MAHUBIRI YA DOMINIKA YA TATU YA KWARESIMA MWAKA A WA
KANISA: KWELI UNA KIU CHA MUNGU?
MASOMO
SOMO LA KWANZA. Kutoka 17: 3-7
SOMO LA PILI Warumi 5: 1-2, 5-8
SOMO LA INJILI Johane 4: 5-42
WAZO KUU: TUWE WATU WENYE KIU CHA MUNGU NA MATUMAINI
KWAKE
UTANGULIZI:
BIBLIA NA LITURUJIA
Wapendwa Mama Kanisa: Katoliki Takatifu uwa na
himiza katika mafundisho yake kuwa: jambo muhimu kuliko yote katika adhimisho la
Liturujia ni Maandiko Matakatifu, maana katika hayo huchukuliwa masomo ya
kusomwa na kufafanuliwa katika mahubiri, na pia zaburi zinazoimbwa. Sala,
maombi na nyimbo hupata uvuvio toka Maandiko, kama vile toka Maandika matendo
na ishara hupata maana. Kwa hiyo, ili kufaulu kufanya marekebisho na maendeleo
na malinganisho ya Liturujia, ni lazima kuhimiza ule upendo mtamu na hai wa
Maandiko Matakatifu, ambao unashuhudiwa na mapokeo mastahiki ya Makanisa ya
Mashariki na Maghari.( haya tunayapata katika Hati za Mtaguso Mkuu wa Vatican II katika Constititusio juu ya Liturujia ufahamika kama Sacrosanctum Concilium article 24)
Basi tukiwe na lengo hilo
ndani mwetu basi tuangane na Maandiko Matakatifu ya leo inao tutaka leo mimi na
wewe kuwa na kiu cha Mungu na matunaini kwake.
SALA: Tumuombe Mungu kusudi tushindwe mateso, magumu, magonjwa... kila mtu kadiri ya wito wake aweze kushinda kiu
chake kama fedha, anasa, madaraka, wizi, ushirikina, mali inao tupeleka
kuwahudumaza wenzetu na kumwacha Yeye Aliye Maji ya Uzima. Pia tuombe neema na
utakaso wa Mungu katika wakati huu Dunia iko katika shida na hofu ya ugonjwa wa
cororavirus.
UFAFANUZI
WA MASOMO YETU
Wapendwa leo tunahadhimisha Dominika ya tatu ya
kwaresima katika mwaka A wa Kanisa. Katika Dominika hii tunaalikwa na Yesu
kumfuata Yeye Mungu na Mwokozi wetu kusudi tupate Maji ya Uzima wa milele hili
tumalize kiu chetu. Basi nawalikeni sote kutafakari Mafumbo Matakatifu huku
tukijiweka tayari kuongea na kumsikiliza Yesu kama yule Mwanamke Msamaria
katika injili yetu ya leo.
Wapendwa, katika somo la
kwanza tunasikia mwendelezo wa manunguniko na upungufu wa imani wa wana
waisraeli. Kitabu cha Kutoka kinatupa picha halisi ya maisha ya wana wa Israeli
katika safari yao ya ukombozi katika jangwa. Wapendwa katika sura ya 16 ya
Kitabu cha Kutoka, katika Jangwa wana wa Mungu walipatwa na njaa na mkutano mzima
wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani... wakawaambia:
laiti tungalikufa kwa mkono wa bwana katika nchi ya Msri, hapo tulipoketi
karibu na zile sufuria za nyama, tulipolula vyakula hata kushiba; kwani
mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili
lote. Ndipo Bwana akamwambia Musa: tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya
mkate kutoka mbinguni... Mungu ni Baba yetu na katika agano lake yeye
ubaki kila siku Mwaminifu na Mwenye Haki. Yeye alisikia kilio cha watoto wake
naye akawajibu na kuwapa Mana.
Cha kushangaza
wana wa Israeli wanashindwa kumtegemea na kumtumainia Mungu kila mara walipata
mateso na magumu katika safari ya ukombozi wao. Ndo sababu leo katika somo letu
la Kwanza, kutoka katika katika kitabu cha Kutoka sura ya 17. Wana wa Mungu
wakawa na kiu huko; nao wakamnungu;unikia tena Musa kama vile walivyofanya katika sura ya
16... Musa akamlilia Bwana, akisema, niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo
nao watanipigia kwa mawe... Bila shaka Mungu anawatendea tena muujiza
nao wakapata maji. Wapendwa baada ya muujiza kutoka kwa Mungu, Musa alipahita
mahali jina lake Masa kwa sababu ya mateto ya wana wa Israeli na Meriba kwa
sababu walimjaribu Bwana, wakisema, Je Bwana yu kati yetu au sivyo?
Wapendwa maji bila shaka
ni alama ya uzima, maji ni alama ya utakaso katika miili yetu na katika roho
zetu, maji inatumika katika sakramenti ya ubatizo. Ndio sababu Mama Kanisa
linatufundisha kama ifatavyo kuusu maana ya maji Mosi: katika liturujia ya Usiku wa paska, wakati wa kubariki maji ya Ubatizo,
kanisa linafanya rasmi kumbukumbu ya matukio makuu ya historia ya wokovu ambayo
yalikuwa kifano cha fumbo ya Ubatizo: kwa hiyo Mungu anatenda kwa
nguvu isiyoonekana mambo ya ajabu kwa njia ya sakramenti. Umekifanya kiumbe
maji kwa namna mbalimbali kiwe ishara ya neema ya Ubatizo.(cf.
Katekisimu ya kanisa katoliki art. 1217 pia kitabu cha mwanzo 1:2) Pili: Maji ya chemchemi yanapokuwa
alama ya uzima, maji ya bahari yanakuwa alama ya mauti. Ni kwasababu hiyo maji
haya yanaweza kuwa kifano cha fumbo la msalaba. Kwa njia ya mfano huu Ubatizo
juashiria ushirika katika mauti ya Kristu.(Cf. Katekisimu ya Kanisa
Katoliki art. 1220)
Wapendwa tujiulize sasa kwetu sisi somo hili linatufundisha
nini? Kwanza kabisa tutambue kwamba kutokuwa na imani kwa wana wa Israeli kila
mara wanapopatwa na shida, magumu ao mateso, uonyesha picha halisi ya kila
mwanadamu anaye tujiuliza kama kweli Mungu yu katika maisha yake hususani
pale anapopata shida, magonjwa, mateso,, njaa na kazalika. Lakini tutambue
kwamba, jangwa si sehemu ya mateso ya kudumu ila kwa anaye mwamini Mungu, katika
jangwa tunasafiri na katika safari kuna vishawishi, changamoto, shida... lakini
kwa mkristu nilazima kumtumainia Mungu kama Msimamizi wa safari yetu. Kwa hiyo
jangwa inakuwa kwetu sehemu ya kusali, ya kujithamini, kujitakasa na ya
kuvumilia mateso...basi kupata maji katika jangwa maana yake ni kuwa na
matumaini ya kwamba Mungu yuko nasi hata katika shida, Mungu yuko nawe hata
katika magonjwa, hata katika coronavirus, inayoitajika ni kuwa na imani, kuwa
na matumaini na kutemgemea Yeye kila siku ya Maisha yetu. Basi tusimjaribu na
kumwacha Mungu wakati wa shida ao mateso huku tukitanga tanga ya kutafutu
miungu wasiojulikana. Tukimwamini Mungu tutapata maji ya uzima wa milele.
Wapendwa katika injili
tunasikia simulizi ya Yesu na yule mwanamke Msamaria kuusu Maji. Yesu katika
safari yake ya kuelekea Yerusalemu akafika kunako mji wa Samaria, Yeye kama
myaudi anamwomba Msamaria akisema: Unipe maji ninye. Bila shaka yule
Mwanamke anamjibu na kumwambia kuwa: wayahudi hawachangamani na wasamaria...
Yesu akajibu, akamwambia: kama ungalijua karama ya Mungu, naye ni nani
akuambiaye, nipe maji ninye, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
Maneno ya Yesu yanamufanya mwanamke kuvutiwa na mazungumzo na Yesu na kusema: Bwana,
huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji
yaliyo hai...? Yesu akajibu: kila anywaye maji haya ataona kiu tena;
walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele;
bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika
uzima wa milele. Na yule mwanamke akwamwambia: Bwana, unipe maji hayo, nisione
kiu, wala nisije hapa kuteka.
Wapendwa simulizi hii inaonyesha wazi nia ya Mungu
ya kumuokowa kila mtu hata yule alietengwa na wanadamu wenziye, alietengwa na
jamii ao ndugu, rafiki huku akionekana kuwa mkosefu zaidi mbele yao. Yesu alikuja
kutafuta wakosefu na kuwapa uzima wa milele watu wote. Na injili ya Mathayo 18:
12-14 inasema hivi: Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmja akampotea, je hawawaachi wale
tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliye potea? Hata akipata
kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini
wasiopotea. Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba
mmja wa wadogo hawa apotee.
KATIKA MAISHA YETU
Wapendwa, katika simulizi
ya leo tutafakari mambo muhimu ifatavyo: Mosi:
ni vema kutambua kwamba Mungu anatupenda sisi sote na yuko na mpango na
kila mmja wetu. Kwa hiyo katika safari ya wokovu wetu ni Yeye kwanza anayechukua
hatua ya kwanza na kuja kwetu kutafuta urafiki nasi basi mimi na wewe tunaombwa
kumsikiliza na kuonyesha ushirikiano katika wito wake kwetu. Yesu ni Yeye
kwanza alitafuta urafiki na yule mwanamke kusudi amwokowe katika hali yake ya
upotovu na yule mwanamke alionesha usikivu na ushirikiano hadi akapatwa na kiu
cha Mungu: Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.
Pili katika wito wetu Mungu anayajua mapungufu yetu yote
vizuri. Sisi nilazima kuwa wazi mbele yake na kufanya jitihada ya kuyaacha.
Yesu alienda kisimani saa sita kusudi akutane na yule mwanamke: watalamu wa
Biblia uwa na tafsiri kwamba sio kawaida kwenda kisimani saa situ kwa kina
mama. Wanawake wengi uwa naenda kuteka maji asubuhi ao jioni huku mara nyinyi
wakiongozana kama kundi ya watu wawili ao watatu ao zaidi... lakini yule
mwanamke msamaria inaonekana alikua akitengwa na jamii labda kwaajili ya
matendo yake uliokuwa ayendani na mila au desturi ya jamii yake huku akisubiri
na kulenga kuwa kisimani hakuna mtu ili awe katika amani na salama... na haya
hudhibitiswa wakati Yesu anamwambia: Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. Yule
mwanamke akajibu, sina mume. Yesu akamwambia, umesema vema, sina mume; kwa
maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo
umesema kweli. Maana yake hatuna budi kujificha mbele ya Mungu ila tujifunze
kumwambia Mungu ukweli na uzito wa udhaifu wetu nasi tutapata faraja kama huyu
mwanamke...tunaweza kuwakimbia binadamu wenzetu lakini hatuwezi kumkimbia wala
kujificha mbele ya Mungu. Tuwe watu wenye kujitambuwa hasa kutambuwa makosa na
dhambi zetu.
Tatu: nilazima kumtambua Yesu kupitia mazungumzo naye. Tumumpe
Yesu nafasi ndani ya maisha yetu kusudi tupate kumtambuwa yeye kama Masiya.
Kwetu ni kama kupitia sakramenti, sala, mioyo zetu, wenzetu,maskinin, wanyonge,
mangonjwa, shida, Kanisa... hizi ni nafasi ambao tunakutana na Yesu. Yule mwanamke
alimpa Yesu nafasi na kumsikiliza hapo alifunuliwa naye hadi kumkiri na kusema:
Bwana,
naona ya kuwa u Nabii... Naye Yesu akamwambia: Mama, unisadiki, saa inakuja
ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu... Lakini saa
inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na
kweli. Yule mwanamke akamwambia: Najua ya kuwa yuaje Masiha, aitwaye Kristo;
naye atakapokuja, yeye atatufunulia mabo yote. Yesu akamwambia: Mimi
ninayesema nawe, Ndiye.
Inne: Tunapo mtambuwa Yesu
kama Masiya ni lazima tuondoke, twende kuwapasha, kuwahubiri, na kuwavuta
wenzetu pia waje kumtambua. Hii ni jikumu la kila mmja mwetu baada ya Ubatizo kadiri ya wito wake
ndani ya kanisa kumtangaza Kristo popote ulimwangani kwa ushuhuda wa maisha na
imani yetu kama wakristu, kwa kuwaudumia watu bila kochoka... hayo tunayapata
katika injili. Yule mwanamke baada ya kutambua Yesu kuwa ni Masiya akauacha
mtungi wake yaani akaacha matendo yake yote ya zamani, akaenda zake mjini na
kuwa missionari na muhubiri wa habari njema kwa watu: Njoni, mtazame mtu aliyeniambia
mambo yote niliyoyatenda. Je haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? Basi wakatoka
mjini wakamwendea.
Nataka nikwambiye leo: usikate tama,usichoke
kumtafuta Yesu Kristo katika maisha yako hususani katika shida, mateso,
magonjwa... usichoke kuungama mbele yake kama mzambi na mkosefu, tambuwa
mapungufu yako na utubu naye Yesu atakufunya kuwa chombo cha habari na baraka yake kwa watu
wanao kuhukumu wewe kama mkosefu. Ndio maana Mtume Paulo katika somo la pili
kutoka katika waraka kwa warumi hutusihi na kutuonya kwamba: Na tuwe na imani
kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Ambaye kwa yeye tumepata kwa
njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na kufurahi
katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Tumsifu
Yesu Kristo
Shemasi
Bienvenu Kabeya Kungwa Ngungwa Poulain Loquace
Commentaires