MAHUBIRI YA SHEREHE YA MTAKATIFU YOSEFU, MUME WAKE
BIKIRA MARIA
MASOMO
Somo I: 2Sam 7:12-14
Somo II: Warumi 4:16-18,
22
Somo III: Mt. 1:16,
18-21, 24
UFAFANUZI WA MASOMO
Wapendwa leo
tunaadhimisha sherehe ya Mt. Yusefu, mume wake Bikira Maria. Tukisoma Luka 1:
30-31 tutasikia utabiri wa kuzaliwa kwake Yesu: Malaika akamwambia, Usiogope,
Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba na kuzaa
mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Wapendwa Mpango wa Mungu
wa kilikombowa ulimwangu aukumustuwa tu Bikira Maria lakini ulimustuwa pia
mchumba wake Yusufu. Lakini kama Bikira Maria, Yusufu alipata pia neema kwa
Mungu huku akifunuliwa jina na kazi ya Masiha: basi alipokuwa akifikiri hayo,
tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa
Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho
Mtakatifu. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye
atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Wapendwa Yusefu
ni nani? Mosi tutambuwe kwamba Yusufu
anatajwa tu mara 14 katika injili. Ametajwa kuwa mume wa Bikira Maria na baba
halali mlinzi na mlishi wa Yesu(Yohane 6: 42: wakasema, huyu siye Yesu, mwana
wa Yusefu, ambaye twamjua babaye na mamaye?, Luka2:48: Na
walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetenda
hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni)
Yusufu ni mtakatifu anayefamika kuwa na ustaarabu na utilivu wa pekee.
Tunamfahamu kwa ukimya wake, upole na utayari wa kufikiri kabla ya kutenda: kwa
tabia hizo zilimfanya achaguliwe na Mungu kuwa baba mlinzi na mlishi wa Yesu na
mchungaji wa Familia nzima Takatifu. Tena tutambuwe kwamba Kanisa letu Katoliki
linawapa na fasi ya pekee Maria na Mt. Yusufu hadi kuwakumbuka na kuwataje
katika adhimisho ya Misa kuwa Yusufu ni Mtakatifu aliyeishi nadhiri ya usafi wa
Moyo na Maria ni Bikira milele basi kwa mafundisho haya Yusufu na Maria awakuwa
na watoto wengine ila Yesu tu.(kwa sababu kuna baathi ya watu utabiri vibaya
injili ya Marko 6:3: Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na
ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni?)
Pili tutambuwe
kuwa injili ya Mathayo na Luka inatufundisha wazi kwamba ni kupitia Mt. Yusufu,
Yesu aliingizwa rasmi katika ukoo wa Daudi.( Luka 3:23-28, Mt.1:1-17), uwepo wa
Yesu katika ukoo wa Daudi ni hitimisho wa mpango wa ukombozi wa Mungu kuanzia
Abrahamu-Musa-Manabii.(hata Yohane hudhibitisha katika injili yake sura 1:45: Filipo
akamwona Nathanaeli, akamwambia, tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika
torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti)
Ndiyo sababu
somo letu la kwanza linatoka katika kitabu cha 2 cha Samweli ambapo Mungu
kupitia nabi Nathani anaahidi kuusimika ufalme wa Daudi milele kwa kupitia
mwanae Solomoni alierithi kiti chake na aliyefanikiwa kulijenga Hekalu la Bwana.
Kwa hiyo ufalme wa Daudi uliimarishwa milele kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo
aliyekuwa mzao wa Daudi na aliyenjenga Hekalu la Mungu na kusimika ufalme wa
Mungu Milele kwa mateso, kifo na ufufuo wake. Ndiyo maana injili ya leo
utuonyesha wazi namna gani Mt. Yusufu alivyo toa mchango mkubwa sana kwa
kukubali kumpokea Mariamu Mkewe aliyepata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu ili
ufalme wa Mungu wa kilikombowa ulimwengu nzima ukamilike. Ndio maana Mt. Paulo
katika somo la pili anadhibitisha kuwa: kwa maana ahadi ya kwamba atakuwa mrithi wa
ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa haki
aliyohesabiwa kwa imani. Basi wapendwa bila imani hatuwezi kuonja
utukufu wa Mungu kwetu. Na Yusufu alionja utukufu wa Mungu kwa sababu aliweka
matumaini na imani yake kwa Mungu hadi kupokea ujumbe wa malaika na kuhufanyia
kazi.
Wapendwa, hapo
lazima tujifunze mengi kutoka kwa Mt. Yusufu. Ki ukweli tuko wengi kati yetu
tunapoteza baraka ya Mungu kwa sababu ya kutokuwa na utulivu, imani imara na dhabiti,
siri na ukimya wa moyo. Hakika Yusufu angelikuwa papara angepoteza bahati ya
kuwa mlinzi na baba mlishi wa Yesu. Lakini sisi kwa sababu ya kwenda haraka
katika mahamuzi yetu, tumeishia kufanya matendo kama wapagani na wasiokuwa na
imani yenye msingi. Wewe kama mtawa, mkristu, shemasi ao padri, nilazima
tumbuwe kwamba bila utilivu na ukimya wa moyo hatuwezi kufanikisha kazi yetu ya
kitume. Pale tunapopata shida, tatizo kama Corona Virus leo yafaa tutulie
kwanza kabla ya kutenda na kupiga kelele. Nilazima kusikia kwanza ushauri
utokalo ndani ya mioyo yetu baada ya kutafari kabla yakutafuta ushauri kutoka
kwa wenzetu kwa sababu mshauri wa kwanza ni Roho Makatifu katika mioyo yetu.
Pia Kwa ndungu zetu wanyonge, wangonjwa wa tabia, wa miili, kwa ndungu zetu
watawa na wengine wote tunao waita mizigo kwetu tusiwaepuke lakini tuwe kama Yusufu kwao kwa
kuwalinda na kuwasaidia katika shida na matatizo zao. Baba zetu wafamilia nilazima kulinda familia zetu katika upendo na utulivu wa kweli kama Mt. Yusufu. Na jami nzima ni vizuri kutafuta kuzuia unyanyasaji wa watoto na pia utowaji wa mimba. Mungu kupitia malaika wake na kwa utayari wa Mt. Yusufu, Yeye aliye Uzima aliukinga maisha na Uzima wa Mwanae Mpendwa Mungu na Mwokozi wetu. Basi mimi na wewe leo tunaalikwa kuthamini na kuzuia uwaji wowote kuusu maisha ya watoto. Tuwapenda watoto wetu, kwa kuwapa elimu ya kiriho na kimwili kusudi wafanyikiwe kesho na wawe matumisha bora wa taifa na Kanisa letu nzima.
Shemasi Bienvenu Kabeya Ngungwa
Kungwa Poulain Loquace, SDS
Commentaires