa milele ndio
huu: wakujue Wewe, Mungu wa pekee wa Kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Na pili Dominika ya leo inatufundisha pia bila Ukarimu katika maisha
yetu ni vigumu sana kuona baraka na utukufu wa Mungu. Basi ndugu yangu, Yesu
anakuambia leo kwamba Yeye Mtendaji na Mzimamizi katika Maisha yako kuliko
wanadamu na vitu unavyo: tambuwa kwamba wazazi, marafiki, mali ao utajiri,
elimu, maisha na uzima... unavyo ni mali yake Mungu basi umpe kwanza Mungu
nafasi ya kwanza katika maisha nawe utashuhudia mkono wake wa baraka katika familia,
shughuli, kazi, urafiki... wako. Basi leo kila mmoja wetu amwambiye Yesu aje
apenye moyo wake kusudi tutambuwe udhaifu wetu ili tuchukue hatua ya kumfuata
kwa ukweli kila siku ya maisha yetu.
UFAFANUZI
WA MASOMO YETU
Wapendwa katika KATEKESIMU ya
Kanisa letu Katoliki tunafundishwa kwamba Ndoa ambao inatunga familia asili
yake ni Mungu Mwenyewe(Gen. 1:28): kwa hiyo Baba na mama huanzisha kwa
makubaliano yao jumuiya ao familia mpya katika mapenzi yake Mungu. Kwa hiyo
mapendo ya mume na mke na uzazi wa watoto huanzisha kati ya watu wa familia
moja uhusiano wa pekee na uwajibikaji wa kwanza. Basi Mungu kwa kuwaumba
mwanamume na mwanamke alianzisha familia ya kibinadamu na kuijalia katiba yake
ya msingi. Wanafamilia hawa ni binadamu walio na hadhi sawa. Basi familia ya
kikristo kwanza ni chembe ya kwanza ya maisha ya jamii: ni familia ya imani, ya
ukarimu, ya matumaini, ya upendo. Pia ni umoja wa watu ishara ya umoja wa umoja
wa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Tena kwa kazi ya uzazi na malezi ya watoto
hunurisha kazi ya Baba ya uumbaji. Kwa hiyo familia yaitwa kushiriki sala na
sadaka ya Kristo, upendo na ukarimu wa Kristo, huruma na neno la Kristo kusudi
huimarisha upendo ndani yake na ndani ya ulimwengu mzima. Na ni kwa mawazo haya
tunaweza kuelewa maandiko yetu ya leo hususani injili Takatifu.
Ndio maana katika somo la kwanza
kutoka kitabu cha 2 cha Wafalme utuonya kwamba kwa ukarimu na upendo wao, nabii Elisha anawabariki wanandao wawili ambao walikuwa tayari na umri mkubwa bila
kupata uzazi ao watoto na anawahidia mtoto. Baraka ya familia hii inatoka kwa
ukarimu wa mama huo na usikivu wa mume wake: mama huu alitambuwa kwamba nabii
Elisha ametoka nchi ya mbali na hakuwa na nyumba wala ndugu ao familia kule
endako mama huo anamkaribisha na kumuhudumia kama mmoja wao. Pia katika kitabu
cha Mwanzo sura 18: 1-15: Abrahamu kwa ukarimu wake anahaidiwa mtoto pamoja na
mke wake Sara ambao tayari walikua wakongwe kabisa. Basi wewe ambaye utasoma
mahubiri hii tambuwa kwamba familia yako ni baraka na inatoka kwa Mungu kwa hiyo
umpe Yesu kwanza nafasi ya kuitawala na kuwa msingi wa maisha yako, maisha yetu
mtakirimiwa baraka na utukufu. Wewe mama, wewe
baba wakati mnapokea wageni mnafanya nini? Mnajisikiaje? Ni nani mgeni?
Waswahili usema kwamba mgeni kila siku ni baraka.
Lakini leo tukichunguza kwa
undani kabisa ndoa ao familia nyingi zinabomoka licha tu ya kuhabudu chakula: kuna
baadhi ya akina mama ambao wanashindwa kutambuwa ndugu wa waume zao kwa sababu
tu ya uchoyo, ubinafsi, tamaa na ubaguzi... wakitazama chakula kama kitu cha
muhimu kuliko hata Yule ambaye anayewajalia uzima, chakula na nguvu. Maana wakiwaona
wageni wanashikwa na hasira na chuki hadi kutenda matendo ambao kijumwiya
hairusiwi kama kubadilisha maji ya ugali na kuyafanya kuwa maji ya kuwaogesha
watoto ambao tayari walikua wamesha kuoga na wasafi licha tu kutokuwa na
ukarimu... kutumia lugha chafu na kushuhudia uwongo, kupiga watoto na matusi
licha tu mgeni atambuwe kwamba hapa nilipo hakuna amani ili ajiandae
kuondoka... Wengi ni akina baba ambao ushindwa kujitambuwa mbele ya chakula na kutambuwa kazi yao kama baba ndani ya
familia na kuifanya familia yao kama sehemu ya utumwa, mateso na shida: baba
anahesabu vipande vya samaki wengine wanajua kabisa kuku anavipande vingapi ao kuwapimia
wake zao kila siku kiasi cha unga, mafuta na kazalika... hayo yote inawafanya
akina mama kushindwa kumiliki ofisi yao kama mama na kuona mateso ya kuweza
kushiriki maisha ya ndoa...
Basi somo hili ni mfano kwangu
mimi na wewe wanandoa hawa wawe kwetu fundisho na nabii Elisha anawakilisha
Mitume, mimi na wewe na viongozi wetu wote wa dini ambao Yesu katika injili utualika
kwanza kumpenda Yeye kuliko vitu vyote. Tukiwa na Yesu maisha na ndoa zetu
zitaneemeka na kustawi katika amani, ukarimu, furaha na uvumilivu. Kumpenda Yesu
kuliko vitu vyote ni kuwa tayari kusaidiani sisi kwa sisi hasa zaidi kuwajali
wale ambao ni wadogo kabisa katika jamii yetu kama vile maskini, wangonjwa
hususani wakati huu wa Corona wengi kati yetu wanashindwa kuendelea na shughuli
zao na kupambana na mateso, magumu makali, yatima, wajane na wengine wote ambao
kwa mtazamo wetu tunawaona kama waitaji. Haya ndio mafundisho ya Yesu. Maana
imani yetu na matendo lazima viendane. Ndio maana mtume Yakobo katika waraka
wake sura 1: 14-18: imani bila matendo imekufa.
Kwa imani na matendo ya wanandoa hawa katika somo la kwanza, Mungu anawapa
furaha ambao ilikuwa itaji katika maisha yao yaani kupata mtoto.
Basi nakwambia leo: usisema
kwamba wakati umeisha na kukataa tamaa na kuhisi kwamba wewe hauwezi kubarikiwa
katika ndoa yako na kupata watoto, kuolewa ao kufanyikiwa kimaisha... tambuwa
kwamba Yesu Kristo ndiye Ngao na Mwokozi wako, wangu, wetu: wewe unaitajika
kufanya jitihada na kutafiti maisha yako ya kimwili na kiroho kusudi Yesu
Kristo apate nafasi ya kupenya moyo ao mioyo yetu tukifanya hyvio tutabarikiwa....
hauwezi barikiwa wakati wewe unazuia wengine kupata baraka, wakati unashindwa
kuwasaidia wengine... kila mmoja wetu anao chochote cha kutoa basi uwe baraka kwa
familia yako, kanisa lako, rafiki zako na uwe tayari kuwaombea wengine wapata
kubarikiwa. Basi tukifanya hivyo tutaelewa mafundisho ya Paulo Mtume katika
somo letu la pili: Hamfahamu ya kuwa sisi sote
tulibatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?... Lakini tukiwa
tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye...
Basi mkristu ni yule ambaye hutoa uhai, maisha na uzima wake kwa ajili ya wangine.
Mungu azidi kuwabariki na kuwapigania kila siku katika familia na ulimwengu
wetu huo.
SHALOOM/TUMSIFU YESU
KRISTO
SHEMASI
BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS
Commentaires