TAFAKARI YA DOMINIKA YA PILI YA KWARESIMA MWAKA A WAKANISA: HUYU NI MWANANGU, MPENDWA WANGU, MSIKIENI YEYE


TAFAKARI YA DOMINIKA YA PILI YA KWARESIMA MWAKA A
 MARCH 8th 2020
Masomo:
Somo I: Mwa. 12:1-4a
`Somo II: 2Tim. 1:8b-10
Somo III: Injili ya Mt. 17:1-9

UTANGULIZI
Leo tunaadhimisha Dominika ya pili ya Kwaresima, kipindi ambacho kinatuelekeza kwenye safari ya ukombozi wetu kutoka kwa  Bwana wetu Yesu Kristo: Yesu Kristo na Masiya wetu anakamilisha wito wake kwa mateso, kifo na hatimaye ufufuko na  utukufu wake. Wapendwa tukiwa na lengo hili basi tuangane na masomo yetu ya leo inayo tualika kutafakari kuusu wito wetu huku tukitambulishwa na Mungu Masiya wa kweli Yesu Kristo Mwanae Mpendwa. Kwa Hiyo kwa kutekeleza wito wetu ni lazima kwanza kumzikiliza Yesu kama vile Mungu anatuamuru katika injili ya leo na pili kuwa tayari kushiriki mateso pamoja naye huku tukiwa na matumaini ya kupata utukufu na uzima wa milele.

SALA: Tuwaombea na kuwakumbuka wanawake wote ulimwenguni wanao sherekea leo siku ya wanawake duniani kusudi kwa maombezi ya Mama Bikira Maria Mama wa Mungu na Mama yetu, wawe wanawake bora katika jamii katika kutekeleza malezi bora ya ulimwengu mzima.
UFAFANUZI
Wapendwa, wakati nilipoanza masoma yangu ya Teologia, Mmja kati ya walimu wangu kila akitufundisha uwa nahimiza na kukazia mambo muhimu mawili ambacho ufafanua chanzo na chimbuko ya imani yetu leo kama wakristu pia na ya imani ya wana waisraeli. Alisema hivi: Wapendwa tutakumbue kwamba Biblia ni kitabu kitakatifu lakini kimeandikwa na wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo wanadamu hawa waliandika kuendana na maisha yawo ya kawaida huku wakitumia mifano na experience yao ya kawaida. Pili kwa waisraeli, kitabu cha kutoka katika Torati ya Musa kinanafsi ya pekee katika maisha yao ya imani. Ukombozi wao kutoka utumwani misri ni hatua ya kwanza ya maisha yao ya imani na ya kumtambua zaidi Mungu. Lakini kwetu sisi wakristu leo, Ufufuo wa Bwana Yesu Kristu ni msingi wa imani yetu na chanzo cha matumaini yetu katika safari ya kumtafuta Mungu zaidi kila siku ya Maisha yetu. Basi mimi na wewe leo tunatakiwa kwanza kusoma na kuyahelewa mafundisha ya Agano Jipya kabla ya kutafsiri ukurasa wa agano lakale kwa sababu Yesu Kristo ndiye anae hitimisha agano lakale.(Cf. Mwalimu wangu wa Introduction to Theology) 
Kwa nini naanza ya kahuli hiyo kwa sababu masomo ya leo hususani somo la injili tutatambua kwamba tukio la kugeuka sura Bwana wetu Yetu Kristo ni hitimisho ya baadhi ya sehemu ya maisha ya waisraeli na pia baadhi ya vipengele katika kitabu cha Kutoka. Kwa hiyo ninawaalika kuwa makini wote pamoja tutafakari huku tukimualika Roho Mtakatifu kusudi tujaliwe neema ya kuyaelewa mafumbo matakatifu.
Wapendwa katika Kristo, kutoka somo la kwanza tumesikia kuusu wito wa Abrahamu. Aliitwa na Mungu na kuambiwa atoke kwenye nchi  na jamaa zake aende ugenini ili maongozi ya Mungu yatekelezwe,yaani Abrahamu afanyike Taifa kubwa. Katika simulizi hizi tutambue kuwa wito wetu ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa hiyo wito hutudai mambo muhimu ifatavyo mosi wito hutudai imani, Pili uamuzi mzito ambao unaweza hata kuwashangaza wengine. tatu hutudai utii na uvumilivu kwa kutekeleza sauti na nia ya Mungu. Kwa hiyo kuachana na ndugu, jamaa na nchi yake aliyoizoea (Harani) humdai Abrahamu uamuzi mzito. Lakini kwasababu ya utii kwa Mungu, aliyavumilia mateso ya kuachana na jamaa na nchi yake akawa tayari kupambana na magumu ya safari kwenda ambako Mungu umwamuru. Aliyapokea yote kwa imani thabiti akitumainia neema na baraka nyingi toka kwa Mungu: Kwa hiyo kwa wito wa Abrahamu historia nzima ya wanadamu ilifamika kuwa nafasi ambapo ahadi ya ukombozi wa Mungu uanza kujionesha taratibu ukombozi ulianza na wana waisraeli utumwani Misri na pia ulio itimishwa na Kuteswa-Kufa-Ufufuo wa Bwana wetu yesu Kristu alie ukomboa ulimwengu nzima.
Wapendwa dominika ya Kwanza na pili ya kwaresima utualika kutoa mahamuzi yetu katika safari yetu ya imani. Katika dominika ya kwanza Adamu na Eva walichagua kifo ambacho uonyesha kutokua na neema ya Mungu leo katika dominika ya pili, Abrahamu anachagua uzima na tegemezi kutoka kwa Munga ndio sababu alizawaidiwa kuwa mwenye haki na baba wa mataifa-dini. Ndio maana zaburi yetu ya leo inasema ivi: Kwa kuwa neno la Bwana lina adili kwetu, na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu...Nafsi zetu zinamngoja Bwana yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, kama vile tulivyokungoja wewe. Basi leo Mungu anatualika mimi na wewe kuchagua na kutoa mahamuzi yetu katika safari ya kumrudia Yeye. Basi kwa Upendo wake kwetu Mungu katika injili anatupa chaguo lenye baraka na neema tele: ndio maana anamtubulisha Mpendwa Mungu na Masiya wetu na kutuomba tumsilkilize na kumtafuta.
wapendwa simulizi ya kugeuka sura Bwana wetu Yesu Kristo mbele ya wanafunzi wake watatu mlimani Tabor ni kielelezo wazi kwa wafuasi wake kwamba mateso na utukufu vinaambatana na hiyo ni sifa na utukufu wa Mungu. Wapendwa kabla ya tukio ya kugeuka sura watu wengi hata mitume walikuwa bado hawajamtambua Yesu ni nani. Yesu alipo wauliza swali “Wengi husema Mimi ni nani?” walishindwa kulijibu swali hili kwa ufasaha. Kwa nafasi hii mtume Petro anafanikiwa kujibu swali hilo vizuri kuwa Yesu ni Masiha, Mwana wa Mungu baada ya kupewa ufunuo na Mungu Baba. (Mt16:13-15) Yesu anapoona wanafunzi wake wamemtambua yeye ni nani, tukio linalofuata anawafunulia yatakayompata. Anatabiri juu ya mateso, kifo na ufufuko wake. (Mt 16:21-22) Cha kushangaza tena Mtume Petro hakubaliani na mpango wa Yesu kupitia mateso na kifo cha msalaba. Basi mwishoni Yesu anahamua wazi kutoa fundisho zito kwamba anayetaka kuwa mfuasi wake,auchukue msalaba wake na kumfuata katika njia yake ya mateso. (Mt16:24). Basi mara baada ya fundisho hili baada ya siku sita Yesu anawachugua Petro, Yakobo na Yohana ndunguye huku akigeuka sura.
Ndugu zangu basi tulifafanue tukio hili la Yesu kugeuka sura na kuona yaliyomo. Injili iko wazi na tumesikia kuwa Yesu aligeuka sura mbele ya wanafunzi wake Petro, Yakobo na Yohane. Tunaweza kujuliaza kwa nini awa wanafunzi watatu kila mara wanaonekana kwenye matukio na Yesu: kwa mfano tukisoma Luka sura ya 8: 40-56 tutasikia tukio ya uponyaji wa mwanamke alie tokwa na damu kadiri ya miaka kumi na miwili pia Yesu anamfufua binti wa Yairo na ukiendelea hadi mustari wa 51 utasikia ivi: alipofika nyumbani hakuchukua mtu kuingia pamoja naye, ila Petro na Yohana na yakobo…hata tena katika bustani ya gestemani walikuwapo… lakini tutambue kwamba tukiambatana na kumfuate yesu tutafunuliwa mambo mengi kwa sababu Yesu katika injili ya Mathayo sura 13:11 aliwaambia mitume hivi: Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa. Na mmja ya siri ya ufalme wa mbinguni ni tukio ya kugeuka sura Bwana wetu Yesu.
Wapendwa katika tukio ya kugeuka sura ya Bwana wetu Yesu Kristo tutambue mambo ifatavyo: Mosi Katika tukio la Yesu kugeuka sura walitokea Musa na Eliya wakiwa wanazungumza na Yesu. Tunasoma katika maandiko Matakatifu kuwa:Waisraeli waliongozwa na wingu kule jangwani(Kut13:21). Wingu liliifunika hema ya kukutania(Kut 40:34).Pia Musa alipokea amri za Mungu juu ya mlima uliofunikwa na wingu (Kut24:16-18) Je kiini cha mazungumzo yao kilikuwa nini? Muenjili Luka peke yake anatujulisha kuwa walizungumza juu ya kifo cha Yesu ambacho kingekamilishwa kule Yerusalemu(Lk.9:31). Kwa upande mwingine uwepo wa hawa wawakilishi wawili Agano la Kale hutoa ushuhuda kuwa sheria na manabii vinapata utimilifu katika Yesu Kristo mkombozi kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake.
 
Pili Wapendwa katika hali ile ya utukufu waliyoonjeshwa wafusi wa Yesu: Petro, Yakobo na Yohane pale mlimani, iliwavutia na kuwafurahisha sana.Wakatamani hali hiyo iwe ya kudumu hata wakataka kubaki pale Mlimani.Rejea pendekezo la Petro,nitajenga vibanda vitatu; kimoja chako Wewe, kimoja cha Musa na Kimoja cha Eliya. Petro kama myaudi anakumbuka namna gani wayaudi wanavyo sherekeye sherehe ya Vidanda katika siku sita ao 8. Katika sherehe ya vibanda wayaudi kwanza wanamshukuru Mungu na kukumbuka ukombozi wao utumwani Misri, huku katika jangwa walijenga vibanda na kuwasha taa  wakiimba zaburi na kucheza huku wakimsifu Mungu, kutoa sadaka na angona tena kwa Mungu pia kumuomba na kusubiria ujio wa Masiya kwao…ukisoma Mambo ya walwi 23: 33-34, kumbuku ya Torati 16: 13-16… sasa Yesu akagundua kwamba Mtume Petro anafunuliwa tena na Mungu kwa mara ya pili kusudi afahamu vizuri mafumbu matakatifu lakini bado kwanza mda wakumushudia Masiya ulikua aujafika na pili kuna kasoro katika kuelewa kwake kuusu Masiya basi kwa ujio wa Masiya sio kwa wana waisraeli tu kwakulinjenga hema tatu ya Yesu-Musa-Eliya lakini kwa kulihubiri injili popote ulimwenguni. kwa hiyo anawakemea mitume watunze siri hadi pale wataimarika kwa kushudia mateso-kufa na ufufuo wake. Na hayo hutimishwa katika injili ya Yoane sura 7:1-4: na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya, maana hakutaka kutembea katika uyahudi, kwa sababu wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Na sikukuu ya wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, ondoka hapa, uende uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Na haya tunashuhudia katika kitabu cha matendo ya mitume mara baada ya ufufuko Yesu Kristo Petro na Mitume wenzake walihubiri injili bila woga na kwa watu wote.

tatu kitu kingine kinachoambatana na tukio la Yesu kugeuka sura ni sauti kutoka katika wingu: Huyu ni mwanangu, Mpendwa, ninayependezwa naye, msikieni yeyeWapendwa katika Biblia neno Mwana wa Mungu ni jina alikua napewa mfalme wa wayaudi katika Yerusalemu na mfalme kwao nimwakilishi wa Mungu pili neno Mpendwa ni jina aliopewa Mtumishi wa Mungu. Na ukisoma Isaya 42 utasikia wimbo wa kwanza wa mtumishi wa Bwana: Tazama Mtumishi wangu, nimtegemezaye naye, mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye. Nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa  hukumu. Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia yake…Bila shaka Mtumishi wa Bwana, Mwanae Mpendwa ni Yesu Kristo na ndiye yeye Masiya wa kwaeli. Ndio sababu Mungu anatualika kumsikiliza Yesu Masiya aliechugua hali yetu ya kibinadamu ili atukomboe. Na haya Mitume wanaoshudia leo Mungu aliwagizi wanawe tangu zamani. Rejea Kumbu kumbu la Torati sura 18: 15: Bwana, Mungu Wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndungu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye. Na mwishoni kabisa nabi Danieli anatuambia hivi: Nikaona katika njozi za usiku na tazama, mmja aliye mfano wa mwanadamu akaja na mawingu ya mbingu; akamkaribia huyu mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.


KATIKA MAISHA
Wapendwa simulizi la kugeuka sura Bwana wetu Yesu mbele ya wafuasi wake ni ufunuo wa utukufu wa yesu atakaoupata kwa njia ya mateso,kifo na ufufuko wake. Hali hiyo ni mwanzo wa kuimarisha wito na imani wa mitume na kuwafanya kusudi wakuwe tayari kuyapokea, kumfuata na kushiriki katika mateso na utukufu wa Kristo kadiri ya mpango wa Mungu Baba. Nasi leo, tunafunzwa kuwa tayari kuyapokea mateso tunayopata katika kutekeleza  wajibu wetu wa kumfuata Kristo kwa sababu utimisho wa mateso yetu ni msalaba wa yesu unao tuletea uzima.
Kwa kushirika katika mateso na utukufu wa Kristo ni kuwa tayari kuyabeba msalaba yetu na kuyapeleka kwa Yesu yeye aliye itimisho wa mateso katika kuteswa, kufa na kufufuka kwake. Basi wapendwa ,Wazazi wanahimizwa  wawe tayari kuyavumilia magumu au mateso wanayoyapata katika kuutekeleza wajibu  wa kikristo kama wana ndoa pia kwa kuzingatia malezi bora kama wazazi kwa watoto wao.  Yawapasa kuvumiliana tofauti zao kitabia , kimawazo, kiafya Pia kwa uvumilivu na saburi wanapaswa kuwatunza na kuwalea watoto wao ipasavyo bila kukata tamaa. Lakini kumbukeni familia bila mwongozo wa Yesu ni migogoro na ungovi kila siku.
Sisi tuliowanafunzi ni lazima tuwe tayari kuvumilia mateso tunayoyapata katika kuitafuta elimu na kufahamu kwamba hakuna pasaka bila ijumaa kuu wala hakuna furaha bila mateso. Basi tuwaoneye wazazi wetu huruma na tuwape faraja kwa kuonyesha juhudi yetu ya kuwa tayari kupambana na shule kusudi maisha yetu ya kesho yawe mazuri. Na leo kwa namna ya peke tunakumbuka siku ya wanawake dunia, siku kama hiyo kwenye ninyi wanawake iwe siku ya kuthamini maisha yako kwanza kama mkristu, kama mwanamke mwanafunzi na tatu kama mama wa kesho atakaye boresha taifa yetu nzima ya Afrika. Tutambue kwamba mwanamke akipewa elimu, dunia inaona nuru.
Mapadre,walimu na walezi,wanawajibu mzito zaidi. Kutuandaa sisi vijana, sisi tuliotofauti kwa vitu vingi si kitu rahisi.Wanatumia nguvu, akili, muda, mali nk kutuunda kiroho, kiakili, kimaadili  ili tukawafae watu wa Mungu na kuwaongoza vema kwake. Ni mateso walioyonayo kwaajili ya kumfuata kristo. Basi tuwape ushirikiano uku vile vile pia matufundishe kwa uvumilivu na upendo bila kochoka ao kukata tama. Wapendwa katika Kristo wakati huu wa kwaresima tujitahidi kumfuata Kristo katika njia hii ya msalaba yaani kuishi maisha ya sadaka kwa Mungu na jirani. Tutekeleze wajibu wetu wa kikristo kwa uaminifu wote ili jitihada zetu za kumfuata Kristo mteseka zitupatia matunda mazuri ya kwaresima


Shemasi Bienvenu Kabeya Kungwa Ngungwa Poulain Loquace, SDS

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

MAHUBIRI YA SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A WAKANISA: ROHO MTAKATIFU HULITAKATIFUZA KANISA

MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA

MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA