MAHUBIRI YA SHEREHE YA KUPASHWA HABARI YA KUZALIWA BWANA: 25 MARCH 2020
MASOMO
Somo I: Isa. 7:10-14
Somo II: Ebr. 10:4-10
Injili: Luka 1:26-38
SALA: Kwa maombezi ya Mama Bikira Maria, tumuombe na
kumshukuru Mungu kusudi atuepushe na maradhi ya ugonjwa wa coronavirus na awape
uzima na pumziko la milele wote walio tutangulia mbele ya haki kupitia ugonjwa
huo.
UTANGULIZI
Wapendwa leo
Mama Kanisa anahadhimisha sherehe ya Kupashwa Habari ya Kuzaliwa Bwana.
Sherehe ya leo ilianze kwaadhimishwa na Kanisa tangu karne ya 6-7 huku wa
kihesabu miezi 9 kabla ya kuzaliwa Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yaani ukihesabu tarehe
25 ya Mwezi wa Tatu hadi tarehe 25 ya Mwezi wa Kumi na Mbili utapata mwezi Tisa. Wapendwa kupashwa habari ya
kuzaliwa Bwana ni mwanzo wa muhula mpya na ukombozi wa Mungu kwetu sisi ambao
Mungu anaonyesha upendo wake mkuu kwa ulimwengu mzima.
UFAFANUZI
Tukisoma
katika Biblia, tutaona kuwa katika historia ya wanadamu na Mungu kuna baadhi ya
watu walipashwa vile vile habari ya kuzaliwa kwa watoto wao katika hali ya
ajabu mno. Katika kitabu cha Mwanzo 18: 9-14 Ibrahamu kupitia mkeo Sara
anapashwa habari ya kupewa mtoto wa kiume: wakamwambia yuko wapi mkeo Sara? Akasema,
yumo hemani. Akamwambia, hakika nitakurudia wakati uu huu mwakani, na tazama,
Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Basi Ibrahaimu na Sara walikuwa wazee, na
umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake... tena
katika kitabu cha Waamuzi 13:2-7, 24-45 Manoa na mkeo alikuwa tasa, hakuzaa
watoto anapashwa pia habari za kupata mtoto: Malaika wa Bwana akamtokea yule
mwanamke, akamwambia: Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba,
nawe utamzaa mtoto mwanamume... na wembe usipite juu ya kichwa chake, maaana
mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa
Israeli na mikono ya wafilisti... Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita
jina lake Samsoni... Katika Agano Jipya: tukisoma Injili ya Luka 1:5-25,
57-80 tutasikia kutabiri kuzaliwa kwake Yohane Mbatizaji: ... Akatokewa
na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Lakini yule Malaika akamwambia,
usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto
mwanamume, na jina lake utamwita Yohane...(Rejea Luka 1: 11-13)
Wapendwa kupashwa habri na Malaika kuhusu kuzaliwa kwa watoto katika Biblia
kulionesha uku na uwezo wa Mungu dhidi ya elimu na akili ya wanadamu. Lakini
katika tukio ya leo nilazima tulitafakari katika mtazamo wa pekee.
Wapendwa tutambue
kwamba tukio ya Kupashwa Habari Kuzaliwa Bwana ni tofauti kabisa na zile
matukio mbali mbali katika Biblia ambamo Mungu anajibu na kutenda maajabu
kutokana na sala na dua ya watoto wake. Lakini katika sherehe ya leo Mungu kwa
hiari yake Mwenyewe anakuja tena kuumba dunia na kutakasa ulimwengu nzima baada
ya upotevu ya wazazi wetu wa kwanza. Pili Mungu anamushirisha mwanadamu katika
ukombozi wa mafumbo haya matakatifu. Ndio maana Kanisa letu Katolika
linatufundisha hivi:
Maandiko Matakatifu ya
Agano la Kale na Agano Jipya na Mapokeo ya kale yaonesha wazi zaidi na zaidi
dhima ya Mama wa Mwokozi katika mpango wa wokovu, na kuiweka mbele yetu
tuifikirie... Mungu wa huruma alitaka Umwilisho(Incarnation) utanguliwe na ukubali
wake yeye aliyeteuliwa tangu milele awe Mama, ili kama vile mwanamke
alivyoshiriki kuileta mauti, kadhalika mwanamke asaidie kuuleta uzima.(Cfr. Konstitusio ya
kidogma juu ya Fumbo la Kanisa, art. 55-56)
Kwa hiyo,
katika sherehe ya leo lazima tukumbushane mambo muhimu ifatavyo: Mosi Maria alitakaswa na Mungu na
kuwekwa kuwa Mtakatifu na kupewa neema tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu kusudi
ya Mungu Yesu akaye kuja kuketi ndani yake. Kwa hiyo hatuwezi kumuongelea Maria
bila kumuunganisha na Mwanae Mtakatifu sana Mungu pamoja nasi Emmanueli. Kwa kweli
kila mvuto wa wokovu kwa upande wa Bikira Maria kwa watu hautoki katika lazima
fulani bali katika mapenzi ya Mungu, na kububujika kutoka wingi wa mastahili ya
Kristo. Pili kwa ukubali na utayari
wake katika kuifanya mapenzi ya Mungu: Bikira Maria anakweza na Mungu na kuitwa
Mwenye heri Mama wa Mungu: wapendwa umama huu wa Maria katika mpango wa neema
unadumu bila kukatizwa tangu nukta ile ya ukubali aliotoa kwa imani wakati wa
tangazo la kuzaliwa Bwana na alioushikilia bila kusita chini ya msalaba, hadi
ukamilifu wa milele wa wateule wote. Tatu
Maria alitukuzwa kwa neema ya Mungu, baada ya Mwanawe, kupita malaika wote na
wanadamu wote, kwa maana yeye ni mama mtakatifu sana wa Mungu aliyeshiriki
mafumbo ya Kristo basi kwa sababu ya hiyo Bikira Maria anaheshimiwa kwa haki na
Kanisa kwa ibada ya pekee, nao waumini wote wanaukimbilia ulinzi wake,
wakimwomba katika hatari zote na mahitaji yao.
Basi ndugu zanguni, leo ni siku
ya furaha kwetu, siku ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya upendo wake mkuu kwetu ili
tupate wokovu. Pia tunafurahi kwa sababu ya Bibi Yetu Bikira Maria anaye
tufundisha kujitoa na kuwa waaminifu na tayari katika kazi ya kumtumikia Mungu:
Maria kwa ndio yake neema katika maisha yetu huitimishwa katika tukio nzima ya
ukombozi wetu basi mimi na wewe leo kupitia Ubatizo wetu tunaalikwa na Mungu
kuwa tayari kusema ndio kwa kufanya mapenzi yake. Basi wapendwa Mama Bikira Maria
ni mfano wetu bora wa kuwa mfuasi kweli wa Kristo kwa kujikabidhi na kujitolea
bila kujibakiza hadi kushudia mateso, kifo na ufufuko wa Mwanae Mpendwa kwa
hiyo tunahitaji waombezi yake kwa Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo asa zaidi
katika kipindi hiki ya maradhi ya Coronavirus ili tupate utakaso wa miili na
mioyo yetu pia tuwe tayari kumtumikia Mungu kupitia wagonjwa, maskini, wafungwa
na wahitaji wote.
Tusema wote pamoja katika imani: kwa
hiyo ajapo ulimwenguni, asema, dhabihu na toleo hukutaka, lakini mwili
uliniwekea tayari. Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo,
ndipo niliposema, Tazama nimekuja katika gombo la chuo nimeandikiwa niyafanye
mapenzi yako, Mungu.(Ebr.10: 5-7)
Shemasi Bienvenu Kabeya Kungwa Ngungwa Poulain Loquace,
SDS
Commentaires