MAHUBIRI
YA DOMINIKA YA NNE YA KWARESIMA YAANI DOMINIKA TA FURAHA/LAETARARAE: MWAKA A WA KANISA
SOMO
I: 1 Sam 16: 1b 6-7, 10 -13a
SOMO II: Ef 5: 8-14
INJILI: Yn 9:1-41
SALA: Tumuombe Mungu atuepushe kwa Marathi ya Corronavirus pia awanusuru wote waliopata Marathi hiyo kusudi wapate kupona kama huyu mtu kipofu na mwishoni awapokea na kuwapa raha ya milele wote walio tutangulia katika dunia hii kwa ugonjwa wa Corona.
UTANGULIZI
Wapendwa
leo ni Dominika ya nne ya kwaresima
mwaka A. Kiliturjia, Dominika ya leo uitwa Dominika ya Furahi “Laetarae”. Dominika
ya furaha kwa sababu tangu tulipoanza kipindi cha Kwaresima leo tumemalisa nusu
ya safari yetu. Basi tukiwa na furaha hiyo tuungane na masomo yetu ya leo inao
tualika kutafari kuusu upofu wetu katika maisha yetu.
UFAFANUZI
Wapendwa nilazima tukumbushane
kwamba Jumapili ya tatu, ya Inne na ya Tano ya Kwaresima: ziliwekwa rasmi na
Mama Kanisa tangu zamani kwa ajili ya kuwaandaa Wakatekumeni ambao walitazamiwa
kubatizwa wakati wa sherehe za Mkesha wa Pasaka. Baada ya kuwapa katekesi ya
kutosha kadiri ya miaka mitatu. Dominika ya kwanza ao ya tatu ya kwaresima
wakatekumenu wanapokelewa na kuteuliwa na Mama Kanisa na leo jumapili ya nne
pamoja na
sala, Kanisa anawafanyia matendo mbalimbali ya kiliturujia ambayo ni ishara ya
madhehebu ya kuwatakasa yaani exorcism kuwafumbua macho, masikio na midomo yao
na ni neema na kazi ya Mungu inayotendeka ndani mwao. Ndio maana katika injili
tumesikia kuusu uponyaji wa mtu aliezaliwa kipofu. Basi tuwakumbuke
wakatekumeni wetu wote katika Misa hii Takatifu.
Wapendwa katika somo la kwanza kutoka kitabu cha 1
cha Samweli sura 16 tunasikia namna gani Bwana Mungu anamwamuru Samweli kwa
njia yake aende kumpaga mafuta mfalme aliopendezwa naye katika wana wa yese.
Tunaweza kujiuliza kwa nini Bwana anamtaka mfalme mpya wakati wana wa Mungu
walikuwa tayari na mfalme wao? Basi ni vizuri kusoma kitabu cha 1 cha samweli sura
ya 8 na 15 hapo tutapata jibu. Tukisoma Katika kitabu cha 1 cha Samweli sura ya
8 tutasikia namna gani wana wa Israeli wakidai kuwa na Mfalme wakamwambia: angalia wewe unakuwa mzee, na
wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa
mataifa yote... lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema
tupe mfalme atuamue... Samweli anajua kwamba mfalme wa Israeli ni Mungu
Mwenyewe lakini wao wanatamani maisha ya mataifa nyingine. Naye Samweli
akamwomba Bwana. Bwana akamwambia Samweli, izikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakolokuambia; kwa
maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.
(1Sam 8:1-22) lakini kabla ya kupewa mfalme mpya Mungu kupitia Samweli aliwapa
tahadhari ya taabu za utawala wa kifalme kutoka kwa binadamu.
Basi walipewa mfalme Sauli kuwa mfalme wa kwanza
wa Israeli na hapo uonyesha mwanzo wa mateso ya wana wa Israeli kutawailawa na
kuteswa tena na mataifa nyingene. Ukweli ni kwamba katika maisha yetu, familia
yetu, jumuiya yetu ya kitawa bila Mungu, bila mwongozo wa Yesu ni shida na
migogoro kila siku. Na ukisomo kitabu cha Samweli cha 1 sura ya 15: 10-35
utasikia namna gani Sauli anaachwa na Mungu mara baada Sauli kuvunja amri ya
Mungu na kuungana na mataifa mengine hususani mfalme wa Ameleki na kujipatia
vitu vingi toka kwake. Ndipo Mungu akamtuma Samweli kwenda katika Bethlehemu
kumchagua mfalme mpya ambaye amependezwa
naye mwenyewe katika nyumba ya Yese.
Samweli baada ya kumuona mtoto ya Yese wa kwanza:
kwa uzuri wake, urefu na nguvu, alidhani huyu ndiye ambaye amependezwa na
Mungu: lakini Bwana akamwambia
Samweli, usitazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maan mimi nimemkataa.
Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya
nje, bali Mungu huutazama moyo. Basi Yese akawapitisha wanawe saba
mbele ya Samweli lakini Bwana hakuwachagua hawa. Amesalia mdogo wao, na tazama,
anawachunga kondoo asema Yese. Basi Samweli akamwambia, tuma watu, wamlete...
naye akamleta kwao. Naye alikuwa
mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza Bwana
akasema, ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye. Naye ni falme Daudi.
Wapendwa tutambue kwamba mbele ya Mungu hatuwezi
kujificha na Mungu anatujuwa vizuri. Kwa hiyo usimzarau mtu kwa sababu ya
mwonekano wake, upungufu wa elimu aliopata ao maisha yake kwa sababu haujui
nini Mungu anamwandalia kesho. Kila mja wetu aliumbwa kwa sura na mfano wa
Mungu na kila mja wetu anathamani kubwa mbele ya Mungu kwa hiyo anatakiwa kuheshiwa
kama mwanadamu. Mungu anawakweza wanyonge, wadogo, wale sisi tunaona awafai na
kuwashusha walio na nguvu, walio na akili, walio na majivuno. Kuwa mkubwa mbele
ya Mungu ni kuwa mtumishi wa watu ni hiyo ndio kazi ya mfalme, kazi ya kila mja
wetu kama mbatizwa, kuwa mtumishi wa watu.
Basi wapendwa Yesu kama mfalme wa kweli
amejifanya kuwa mtumishi kwa kuwasaidia na kuwaponya watu kila mja kadiri ya
ungonjwa wake. Leo katika injilii Yesu anamponya mtu ambaye alizaliwa kipofu. Yesu anamwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa kwake. Mitume
wanamwuliza: Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake hata azaliwe kipofu? Mitume waliuliza hivyo kulingana na mafundisho
ya Waalimu wao wa kiyahudi juu ya asili ya ugonjwa. Jibu la Yesu ni tofauti na
mwono wa waalimu wa kiyahudi. Yeye anajibnu: Huyu hakutenda dhambi, wala
wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
Alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate, kishapo akachukua tope na
kumpaka kipofu macho yake na kumwambia: Nenda kanawe katika birika la Siloamu. Kipofu alikwenda, akanawa,
akarudi angali anaona. Kwanza ni vizuri
kutambua kwamba wayahudi waliamini kuwa mate ya mtu huweza kutumika kama dawa.
Na Yesu kama myaudi Katika nyakati mbalimbali ametumia mate kuwaponya vipofu.
Rejea Mk. 8:23. Lakini kwa tukio ya leo tumesikia:
Alinipaka
tope juu ya macho yangu, nami nikanawa na sasa ninaona. Tendo hili
kiteolojia lina maana kwamba binadamu ameumbwa kutoka katika udongo hivyo Yesu
anamwumba tena mwanadamu huyo kutoka katika asili yake, pamoja na mwanga wa
roho. Basi nasi pia kwa njia ya ubatizo tumeumbwa mara ya pili na tumekuwa
viumbe vipya. Baada ya kupakwa tope hilo lenye nguvu ya kuponya, kilichobaki ni
kuondoa lile tope kwa kunawa maji. Hapo tunapata fundisho na sisi: Haitoshi
kusema nimejuta dhambi zangu sihitaji kuungama. La, sivyo. Ni lazima tuende
tukanawe, tukaondoe upofu wetu na madhambi yetu kwenye kiti cha Kitubio, kama
vile yule kipofu alivyopasika kwenda kuondoa tope zile machoni mwake kwa kunawa
maji ya Siloamu. Birika la Siloamu ni Kiti chetu cha Kitubio.
Yule kipofu alirudi kutoka Siloamu anaona, lakini bado alikuwa kipofu.
Alikuwa kipofu kwa vile hakumtambua Yesu. Hapo alihitaji si tu nguvu ya kuona
(eye sight), bali mwanga wa imani. Ndiyo maana Yesu alimwuliza: Wewe, wamwamini
Mwana wa Mungu? Akajibu yule kipofu aliyekuwa anaona: Ni nani Bwana, nipate
kumwamini? Yesu akamjibu: Umemwona, naye anayesema nawe, ndiye. Hapo ndipo yule
kipofu, baada ya kuangaziwa na Yesu mwenyewe akasema: Naamini Bwana. Akamsujudia.
Basi nasi pia tukiwa na imani ya kweli kwa yesu tutapata uponyaji.
Wapendwa tutambue kwamba shida, magonjwa, marathi, udhaifu na changamoto
vinakuwa na nguvu pale ambapo vinatusaidia kumrudia Mungu. Mtu kipofu anaponywa
kimwili na pia kiroho. Ni ishara ya kupewa uhai na uzima. Kipofu amefunguliwa
macho ya kimwili na kiroho hivyo anaanza kumtambua Yesu. Hakuona tu mwanga wa jua
bali mwanga wa ulimwengu ndiye Kristo. Kipofu amekubali kwamba ni kipofu, na
hivyo anafunguliwa macho na Kristo, anapata kuona na kumwona Kristo, yaani
kumpokea Kristo na mafundisho yake. Ndio maana somo la pili linaanza na kusema:
Zamani ninyi mlikuwa katika giza, bali
sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Maana yake kabla ya ubatizo kila mmoja
wetu alikuwa gizani. Kwa ubatizo
tumewekwa katika mwanga kwa kumfahamu Bwana na kuishi kama watoto wa mwanga.
Kristo ndiye anayetufungua macho ili tuweze kuishi kama watoto wa mwanga.
Yatupasa kufahamu kwamba kufumbuliwa macho kwetu sisi ni suala endelevu. Sio
tukio la siku moja tu; bali kila siku tunahitaji kuona zaidi na zaidi, hivyo
kukua katika kumwelewa na kumfuata Kristo.
Basi ndungu zangu, labda mimi na wewe ni vipofu kama wafarisao, kwa kupinga
kazi ya Mungu iendelee, kwa kutojitambua kwamba tunawaonea wengine,
kwakutofahamu udhaifu wetu na kwakutotimiza wajibu wetu basi kila mja wetu lazima
ajichunguze na kujitafiti kisha amfuate Yesu ili apate kuona.
Shemasi Bienvenu Kabeya Ngungwa
Kungwa Poulain Loquace, SDS
Commentaires