MAHUBIRI YA DOMINIKA YA SITA YA PASAKA MWAKA A WA KANISA/2020


MAHUBIRI YA DOMINIKA YA SITA YA PASAKA MWAKA A WA KANISA/2020: YESU ALISEMA: MTU AKINIPENDA, ATALISHIKA NENO LANGU, NA BABA YANGU ATAMPENDA NASI TUTAKUJA KWAKE
MASOMO
SOMO I: Acts8:5-8, 14-17
SOMO II: 1Pet. 3: 15-18
SOMO III: John 14: 15-21
SALA: Tumuombe Mungu Baba Mwenyezi, kwa nguvu ya Mungu Roho Mtakatifu, awasaidiye wale wote ambao wanajitahidi kutafuta dawa ya ungonjwa huu wa corona waweze kufanikiwa ili Dunia yetu ipate amani na faraja ya Yesu-Kristo Mfufuka katika wafu na Mkombozi wetu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amen.



UTANGULIZI

Wapendwa Taifa la Mungu, SHALOOM: leo ni Dominika ya 6 ya Pasaka Katika Mwaka A wa Kanisa letu Katoliki la Roma. Wapendwa taratibu tunaelekea kuhitimisha Pasaka yetu ambao tunamsherekea Kristu, yaani Mungu na Mkombozi wetu alieshinda mauti kwa kufufuka katika wafu. Basi tukiwa na nia hiyo tuungane na masomo yetu la Dominika hii ya 6 ambao inadokeza ujio wa Msaidizi ambaye Kristu alituahidi mara kabla ya kufa kwake. Na Msaidizi huu ni MUNGU ROHO MTAKATIFU, yaani ROHO wa kweli ambaya atakuja kutuimarisha zaidi kiimani. Tutambue ya kwamba ujio wa Roho Mtakatifu aimanishi ya kwamba tunaanza tena ukurasa mpya wa wokovu wetu, APANA. Lakini Roho Mtakatifu: ni wakili, Msaidizi na Mshauri...anafanya kazi ileile kama Kristo. Maana yake Yeye ni Nafsi kama Kristo, ambaye anatuongoza kwenye kweli yote(Jn 16:13) na anamshuhudia Kristo.(Jn10:25, 15: 26 na tena 16: 8) Basi ndungu zangu, tukiwa na dhamira hiyo tumuombe Munga katika Dominika hii kusudi tujiandae kiroho vizuri ili Roho huyu tuliempokea siku ya Ubatizo wetu na kuimarishwa zaidi siku ya Kipaimara(confirmation) adumu ndani mwetu kama Msaidizi-Mungu ambaye utuonyesha na kutupeleka katika njia ya ukweli na ya imani ya wokovu wetu.
UFAFANUZI WA MASOMO
Wapendwa, katika somo la kwanza tunasikia ya kuwa Filipo kwa uweza wa Roho Mtakatifu na mara baada ya kushuhudia UFUFUKO wa Kristo, Filipo anamuhubiri Kristo. Wapendwa zawadi ya Roho Mtakatifu ambaye kitabu cha Matendo ya Mitume uongelea, utuonyesha wazi kuzaliwa kwa jumuiya(Kanisa la mwanzo) ambayo mwandishi Luka hutabiri kuwa jumuiya ya kimataifa ambayo imejijenga siku kwa siku kwa mafundisho ya Yesu na kwa nguvu na msaada wa Roho Mtakatifu. Ndiyo maana katika somo letu la kwanza tunasikia mji wa Samaria ambalo ulihazibiwa na kutengwa na wayahudi kwa sababu ya dhambi ya kila ina, leo umekubali Neno la Mungu kwa hiyo kuneemeka na kubarikiwa hadi kujaliwa Roho Mtakatifu.
Katika somo hili la kwanza ni vizuri kutambuwa kwamba kazi ya wokovu ya wanadamu ni ya Mungu tu. Sio kazi ya wanadamu wala ya wale walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kulihubiri injili. Swali la msingi kwetu leo ni kwamba: kweli mimi baada ya ubatizo wangu, mimi kama mkristu, na muhubiri huyu Kristu kwa watu katika kweli? Ni ishara gani ambalo watu wale watahubiriwa itokalo katika mahubiri yangu itawafanya wavutiwe zaidi na Kristo? Bila shaka matendo na mwenendo wangu, wako ao wetu ni chimbuko ya kuwavuta wengine kwa Yesu. Kama leo hii tunashindwa kuonyesha huruma kati yetu sisi kama wakristu, tunashindwa kusaidiana, tunashindwa kuishi uwaminifu katika ndoa yetu, wito wetu katika mahusiano yetu bila shaka tutashindwa kumuhubiri Kristo kwa ukweli na madhara yake ni kuwa watu wengine wanaweza kushindwa kuzikiliza Neno la Mungu kwa kasababu ya tabia na mwenendo wetu mubaya. Basi kila mmoja wetu ni mtume wa Kristu, ni muhubiri wa Kristo basi tutafiti kwanza maisha yetu kusudi Roho wa Kweli aje ndani mwetu kutusaidia kila siku katika utume wetu, familia na shuguli zetu za kila siku ili kwa matendo, mwenendo na mifano yetu wengine wavutiwe na Kristo.
Ndiyo maana katika injili Yesu aliwambia wafuasi wake na anatuambia sisi leo: Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele, ndiye Roho wa Kweli... sitawaacha ninyi yatima... wapendwa mara nyingi tunakutana na changamoto nyingi sana kuusu hali(nature) ya Roho Mtakatifu. Yesu Mwenyewe leo umwita MSAIDIZI MWINGINE maana MSAIDIZI KAMA YEYE, ambaya atakaa nasi hata milele. Basi wapendwa Roho huyo ni Mungu ambaye pamoja na Mungu Baba na Mungu Mwana(Kristo) hutimisha kazi ya wokovu wetu na hii ndio fumbo ya imani ya Kanisa letu: yaani Mungu Mmoja katika Nafsi Tatu. Basi tusitumiye vibaya tafsiri ya Biblia wala tusishindwe na mafundisho nyengine ambayo utuonyesha ya kuwa binadamu anaweza kukushushia Roho Mtakatifu ndani yako lakini tukishika amri ya Mungu na kuishi kiaminifu kila siku ya maisha yetu: Yesu atamwomba Baba, naye atatujalia Msaidizi yaani Mungu Roho Mtakatifu.
Katika imani yetu sisi wakristu wakatoliki, uzawaidiwa na Mungu Roho Mtakatifu siku ya Ubatizo wetu na uimarishwa zaidi siku ya kipaimara(confirmation) maana yake atuna budi tena leo kuzurula na kutangatanga kutafuta tena Roho Mtakatifu bali cha msingi wewe na mimi leo tunatakiwa kuishi katika imani ya kweli kusudi tupate kuona nguvu ya Roho huyu ndani ya maisha zetu, ndani ya familia yako, ndani ya kazi na shuguli zetu. Wapendwa kwa sababu ya upungufu wa imani yetu sisi leo tunashindwa kutambuwa msaada wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu. Kama kila siku tungelikuwa nafanya tafakari(meditation) ya maisha yetu tungetambua kweli Roho huyu anafanya mambo mengi sana ndani mwetu lakini sisi atuyaoni kwa sababu ya mazoea ya maisha yetu: 
Leo hii labda ulisafiri, ukivaa barakora(mask) na kuzingatia ushauri wa wahudumu wa afya na kazalika... na unaitimisha safari yako bila kupata ajali wala mahambukizi ya corona lakini unajisifia kwamba nilifanya service nzuri ya gari yangu, huyu dereva mzuri sana, nilijikinga vizuri kwa kutumia barakora kwa hiyo unachukulia kawaida kila tukio...lakini kumbuka kuko wale wengine binadamu kama wewe, waliozingatia kila kitu kama wewe lakini leo wametoweka kwa ajali, kwa ungonjwa wa corona... labda leo unaishi peke yako na watoto inawezekana mume ao mke wako kashafariki ao mumeshatengana, lakini watoto wanapata elimu, matibabu wanakuwa vizuri bila changamoto yeyote lakini unajisifia kwamba kazi yangu ni nzuri sana yaani na pambana sana mimi ni shujaa...ni vizuri. Lakini tambuwa kwamba kuna wale waliojaliwa elimu kubwa kuliko wewe, kazi nzuri kuliko ya kwako leo wameshindwa kufanya kazi kwa sababu ya ungonjwa fulani, kwa sababu ya vita na migogoro ya kila siku.... basi nilazima kumshukuru Mungu ambaya kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu wewe leo umeitwa baba ao mama wa mtu fulani...
Basi ndungu zangu kutambuwa uwepo wa Roho Mtakatifu ndani mwetu ni kujipimi kiroho kupitia sala. Bila sala sisi kama wakristu hatuwezi kufanyikiwa. Katika sala tunaboresha mahusiano yetu na Mungu pia tunampa tena nafasi Roho Mtakatifu atuimarishe zaidi. Katika sala tunakomaa zaidi ki imani na tunajaliwa vipaji vya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kulijenga kanisa lake Kristu basi wapendwa nilazima kutenga mdaa kidogo hata dakika tano tu kumshukuru na kumwomba Mungu kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu tustawi katika neema na imani.
Ndiyo sababu Mtume Petro katika somo la pili utukumbusha leo kwamba tuwe tayari sikuzote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu, lakini kwa upole na kwa hofu.(1Pet.3:15ff) maana yake hatuna budi ya kuwaogopa maadui zetu ambayo wanaweza kuuwa miili yetu kwa sababu ya Kristu lakini tubaki imara na kuwajibu nguvu ya tumaini lililo ndani mwetu ambayo ni UFUFUKO WA BWANA WETU YESU KRISTU: kwa hiyo nilazima kuwa na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale waukutano mwenendo wenu mwema katika Kristo.

SHALOOM NA DOMINIKA NJEMA
SHEMASI BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN LOQUACE, SDS


Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

MAHUBIRI YA SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A WAKANISA: ROHO MTAKATIFU HULITAKATIFUZA KANISA

MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA

MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA