MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA
MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI
KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA
Somo I : Kut 12 :1-8,
11-14
Somo II : 1Kor 11 :23-26
SomoIII: Yohane 13:1-15
SALA: Tuwaombee
mapadre wote ili Mungu awajalie juhudi na ujasiri wa kuwahudumia Taifa lake
lote bila ubaguzi wa rangi ao wa taifa tena wabaki imara katika wito wao kila
siku ya maisha yao.

UTANGULIZI
Leo Mama Kanisa anaadhimisha Alhamisi
Kuu, mmja kati ya siku kuu tatu kabla ya kusherekeya mafumbo ya imani
na matumaini ya wokovu wetu sisi wakristu: ndiyo Pasaka ya Kikristo yaani kuteswa,
kufa na kufufuka Bwana wetu Yesu Kristu. Katika ukumbusho wa siku ya leo Bwana wetu Yesu
Kristo pamoja na wanafunzi wake, saa chache kabla ya kukamatwa na kuhukumiwa
kifo, alikula karamu ya mwisho. Katika karamu ya mwisho, alionyesha mfano wa
kuishi Amri ya Mapendo na akaweka Sakramenti mbili muhimu kabisa
ndizo: Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Sakramenti ya Daraja Takatifu
(Upadre).
UFAFANUZI
Katika Somo la kwanza tunasikia historia ya wana wa Mungu wakiongozwa na
Musa kuhusu desturi ya hizo za Pasaka: Kawaida na desturi hizo za Pasaka na za
Mkate usiotiwa chachu zilikuwa kawaida mbalimbali mwanzoni. Kiwalisia Sikukuu
ya Pasaka ni hasa desturi ya Wachungaji na Wafugaji wa wanyamawatoao wazaliwa
wa kwanza kama sadaka. na Sikuu ya Mkate usiotiwa chachu ni desturi ya Wakulima
watoao mazao ya kwanza ya ardhi kama sadaka. Punde si punde desturi hizo mbili
zikaungana katika sikukuu moja.
Lakini tutambue kuwa desturi hizo za Pasaka na za Mkate usiotiwa chachu yamepata
maana mpya wakati Waisraeli kwamwongozo wa Musa walipotoka nchini Misri: na
ikawa kwao ishara ya wokovu. Basi wapendwa, Pasaka ya Waisraeli yadokeza Pasaka
ya Wakristo, yaani wokovu ulioletwa na Kristo: Mwanakondoo wa Mungu
amejidhabihu msalabani, alijitoa kama chakula katika karamu ya mwisho katika
juma la Pasaka ya Waisraeli.
Ndio maana kwetu sisi wakristu Agano Jipya ni hitimisho ya Agano la Kale:
kwa hiyo Pasaka ya kiyahudi ni mwanzo wa safari ya wokovu wa ulimwengu mzima.
Basi Kristo ameiletea dunia yote wokovu kwa karamu yake na msalaba wake. Kadiri
ya imani yetu sisi Wakatoliki tendo lilelile la karamu na msalaba linaendelezwa
na Kristo katika Misa Takatifu iliyo karamu na sadaka ileile ya Kristo.
Ndio sababu katika somo la pili Mtume Paulo anatuenyesha kusimikwa kwa
sakramenti ya Ekaristi Takatifu kama wasimuliavyo wainjili. Wapendwa Ekaristi
ni Karamu ya wakristo inao wakumbusha sadaka ya Yesu kama kondoo aliechinjwa
kwa ajili ya utakaso wa ulimwengu nzima: kwa hiyo Ekaristi ni upendo na huruma
wa Utatu Mtakatifu kwa ulimwengu pia ni ishara ya umoja na ushirika wa wakristu
wote.(1Kor 10:16). Kwa hiyo Ekaristi Takatifu hutuunganisha Wakristo wote kuwa
ndugu. Pia kila tunapokula vema karamu hiyo tunashiriki na kutangaza kifo na
ufufuko wake Kristo.
Lakini hatuwezi kushiriki pamoja kama ndungu bila upendo, bila kiongozi
kati yetu, bila msaidizi ao wasaidizi ao wahudumu... ndio maana somo letu la
injili linatuonesha kwa kina juu ya uwekaji wakfu wa Ekaristi Takatifu na
Daraja la Upadre na Yesu Mwenyewe: na hayo yote aliyafanya kwa upendo mkuu: kwa
maneno haya “Fanyeni hivi kwa ukumbusho
wangu”. Yesu anaweka wakfu Sakramenti ya Ekaristi Takatifu na Daraja
Takatifu la Upadre. Chakula chetu cha roho cha kila siku ni Ekaristi, Wahudumu
au Waandaaji ni Mapadre, wakiongozwa na sera ya Upendo.
KANINSA NA EKARISTI
Wapendwa kwanza tutambue kwamba Ekaristi hukamilisha kuingizwa katika
Ukristo.Wale walionuliwa katika heshima ya ukuhani wa kifalme kwa Ubatizo na
kufananishwa kwa ndani zaidi na Kristo kwa Kipaimara, hushiriki pamoja na jumuiya
yote katika sadaka moja ya Bwana pia ni chemchemi na kilele cha maisha yote
ya kikristo. Sakramenti nyingine, kama zilivyo pia huduma zote za kanisa za
utume, zaungana na Ekaristi na zaelekezwa kwake: kwani katika Ekaristi takatifu
mna kila hazina ya kiroho ya kanisa, yaani Kristo Mwenyewe, Pasaka wetu.(KKK
1322-1324)
Tena Ekaristi ndio ishara thabiti na sababu ya hali ya juu kabisa ya
ushirika katika uzima wa kimungu na umoja ule wa Taifa la Mungu ambao
unalifanya Kanisa liwepo: Ekaristi ni kilele cha tendo la Mungu la
kuutakatifuza ulimwengu katika Kristo, na kilele cha tendo la kumwabudu Mungu
wampalo watu Kristo, na kwa njia yake wampalo Baba katika Roho Mtakatifu.(KKK
1325) Na mwishowe, kwa njia ya adhimisho la Ekaristi tunaungana tayari sisi
wenyewe na liturjia ya mbinguni na tuaanza kutangulia kushiriki uzima wa milele
Mungu atakapokuwa yote ktika wote.
Kwa nini sakramenti ya Ekaristi? Mwokozi wetu kama vile tulivyo sikia katika
injili: katika karamu ya mwisho, usiku alipotolewa, aliweka sadaka ya Ekaristi
ya Mwili wake na Damu yake. Alifanya hivyo ili kuendeleza sadaka ya msalaba
siku zote mpaka atakaporudi, kusudi amwachie Bibi Arusi mpendwa, yaani Kanisa,
ukumbusho wa kifo chake na ufufuko wake: sakramenti ya upendo, umoja, kifungo
cha mapendo, karamu ya pasaka ambamo Kristo huliwa, na roho ujazwa neema, na
ambamo tunapewa amana ya uzima wa milele.(KKK 1223)
Ndio maana yeye Mwenyewe usimika wazi sakramenti ya Upadre kwa hiyo katika
utumishi wa kanisa wa mhudumu mwenye daraja, ni Kristo Mwenyewe aliye katika
kanisa lake kama kichwa na mwili wake, mchungaji wa kundi lake, kuhani mkuu wa
sadaka ya ukomnozi, mwalimu wa Ukweli: basi mapadre ni wahudumu wa Kristo kwa
taifa lake. Wajibu huo alioutoa Bwana kwa wachungaji wa taifa lake, ni huduma
halisi. Wamtegemea Krsito na ukuhani wake mmja na umewekwa kwa manufaa ya watu
na jamii ya Kanisa.
UTUMISHI
Basi ndungu zangu Yesu kama Mwalimu anatoa mfano kwa kuwaosha miguu
Wanafunzi wake kwa maana: kuwakumbusha watumishi wake kwa upekee na wakristu
wote kwa jumla kwamba (mtumishi yaani padre kwa sakramenti ya upadre ao wakristu
wote kama mapadre kwa sakramenti ya Ubatizo) lazima kuwa mdogo mbele ya watu na
kuwa mhudumu wa watu bila kujidai maslai binafsi bali kuwatumikia watu bila
kujibakiza hayo ndio maana ya kuwa mtumishi wa Mungu.
Basi adhimisho ya siku ya leo (Alhamisi Kuu) tunasherekeya MAMBO matatu mapya: Sakramenti
ya Ekaristi Takatifu yaani Chakula cha
Wakristo, Sakramenti ya Daraja Takatifu (Upadre) yaani Huduma na Amri ya Mapendo- Sera
ya Kanisa. Hivyo kila mara tunapsherekeya Misa Takatifu
zinazoadhimishwa na Mapadre popote duniani: tunakumbuka upendo wa Mungu kwetu
kwa kutupa chakula yaani Mwanae Mpendwa, kwa kutupa wa hudumu mapadre ni mwisho
kwa kutupa Amri kuu ya mapendo ambaye ni sera ya Kanisa letu: kwa hiyo
tunaalikwa kuwa watu wa imani kwa Yesu, kwa kuliheshimu Kanisa na Viongozi wake
na kwa kusaidiana, kuvumiliana na kupokeana sisi kwa sisi katika hali zetu zote
ngumu na rahisi; tukiongozwa na sera ya Upendo.
SHEMASI BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS
Commentaires