DOMINIKA YA KWANZA YA KWARESIMA MWAKA A WA KANISA: TUMTEGEMEE MUNGU TUNAPOPATWA NA VISHAWISHI
JUMAPILI YA I YA KWARESIMA MWAKA A: MARCH 1th 2020
Masomo:
Somo I: Mwa 2:7-9, 3:1-7
Somo II: Rum 5:12-19
Injili : Mt
4:1-11
Utangulizi
Tupo katika kipindi cha
Kwaresima, na leo ni Dominika ya kwanza
ya Kwaresima katika Mwaka A wa Kanisa. Kwa hiyo mandiko matakatifu
inatufundisha kwamba ni lazima kumtegemea Mungu asa zaidi wakati tunapopatwa na
vishawishi.
Wapendwa kabla ya kutoa
tafakari ya dominika ya kwanza ya kwaresima ni lazima tukumbushane kuusu maana
ya kwaresima katika kanisa letu katoliki takatifu. Basi tukiungana na baba
Mtakatifu papa Fransisco katika waraka wake wa kwaresima wa mwaka huu aliendika hivi... yani nitafasiria
kwa kifupi tu: papa anakabizi kwanza kwaresima ya mwaka huu juu la ulinzi na
maombezi ya mama yetu Bikira Maria mama wa Mungu kusudi kwa mfano na maombezi
yake kila mja kati yetu apokee wito wa Mungu ili aungane zaidi na Mungu. Pili
kwaresima ni lazima itusaidie kutafakari kwa kina fumbo nzima ya ukombozi wetu
tuliopewa kwa upendo wa Utatu Mtakatifu kwanzia tendo ya uumbaji hadi ukombozi
wetu kwa njia ya Yesu Kristo katika ushirika wa Mungu Baba na Mungu Roho
Mtatakatifu.
Basi wapendwa ni lazima
tutambue kwamba ujumbe mku wa kwaresima ni kumtafuta Mungu zaidi kusudi ili kwa
kuwaudumia wenzetu na kuwajalia maskini
na wanyonge katika sala, kufunga na kwa kutenda matendo ya huruma tupatanishwe
na Mungu na kanisa lake nzima. Ndio sababu papa wetu anatualika tusome na
kutafakari ujumbe tunao upata katika waraka wa 2 wa mt. Paulo kwa Wakorinto
sura ya 5:20-21: Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa
vinywa Vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo: Mpatanishwe na Mungu. Yeye
asiye jua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kuwa haki ya
Mungu katika yeye.
Wapendwa tukiwa na lengo hili
katika mioyo yetu basi tutatambua kwamba Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini
za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma.
Bwana wetu Yesu Kristo kabla ya kuanza rasmi kazi yake ya kuutangaza Ufalme wa
Mungu hapa Duniani alifunga kwa muda wa siku arobaini. Baada ya mfungo huo, Bwana wetu Yesu Kristo
alishawishiwa/alijaribiwa na ibilisi lakini alibaki kuwa mwaminifu kwa Mungu
Baba yake. Tofauti na Wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Eva walioshawishiwa na
ibilisi wakaanguka dhambini. Sisi nasi tunakutana na vishawishi mbalimbali
katika maisha yetu basi tukiwa na Yesu kila siku ya maisha yetu tutashinda
vishawishi na tutabaki waminifu katika maisha yetu ya kila siku.
Wapendwa somo la kwanza mosi
linatukumbusha historia ya uumbaji wa wazazi wetu wa kwanza. Somo hili linatupa
asili ya binadamu. Mungu aliwaumba Adamu na Eva, wazazi wetu wa kwanza,
akawaweka katika bustani ya Edeni, maisha ya watu wa kwanza yalikuwa maisha ya
heri na amani. Walikaa pamoja na wanyama kwa amani wakajilisha majani na
matunda.(cf. Mwanzo 2:15-17). Pili Somo I la leo kutoka kitabu cha Mwanzo(Mwa
2:7-9, 16-18, 3:1-7) linatukumbusha kuanguka kwa wazazi wetu wa kwanza Na
madhara ya kuangka kwao yaani ya dhambi ya kwanza ni chimbuko ya kuingia kwa
dhambi ya asili na dhambi nyingine katika ulimwengu huu. Adamu na Eva walishawishiwa
na nyoka, mnyama aliyekuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu. Hii ndiyo kazi
ya shetani, kuwashawishi wanadamu wafanye mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya
Mungu. Kwa wayahudi,
neno “shetani” lilimaanisha kitu chochote kinacholeta mgongano kati ya watu,
wenyewe kwa wenyewe na hata kati ya watu na Mungu. Shetani wakati wote yu chini ya mamlaka ya Mungu (Zak
3:1-10; Joe 1-2), kwa hiyo ndugu zangu, “Tumtegemee
Mungu tunapopatwa na vishawishi.”
Wapendwa tukisoma Isaya 5:
20-21 tutasikia kama ifatavyo: ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na
kwamba wema ni uovu, watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watio
uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu. Ole wao walio wenye hekima
katika macho yao wenyewe, na wenye busara katika fikira zao wenyewe.
Wapendwa maneno ya nabii Isaya yanaweza kutupa nafasi ya kutafakari kuanguka
kwa wazazi wetu wa kwanza. Mungu alituumba katika hali ya uhuru. Na katika hali
hio binadamu alipewa nafasi ya kuchagua mema yani uhai ao mabaya yaani kifo.
Kitabu cha Mwanzo kinatupa picha ambao inaoneshwa wazi uhuru wa mwanadamu
katika kuchagua kifo badala ya uhai. Kwa hiyo mwanadamu alichagua uovu panafasi
ya wema, giza panafasi ya nuru, uchungu panafasi ya utamu na mwishoni kabisa
aliweka hekima na busara katika macho yake mwenyewe na hiyo ilikuwa kwake ole
na mwanzo wa mateso yake hadi kuchafua ulimwengu nzima.
Jambo hilo linaonesha wazi kutokujikubali
na kuthamini maisha yetu kama viumbe vya Mungu na kukataa ubinadamu wetu.
Wapendwa, tutambue kwamba, unapojikataa wewe
wenyewe ao ninapojikataa mimi wenyewe, tunafungua nafasi ya kutamani
maisha ya watu wengine yanaoweza kutusababishia madhara makubwa katika maisha
yetu. Basi Mungu anatupa nafasi tena ya kutafakari ubinadamu wetu mbele yake
hili tuweze kupiga hatua ya mabadiliko katika Maisha yetu na kumrudia yeye
aliye Mti mweye kujaa Uhai, Neema na Baraka.
Ndio sababu somo la pili kutoka
katika waraka wa Mt. Paulo Mtume kwa Warumi linatuonesha wazi ukurasa wa
uumbaji wa pili katika kuteswa, kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Basi tunafarijika na maneno ya Mungu kwetu kwamba: kwa kosa moja watu wote
walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa
haki yenye uzima. Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi
walingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa utii kwake mmoja watu
wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
Wapendwa kutokana ya Utii wa
Yesu kwa Baba yake, ulimwengu mzima uliumbwa upya kwa kifo na ufufuo wake. Basi
tutambue kwamba kwa wana wa israeli kitabu cha kutoka kina nafasi ya pekee
katika historia ya maisha yao na Mungu. Yaani ukombozi kutoka utumwani Misri ni
sehemu ya peke katika maisha yao ya imani. Lakini katika kutoka walikutana na
vishawishi na mara ninyi walishindwa kupambana na vile vishawishi... Simulizi la
kujaribiwa kwa Yesu katika Injili ya leo ni hitimisho wa nyakati mbalimbali za
majaribu katika maisha ya wana wa Mungu na katika maisha yetu sisi wana warithi
wa Mungu kwa njia ya Yesu. Ndio sababu kwetu sisi wakristu leo nilazima kwanza
kuelewa maana ya ufufuko kama chanzo cha imani yetu ili tuweze kusoma na
tutafakari vema agano jipya kusudi tutafsiri na kuelewa agano lakale. Masimulizi
haya yamefupishwa na kuwekwa mwanzoni mwa utume wa Yesu ili kuonesha kwamba,
Yesu ndiye kweli hitimisho ya Agano la kale na kweelelezo cha utii kwamba
ingawa alipatwa na majaribu yote katika maisha yake, alichagua kubaki mwaminifu
kwa Mungu.
Hali hii ya Yesu inakumbusha
ile ya waisraeli walipokuwa jangwani kwa miaka arobaini kabla ya kurudi katika
nchi takatifu yaani, nchi ya ahadi. Waisraeli hawakuwa waaminifu kwa Mungu
wakati wote, walishindwa kumtegemea Mungu walipopatwa na vishawishi au majaribu
au magumu katika maisha yao. Katika simulizi ya leo, Yesu kwanza anamshinda
shetani na kujifunguwa na kutufundisha sisi leo kwamba yeye ndiye Neno Timilifu
na Mkate wa kweli utokalo mbinguni. Sehemu hii ya jaribio la kwanza
linahitimisha kitabu cha kutoka sura ya 16 na sura 17 ambao
wana waisraeli walinungunika kuusu chakula huku wakikumbuka sufuria za nyama na
chakula walivyo kula huku Misri hadi kutupilia mbali wema wa Mungu kwao... kwa
hiyo Mungu akamwambia Musa: Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate
kutoka mbinguni... na mkate huyo ni Yesu Kristo wale sio yale chakula
kutoka Misri. Na huku wakigoma kwa sababu ya maji... Ndio sababu tukisoma
kitabu cha Kumbukumbu la Torati sura ya 8:2-3 tutasikia kama hifatavyo: nawe
utaikumbuka njia ile yote Bwana, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini
katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba
utashika amri zake au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa
mana, usiyaijua wewe wala baba zako hawakuijua, apate kukujulisha ya kuwa
mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha
Bwana. Na kwa kuhitimisha hilo Yesu anasema hivyo katika injili ya
Yohane sura ya 6: 54-56: Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu
anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni
chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywanji cha kweli. Aulaye mwili wangu na
kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
Jaribio la pili
linamtaka Yesu ajioneshe mbele ya watu kuwa analindwa na Baba yake. Shetani
naye sasa anatumia Maandiko Matakatifu kutegemeza jaribio lake. Katika Zaburi
91:11-12, Mungu anaahidi kuwatuma malaika wamchukue mtumishi wake asije
akajikwaa kwenye jiwe. Yesu hana shaka na ulinzi utokao kwa Baba yake. Lakini
anakataa kutumia uwezo wa Baba yake bila sababu ya maana. Hataki kujitia
mwenyewe katika hatari ili aoneshe uwezo wake. Kufanya hivyo ingekuwa ni
kutumia vibaya uwezo wa Mungu. Kwa hiyo, Yesu alimjibu shetani akamwambia: “Usimjaribu Bwana Mungu wako” (Kumb
6:16).
Jaribio
la tatu linamtaka Yesu amwache Mungu na amwabudu Shetani kwa malipo ya kupata utawala wa
kisiasa. Mambo yanapofikia hatua hiyo,
Yesu hawezi kuendeleza mazungumzo na Shetani. “Nenda zako, Shetani” Yesu aliamuru. Mwana wa
Mungu hawezi kumwabudu Shetani kwa malipo
ya kiasi chochote, kwani imeandikwa, Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia
yeye peke yake.
Wapendwa katika Kristo, Simulizi la
kujaribiwa kwa Yesu linaonesha kazi ya ibilisi ya kuwajaribu watu katika kazi
zao wanazopewa na Mungu. Ibilisi anakuja kwa Yesu na kujaribu
kupendekeza njia nyingine tofauti za kufanya ile kazi aliyopewa. Njia za
ibilisi zinaonekana rahisi na za kuvutia, zenye Utukufu na ufahari. Anajaribu
kumchanganya Yesu ambaye ni Mungu na Mwokozi wetu lakini Yesu alibaki Imara na kumufukuza
mbali shetani katika kazi ya utume wake.
Wewe na mimi leo tujiulize: wakati tunapo kutana na majaribu, magumu, shida
ao mangonjwa tunaenda wapi? Leo hii wengi kati yetu wanahabudu chakula na kugawanyana
katika familia kwa sababu ya chakula: wakati umepata wageni kwa nini
unakasirika kwa sababu ya chakula hadi kuyachugua maji ya ugali na waogesha
watoto... wakati wanyonge na maskini wanakuja kwako kwa nini unashindwa
kuwasaidia? Wakati huo wa kwaresima uwe kwetu wakati wa kuwajali maskini,
yatima, wangonjwa, wafungwa uku tukiwatendea matendo ya huruma...itampendeza
Mungu kama familia siku mmja munawatembelea maskini, wazee, wafungwa na
kuwasaidia, na kuwaombea...
Leo hii magonjwa, shida na magumu mbali mbali zinatufanya sisi kumusau
Mungu hadi kukufuru na kusau upendo wake ndani yetu huku tukitanganga kutafuta
tiba kwa watu wasio na uwezo wakutuokoa katika shida hizo...wakati huu ni
vizuri kila mmja wetu, kila familia ampelekee bwana shida, mangonjwa, magumu
yake na asali na kufunga huu akitenda matendo ya huruma naye Mungu awezi
kukuacha...
Na ninyi wanafunzi, wazazi wanateseka kuwasomesha huku mama akiuza mchicha,
baba kila siku asubuhi akiamka mapema na kwenda kutafuta apa na pale kusudi
wewe uboreshe maisha yako ya kesho...sasa kwa nini tunashindwa kuwaombea wazazi
wetu na ndungu wetu wengine wanaotusaidia kusudi tusome? Kwa nini tunajisau
huku tukitamani maisha ya wengini inaozidi kipato cha familia zetu hadi
kushawishika huku tikikuza tamaa, kuanguka na kuharibu maisha yetu? Mmtafute
kwanza Yesu na kuwaombea wazazi wenu naye Mungu atawasaidia nyote...Basi ndungu
zangu tukiwa na Yesu Kristo siku zote za maisha yetu, tutamushinda muovu
shetani anaekuja kila siku katika ali mbali mbali ya maisha yetu.
Wapendwa katika Kristo,
Jumatano iliyopita, ndiyo Jumatano ya Majivu, tulianza rasmi safari yetu ya
mfungo wa Kwaresima kwa siku arobaini. Kusali, kujitoa sadaka kwa ukarimu kwa
wahitaji na kufunga, ndizo nguzo kuu tatu za kipindi cha Kwaresima. Tumesikia
katika masomo yetu ya leo habari za vishawishi au majaribu. Leo tunapewa himizo
tukiwa mwanzoni kabisa mwa kipindi cha Kwaresima, “Tumtegemee Mungu tunapopatwa
na vishawishi.”
Tumsifu Yesu Kristo
Shemasi Bienvenu
Kabeya Kungwa Ngungwa Poulain Loquace, sds
Commentaires