MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 3 YA PASAKA / DOMINIKA YA EMMAUSI: KAA PAMOJA NASI EE BWANA WETU YESU KRISTO KILA SIKU YA MAISHA YETU
MAHUBIRI YA DOMINIKA YA TATU(3) YA PASAKA/ DOMINIKA YA EMMAUS: KAA PAMOJA
NASI EE BWANA WETU YESU KRISTO KILA SIKU YA MAISHA YETU
MASOMO
Somo la kwanza: Mdo 2:14, 22-28
Somo la pili: 1Pet 1:17-21
Injili: Lk 24:13-35
SALA: Ee Bwana Yesu Kristo na
Mkombozi wetu, asante kwa kuwa nasi kila siku katika safari yetu ya imani
katika furaha ao katika mangonjwa kwa hiyo tunakushukuru sana na kukutukuzwa
basi ee Bwana utuimarishe zaidi katika imani yetu na hasa zaidi utupoe katika
janga la ungonjwa wa corona.
UTANGULIZI
UFAFANUZI
Wapendwa
katika Kristo, tunaweza kujiuliza ni kitu gani ambacho kinamfanya Mtume Petro
zaidi pia na mitume wengine kusimama imara na kumuhubiri Kristo kwa wale ambaye
waliwatishia kuwauwa mara baada ya kumwangamiza kiongozi wao Yesu? Kwa sababu
Petro alionesha woga hadi kumkana Yesu na kupungukiwa imani yake, ni nini leo
anamfanya kuwa askari hodari wa injili bila kuwaogopa tena watu wa karne yake:
wapendwa jibu sahihi ambayo lilihimarisha tena Imani ya Petro na wenzeka na pia
inao tuunganisha wewe na mimi leo na kuitwa tena wateule wa Mungu ni TUKIO YA UFUFUKO
WA YESU. Basi ndugu zangu ufufuko wa Yesu ni mwanzo wa
maisha mapya ambao kwa njia ya ubatizo wetu tunaalikwa na mama Kanisa kuwa
mashaidi wa ufufuko huo na kuwa tayari kuhuburi injili kwa mataifa yote kama
wamisionari.
Ndio maana katika Somo la kwanza litokalo
katika kitabu cha Matendo ya Mitume Petro na wanafunzi mitume kumi na mmoja
ufafanua vizuri Tukio la Yesu kusulubishwa na kufa msalabani ambalo
liliwakatisha tama wasikilizaji na wafuasi wa kwanza, kwani hawakutegemea kuwa
Kristo aliyefahamika kwao kama mfalme mwenye nguvu na Mesiha afe kifo cha aibu
kama kile. Ndiyo hapo Petro anapochukua jukumu la kuwajibu na kuwaeleza kuwa
kifo cha Kristo Yesu msalabani ulikuwa ni mpango wake Mungu wa kuwakomboa
wanadamu (Mdo 2:23). Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu na hivyo kuibuka
mshindi dhidi ya mauti na dhambi (Mdo 2:23-24).
Na ni kupitia hofu, kukata tama na upungufu wa
imani wa wanafunzi wa kwanza wa Yesu uliomfanya Yesu kuwatokea mitume na
wanafunzi na leo katika injili Mwinjili Luka anatuonesha jinsi Bwana Mfufuka
anavyowatokea wafuasi wake wawili katika kijiji cha Emmausi. Baada ya Ufufuko
wake, Yesu aliwatokea Mitume na wafuasi wake maranyingi ili kuwasadikisha ya
kwamba amefufuka kutoka wafu. Na pia alitaka kuwaimarisha katika imani yao
ambayo ni msingi wa matumaini, sababu twatumaini wenyewe kufufuka tena baada ya
kufa kwetu. Yesu amefufuka akiwa wa kwanza wa wanaolala au akiwa limbuko lao
waliolaa (1Kor 15:20).
Kwa nini kila mara Mama Kanisa
katika kipindi cha Pasaka uwa natupa nafasi ya kutafakari tokeo ya kujionyesha
kwa Yesu mbele ya awa wanafunzi wawili?
Bila shaka Kanisa linatualika mimi na wewe leo
kutambuwa kwamba imani ambayo tunaoipata kwa kuona na kuzikiliza ni mwanzo wa
matumaini na imarisho ya kuweka wa missionari wa injili ya uzima yaani wa
ufufuko wa Yesu Kristo. Wapendwa katika Dominika hii tutazame zaidi tokeo la Emmausi
Kati ya wafuasi wawili wanaotokewa na Bwana Mfufuka mmoja anaitwa Kleopa, na
mwingine hatajwi jina lake, kila mmoja wetu anaweza kuweka jina lake ili
kumshuhudia Bwana Mfufuka.
Kwanza wafuasi ao wawili wanadokeza hali halisi ya
maisha yetu sisi kama wanadamu kila mara tunaposhindwa katika maisha yetu:
tunakata tama, tunaonyesha huzuni, hofu, aibu kwa sababu kwa akili yetu tunaona
kwamba maisha yetu aina tena na thamani... ndio maana kwa yale yote yaliyotokea
Yerusalemu baada ya kifo cha Kristo, baadhi ya wafuasi wake walitawanyika toka
Yerusalemu na Mitume wake walikuwa wamejifungia ndani ya nyumba kwa hofu ya
Wayahudi. Kifo cha Kristo kiliwafanya washindwe kuwa na Imani thabiti juu yake,
kwani hapo mwanzo walimwamini kama mfalme mwenye nguvu ambaye hakustahili kufa
kifo cha aibu kama hicho. Hiki ndicho kilichowafanya wafuasi hawa wawili kutoka
Yerusalemu kwenda Emau. Wakiwa katika safari yao, Yesu anawatokea na
anaambatana nao. Yesu anawadodosa juu ya kile walichokuwa wanaongelea. Nao
wanamweleza kwa huzuni na uchovu habari za Yesu Mnazareti aliyefundisha na
kutenda miujiza mingi na mwisho akatiwa mikononi mwa Mayahudi na kuuawa
msalabani... basi wapendwa nawalikeni tutafakari mambo muhimu inne(4) kutoka
katika injili ya leo ambao Mama Kanisa uwa nahadhimisha kila siku katika
hadhimisho ya misa Takatifu:
Mosi: Njia ya Emmausi uonyesha wazi kwamba
Maisha yetu yote ni safari, na katika safari hiyo tunakutana na vitisho, hofu
au wasiwasi pamoja na kukata tama kutokana na ugumu wa safari hiyo na mara
nyingu tunatenda dhambi kwa sababu ya upungufu wa imani. Hii ni sehemu ya toba katika hadhimisho ya Misa:
ndio maana tunaanza na kuungama dhambi zetu kabla ya kusikiliza neno la Mungu
na kushiriki chakula cha uzima wa milele yaani Ekaristi. Basi safari ya Emmausi
inatualika sisi leo kwanza kumwambia Yesu kila kitu bila kuficha: uzinzi wetu,
chuki, ugonjwa, umbea, wizi, umaskini, shida na mahakaingo zetu... pia kufanya
mahungamo ya kweli mbele ya Yesu kusudi tumupe nafasi ndani kusudi aje akae
nasi.
Pili: Yesu baada ya kuwasikiliza
anawaonya: Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote
walioyoyasema manabii. Je haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia
katika utukufu wake? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika
maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. Sehemu hii ya pili uonyesha wazi liturjia ya neno la Mungu ambaye Muhubiri ni Yesu Mwenyewe: wapendwa tutambue
kwamba kila mara padri anasoma injili na kuhubiri, kila mara msomaji
anasoma somo, ni Yesu Kristo anaeye tusomea kupitia msomaji, ni Yeye Mwenyewe
anae hubiri kupitia padre... basi lazima tuheshimu Neno la Mungu na
kuthamini ukubwa wake katika maisha yetu: wangapi wanasoma neno la Mungu
nyumbani? Wangapi leo wana Biblia? Katika simu zetu tunashindwa kuweka Biblia?
Tutambuwe kwamba neno la Mungu hutufanya tumtambue Kristo katika Ekaristi basi
bila neno hilo imani yetu ni bure.
Tatu: wakakikaribia kile kijiji
walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. Wakamshawisi
wakisema, kaa pamoja nasi... Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa
mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua,
kisha akatoweka mbele yao: sehemu hii ya
uonyesha wazi liturgia ya sadaka na Ekaristi Takatifu. Wapendwa neno
Ekaristi maana yake ni SHUKRANI, tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Mwanae Bwana
wetu Yesu Kristo, aliyekuja kutukomboa sisi wanadamu basi Ekaristi utufundisha
leo kuwa wamoja na wenyi ukarimu na upendo: mara ngapi tuko tayari
kupokea Ekaristi? tunapokea kwa mazoea ao tunaimani kweli yule mkate na divai
ni Mwili na Damu yake Kristo? Nasi pia macho yetu yanafumbuka pale
tunapopokea Ekaristi Takatifu na kumtambua Bwana Mfufuka kuwa yupo kati yetu
kila siku ya Maisha Yetu katika furaha ao katika shida ao taabu.
Inne: wakaambiana, Je Mioyo yetu
haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisemaa nasi njiani na kutufunulia
maandiko? Wakaondoka saa ile ile.... wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli. Nao
waliwapa habari ya mambo yale ya njiani... wapendwa sehemu hii uonyesha mwisho wa Misa takatifu ambalo tunatumwa
na Kaanisa kila siku baada ya kuungama, kuzikiliza neno la Mungu na
kushiriki Chakula cha uzima, kuwa wa missionari wa
injili ya Yesu Mfufuka kwa mataifa yote kila mmoja kadiri ya jikumu lake
ililolipata ndani ya Kanisa. Kuwa missionari wa Kristo ni kuwa tayari
kumweka Kristo mbele ya kila kitu, kujitoa bila kujibakiza na kujali uhai wetu,
kuwasaidia na kuwapa matumaini ya Yesu watu mbali mbali hususani wale walio
kata tama kwa ajili ya ugumu wa maisha, shida, taabu na mahangaiko, walio achwa
na kuzarauliwa na jamii, wanyonge na yatima, maskini na wakimbizi... kusudi kwa
utume wako wapate kuyaonja pia utufuku na uwepo wa Mungu katika Maisha Yao. Basi
wapendwa. Na mara tunapomtambua, basi tuende hima tukawapashe habari wengine
ambao bado hawajui ya kuwa Bwana amefufuka na ametutokea sisi. Habari hiyo
wataipokea kutokana na matendo yetu mema yanayodhihirisha uwepo wa Kristo
Mfufuka ndani yetu.
Tukifanya hivyo Petro katika somo la pili anaendelea
kutuonya kwamba kwa njia ya Yesu sisi tumepewa nafasi tena kumwita Mungu ‘Baba’
kwa sababu tumepokea toka kwake uzima mpya kwa damu ya thamani, kama ya
mwanakondoo asiye na hila. Basi tumwamini Yesu Kristo na tumfuate kusudi tupate
starehe ya milele.
SHALOOM
SHAMASI BIENVENU KABEYA
NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS
Commentaires