MAHUBIRI YA DOMINIKA YA TANO YA KWARESIMA MWAKA A
MASOMO
Somo I: Eze. 37:
12-14
Somo II: Rum. 8: 8-11
Injili: Jn 11: 1-45
SALA: Ee Bwana, tunakuja mbele yako kukusifu na kukushukuru
kwa ajali ya upendo wako mkuu kwetu: Bwana utusaidie kushinda maradhi ya Coronavirus.
UTANGULIZI
Leo Kanisa Katoliki Takatifu
inaadhimisha Dominika ya Tano ya Kwaresima basi wapendwa tuungane na kutafakari
na Bwana Wetu Yesu Kristu anaposema: Mimi ndimi huo ufufuo, na Uzima... Yeye
aniaminiye mimi, hatakufa kabisa hata milele.
UFAFANUZI
Wapendwa, leo
katika jamii yetu ya kisasa kifo bado kinabaki kuwa funguo ya ulizo: mwanadamu
ni nani? Kwa nini kufa? Kwanza tutambue kuwa kuna njia mbili ambazo wandadamu waweza
kuelezea kuusu kifo: papa Benedicto wa XVI aliandika na kutafsiri hizi njia
mbili. Alisema hivi: watu wengi zamani, na baadhi yao wapo bado leo, walifuata njia ya
watalamu ya elimu ama wanafalsafa na kujaribu kufasiriya kifo...walizani kwamba
kunamvutano kati ya mwili na roho katika mwanadamu huku mwili ukifamika kuwa
gereza ama jeneza ya roho ambao ufunguo wa gereza ao jeneza ya roho ulikuwa tu
ni kifo kwa sababu waliamini kwamba wakati kifo kimefika mwili ujifunguwa na
kuachana na roho huku roho upata nafasi ya uhuru na ya kuishi milele. Ndio
maana wengi utesa miili yao na kuhisi kwamba mwili ndo usababisha mateso na
shida...kwa sisi leo wakristu mtazamo huyo sio sahii.

Sasa kifo ni
nini? Kwa wale wasio mwamini Yesu kifo kwao ni mwisho wa kila kitu na mwisho wa
maisha ya wanadamu na hayo yatabaki kuwa maswali bila majibu kwa watu ambao
bado wanashindwa kuweka matumaini yao kwa Mungu lakini kwa yule ambaye Kristo
ni Mwanga, Njia na Uhai maswali haya hakika haina nafasi. Kwa sababu kifo kwake
ni hatua ya maisha mpya katika neema na baraka yake Mungu ambao Kristo
utuonyesha wazi kupitia ufufuo wake.
Kwa mtazamo
huyo kila mara tunapo kutana na kifo ni lazima tujiulize kwamba maisha yetu ya
kimwili yaendana sare na maisha yetu ya kiroho. Kusudi hatatutakapokufa
matumaini yetu kwa Yesu yasififie. Basi wapendwa tukielewa kwamba kifo sio
jeneza ao gereza ya mioyo zetu ao sio mwisho wa maisha ya wanadamu tutatafakari
vizuri masomo yetu ya leo. katika somo la kwanza Nabii Ezekieli anawatangazia
Waisraeli mwisho wa utumwa na kurudi kwao katika nchi ya ahadi toka utumwani.
Nabii Ezekieli anaeleza juu ya kupandishwa kwa taifa la Israeli akitumia mfano
wa kuyafunua makaburi na kuwapandisha watu wake. Ahadi ya uzima inawekwa tena
kwa watu ambao kama mifupa mikavu hawana matumaini ya kuishi. Kuokolewa huko toka utumwani ni mfano
wa Kipasaka wa tumaini la ufufuko. Hata maneno ya nabii yana muono wa
Kipasaka kwetu sisi: “Nitafunua makaburi
yenu…..nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi.” Mungu anaonesha
kuwa makaburi si mahali pa mwisho pa kupotea au shimo la kutupa maiti kama
takataka...bali ni mahali pa mpito na mwanzo wa maisha mapya ya kipasaka.
Ukombozi huo wa kuwatoa katika makaburi ni mfano wa ufufuko wa miili yetu siku
ya mwisho. Kumbe, kwa kifo tunapata
tumaini la ufufuko
Ndio maana
Zaburi(130) yetu leo utuonesha wazi kwamba mbele ya Bwana kuna huruma, kuna
fadhili, na kwake kuna ukombozi. Hapo mkosefu ni taifa nzima la Israeli ambalo utambua upendo usio na mipaka wa
Mungu, Neema na Huruma ya Mungu na kuamini kwamba kuhurumiwa na Mungu ni Mwanzo
wa maisha mpya, wa agano mpya wa matumaini mpya uliozidi ukosefu wao. Wapendwa
hata sisi leo tutambue kwamba sisi ni wakosefu na dunia yetu imechafuka na
maovu makubwa kabisa ambao utuweka sisi makaburini na kufutilia mbali
matumaini yetu kwa Mungu... lakini tutambue kwamba Mungu ni Mwaminifu na Baba
yetu anayekuja na kufungua mikono yake kabla hata sisi atujafungua vinywa vitu(
Luka 15) na kutuonyesha huruma na ukombozi wake uliopita ukosefu wetu basi
katika shida inaotusumbua leo yaani Coronavirus, tusikate tama tuweka matumaini
yetu kwake Yeye ambaye ni kila kitu kwetu na kupiga magoti na kusema: Bwana,
kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha
ili Wewe uogopwe.

Pili Yesu
utualika kuwa watu wa imani kwake: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa
anaishi, naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je,
Unayasadiki hayo? Yesu anataka kutufundisha kuwa kifo si kitu cha
kutisha kwa yeyote mwenye imani bali ni hatua ya kuingia kwenye upya wa uzima
wa milele. Pia tusadiki kuwa utukufu wa Mungu utadhihirika kwa njia yake, yaani
kwa kifo na ufufuko wake. Kwa hiyo inaoitajika ni kumtambuwa Yesu kuwa ni
Masiya na Mwana wa Mungu pia na kukiri imani yetu mbele yake kama vile Petro
na Martha nakusema: Naam, Bwana nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe
Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.
Basi tukiwa na
imani kwa Yesu ni lazima tuishi imani yetu kwa vitendo. Ndio maana katika somo
la pili Mtume Paulo anasema: lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa
Kristo, huyo si wake...ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa
ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo
katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Mtume paulo
anataka kutuambia kuwa kuishi katika Roho ya Kristo ni kuisha katika roho ya
upendo, Roho ambalo utajwa hapa ni Upendo ambao Yesu mwenyewe uonyesha kwa kufa
msalabani kwaajili ya dhambi zetu na ndo Roho yule yule ambaye mimi na wewe leo
tunaitwa kuufata kwa kujitolea bila kijibakiza kwa wenzetu wanao itaji msaada
wetu hususani wakati huu wa Kwaresima.
Wapendwa
namaliza tafakari hii na kusema kwamba kifo ni haki yetu mbele ya Mungu. Kwa
sababu Mungu ametuumba kwa upendo wake na kwa lengo maalumu. Kwa hiyo, mtu
anapokufa anakuwa amemaliza muda wa kuwa hai aliopewa na Mungu. Hivyo basi,
mbele ya Mungu aliye Bwana wa uhai na nyakati zote ni safi na ni vema. Lakini
kwa sababu ya hali yetu ya kibinadamu tunapata taabu, huzuni kwa vile hatuwezi
kuelewa fumbo la Mungu. Basi katika hali hiyo ya kibinadamu, tusihangaike,
tujue kuwa Mungu ata katika hali hiyo, shida ao magumu yu pamoja nasi. Pia
tutambue kuishi miaka mingi au michache hakutimii kwa hesabu zetu za kibinadamu
bali ni zawadi. Tujiandae vyema kupokea kifo, kwani kwa kifo tunapata tumaini
la ufufuko.
Shemasi Bienvenu Kabeya Ngungwa Kungwa Poulain Loquace,
SDS
Commentaires