MAHUBIRI YA DOMINIKA YA PASAKA MISA YA ASUBUHI: YESU AMEFUFUKA KWELI KWELI TUSHANGILIE NA KUFURAHI
MAHUBIRI YA DOMINIKA YA PASAKA MISA YA ASUBUHI: YESU AMEFUFUKA KWELI
KWELI TUSHANGILIE NA KUFURAHI
MASOMO
Somo I: Act10: 34a, 37-43
Somo II: Col. 3: 1-4
Gospel of John 20: 1-9
SALA: Ee Bwana tunakushukuru kwa ku hitimisha siku 40 ya Kwaresima ambayo tulisafiri pamoja Nawe katika safari ya imani na matumaini ya wokovu wetu. Kwa Ufufuko wako, utufanye sisi leo tutambue uwepo wako katika maisha yetu ya furaha ao ya shida hususani katika kipindi hichi cha maradhi ya virusi vya korona. Amen.
UFAFANUZI WA
SHEREHE YA PASAKA
Wapendwa
katika Kristo, zaburi 118 inasema hivi: siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana,
tutashangilia na kuifurahia… Aleluya Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema kwa
maana Fadhili zake ni za milele. Israeli na
asema sasa, ya kwamba Fadhili zake ni za milele... Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la Pembeni. Neno hili limetoka kwa Bwana, nalo ni ajabu
machoni petu... wapendwa Taifa la Mungu,
Shaloom...
Bila shaka leo ni siku ya Furaha
Kubwa sana katika maisha yetu hasa zaidi katika safari ya maisha ya Imani na
Matumaini ya wokovu wetu. Sisi kama wakristu sikukuu ya Pasaka ni sera mpya, ni
mtazamo mpya, ni maisha mapya, ni ushindi ambayo umetufanya sisi tena kuwa
karibu na Mungu kwa sababu Yesu, kwa Kifo na Ufufuko wake ametupatanisha na
Mungu.
Wapendwa kwanza tutambue, Ufufuko
wa Yesu, ni uwepo usiohesabika wa Mungu katika maisha ya wanadamu... pili
Ufufuko wa Yesu unakuwa jibu ya Ukweli katika Imani na matumaini ya wokovu wetu
pia jibu katika maisha yetu ya taabu, mangaiko, mangonjwa yetu kwa sababu kwa
mateso, kufa na kufufuka kwake Kristo ni tukio kubwa katika historia ya yangu
na yako ambayo inabadilisha maisha yetu sisi wanadamu: kwa hiyo dhambi na
mangaiko zako, shida na ugonjwa wako, zinaweza kuwa njia ya furaha yako kubwa
kama tu utamruhusu Yesu Mfufuka leo aje na aingie kwako na kubadilisha maisha
yako.
Na hayo tunayapata katika somo
letu la kwanza na la Injili ambamo Petro na wafuasi wengine wa Yesu walikata
tamaa huku wakiwaogopa wayahudi kusudi wasiuwawe.
lakini baada ya kupewa habari ya Ufufuko wa Bwana, Petro na Yoane walienda mbio kusudi washuhudie wenyewe kwa sababu katika mila na desturi ya wayahudi mwanamke hawezi kutoa hushuhuda wowote katika jamii na pili ushuhuda unaweza kukubaliwa wakati wanaoshudia ni wanaume dhidi ya moja ndio maana walienda wawili kaburini. Lakini injili inatuonyesha wazi yule Mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza wa kufika kaburini: Akainama na kuchungulia... lakini hakuingia. Basi akaja Simoni Petro akimfuata, akaingia ndani ya Kaburi; akavitazama vitambaa...Basi ndipo alipoingia naye yule mwamafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akanona na kuamini.
lakini baada ya kupewa habari ya Ufufuko wa Bwana, Petro na Yoane walienda mbio kusudi washuhudie wenyewe kwa sababu katika mila na desturi ya wayahudi mwanamke hawezi kutoa hushuhuda wowote katika jamii na pili ushuhuda unaweza kukubaliwa wakati wanaoshudia ni wanaume dhidi ya moja ndio maana walienda wawili kaburini. Lakini injili inatuonyesha wazi yule Mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza wa kufika kaburini: Akainama na kuchungulia... lakini hakuingia. Basi akaja Simoni Petro akimfuata, akaingia ndani ya Kaburi; akavitazama vitambaa...Basi ndipo alipoingia naye yule mwamafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akanona na kuamini.
Wapendwa katika simulizi hi
tunapewa picha mbili ambayo mimi na wewe tunatakiwa kujiuliza: mimi ni mkristu wa
aina gani? Ni mkristu ambaye nasadiki tu pale ambapo naona ao naambiwa? Ao ni yule
ambaye nataka kushuhudia mwenyewe huku ni kigusa na kupapasa...? Bila shaka
Petro na Yohane (kila mmja kadiri ya imani yake kwa Yesu) wanatufunda kitu muhimu
katika safari yetu ya imani: Petro ambaye alifunuliwa na Mungu na kumtambuwa Yesu
kama Masiha bado taratibu alitakiwa kuimarisha imani yake, alianguka na kumkana
Yesu lakini alisimama na kutubu, leo hii Petro ambaye alipewa Ufunguo wa Ufalme
wa Mbinguni na Yesu bado halikua ajafahamu andiko, ya kwamba imempasa
kukufuka...lakini wakati alifungua moyo wake na kumwacha Yesu kupenya roho yake
na kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu, Petro alisimama imara na kuwa shujaa wa Yesu na
mhubiri wa Ufufuko wa Yesu bila woga wala shaka na haya ndio ujumbe wa somo letu
la kwanza...Ndugu, ata mimi na wewe leo tunaweza kuitwa wakristu lakini bado
tunaweza kushikwa na hofu na mashaka katika kumwamini Yesu laiki tukimpa Yesu
nafasi katika nafsi zetu na kwa uweza wa Roho Mtakatifu bila shaka tutakuwa pia
washujaa wa injili na wa Ufufuko wa Yesu.
Yohane ni mfano ya baadhi ya wale wanaitaji tu kuona kusudi waamini. Basi ndugu zangu labda mimi na wewe kwa sababu ya
ubinadamu na udhaifu wetu bado tunashindwa kuyaona haya mafumbo matakatifu ya
imani na matumaini ya wokovu wetu kwa hiyo Yesu kwa Ufufuko wake anakuja kuyafumbuwa tena
macho yetu ilio haribiwa na dhambi na kuyapa tena uwezo wa kuona vizuri kusudi
tuamini kama mtume Yohane. Kwa hiyo ndugu zangu: Kuona ni kutambua kwamba
Yeye ndiye Masiha na Mkombozi wetu ambaye kwa Umoja, Upendo, na Ushirikiano wa Baba Na Roho Mtakatifu, mimi na wewe leo tunaangaziwa tena na kuwekwa katika kivule cha neema ya Mungu. Lakini tunamwona zaidi Yesu kwa walio maskini, wafungwa, yatima… pio kumwona Yesu ni kutambua kuwa ni Dactari, Mlinzi na Msimamizi wa wetu,
waliozarauliwa, wasio na utu tena mbela ya wanadamu, wa shida na
mahangaiko yetu... basi tunayaona pale tu tunafanya kama vile Yeye Mwenyewe
alivyotuamuru na tukifanya hivi basi Pasaka itabadili mtazamo na fikra zetu ya
kibinadamu.
Sisi ambayo tulikuwa tumekufa,
tulikuwa tumeelemewa na kifo yaani tulikuwa katika giza ambao ilutufanya mimi
na wewe kutokuyaona maarifa na neema ya Mungu tena leo hii kwa Kifo na Ufufuko
wa Yesu, tumefufuliwa na sasa tunapewa nafasi tena ya kuishi karibu na Mungu na
katika neema yake. Na hiyo ndio Pasaka kwetu yaani akuna kitu chochote
kiwezacho tena kutuweka katika utumwa wa mauti: Yesu ameshinda Mauti na
kuturudishia tena utu wetu mbele ya Mungu: ndio maana mtume Paulo katika somo
la pili utusihi kuyatafuta kwanza yaliyo juu, kwa sababu tumefufuliwa pamoja Kristo.
Basi tumfuate na tumkiri huyu Masiha na Mkombozi wetu.
Shemasi Bienvenu Kabeya Ngungwa
Kungwa Poulain Loquace, SDS
Commentaires