MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA MASOMO Somo I: Ex. 34: 4b-6, 8-9 Somo II: 2Cor. 13: 11-14 Injili: John/Jean 3: 16-18 SALA: Ee Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja, mwenye Upendo na Uzima, tunakuja mbele yako leo kukusifu na kukushukuru kwa ajili ya Uwepo wako katika Maisha yetu, basi tunakuomba uwajalie upendo, amani na masikilizano familia zote, ndoa zote na jamii zote ambayo zinaishi katika shida, vita, ungovi, wivu, migogoro na ubaguzi…tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu, Mungu daima na milele. Amen. UTANGULIZI Wapendwa Taifa la Mungu: SHALOOM . Baada ya kusherekeya msimu mzima ya mafumbo ya wokovu wetu yaani Pasaka na pia baada ya kupokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, leo Mama Kanisa utupa nafasi ya kumtukuza na kumshukuru Mungu ambaye kwa imani yetu ni Mmoja katika ...
Commentaires