MAHUBIRI YA DOMINIKA YA TANO (5) YA PASAKA MWAKA A WA KANISA : YESU KRISTO NI NJIA, NI UKWELI NA NI UZIMA
MAHUBIRI YA DOMINIKA
YA TANO (5) YA PASAKA MWAKA A WA KANISA : YESU KRISTO NI NJIA, NI UKWELI NA NI
UZIMA
MASOMO
Somo la I: Mdo 6:1-7
Somo la II: 1Pet
2:4-9
Somo la III: Yn
14:1-12
SALA: Kwa maombezi ya Mama yetu Bikira Maria, tusali kwa ajili ya wahudumu wote
wa afya ambao wanajitoa bila kujibakiza hadi kuhatarisha uhai wao kwa ajili ya
kuwahudumia wangonjwa wote hususani wale waliohasirika na ungonjwa wa corona-Cov-19
na pia tujiombee sisi wenyewe ili Yesu-Kristo Aliye Njia-Ukweli-Uzima atuongoze
kwenye njia bora na kutufundisha ukweli na mishoni atupe uzima wa milele. Anayeishi
na Kutawala daima na milele. Amen
UTANGULIZI
Wapendwa Taifa la Mungu shaloom. Leo
tunaadhimisha dominika ya 5 ya Pasaka katika mwaka A wa Kanisa. Na Neno la
Mungu leo utualika sote kumtambua, kumfuata na kumutumainia Yesu Kristo ambaye
anajifunua leo kwetu kuwa Njia-Ukweli-Uzima. Leo Yesu anatufundisha kwamba tusiogope wala tusihofu
kila mara tunapo kutana na shida, mahangahiko, mangonjwa, changamoto mbali
mbali bali tutambuwe ya kwamba Yeye Ndiye Njia ya mafanyikio yetu, Yeye Ndiye Ukweli
wa maisha yetu, mateso na shida zetuvna Yeye Ndiye Uzima wa familia zetu, wa mangonjwa
yetu… Basi wapendwa tusihangaike na kutanganga, kuzurula kutafuta njia, ukweli
na uzima ambao utokao kwa wanadamu lakini Yesu anakutaka wewe utakaye soma
mahubiri hii ubadilishe mtazamo wako pia uwe tayari kumpa Yesu nafasi katika
maisha yako, moyo wako, familia yako, mipango, shida, furaha, mateso na
changamoto zako. Kwa hiyo tutajaliwa Uzima tele (Cf. Jn10 :10) tutaonyeshwa
ukweli na mwisho tutafunguliwa njia ya uzima wa milele.
UFAFANUZI
WA MASOMO YETU TATU
Wapendwa somo letu la kwanwa
kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume utuonyesha wazi namna gani Mitume
kwa uweza wa Roho Mtakatifu walilijenga Kanisa la Yesu kwa matakwa yeke Mwenyewe.
Kwanza Mitume wilijagua kiini cha imani yao yaani Neno la Mungu. Wakisema: haipendezi sisi kuliacha
Neno la Mungu na Kuhudumu Mezani. Mitume waligunduwa na kusikiliza
manung’uniko ya wayahudi wa kiyunani juu ya waebrania kwa sababu wajane wao
walisahauliwa katika huduma ya kila siku. Na hapo walipendekeza kuwachagua watu
saba miongoni mwao lakini washuhudiwe kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na
hekima kusudi waweze kuwazaidia...
Wakawchagua: Stefano, Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na
Nikolao basi Mitume wakaweka
mikono juu yao. Wapendwa, katika desturi na mapokeo ya Kanisa letu Katoliki somo
hili utuonesha wazi uwepo wa mashemasi ndani ya Kanisa: mashemasi wapo kwaajili
ya kuwasaidia maaskofu na mapadre pia kuwahudumia watu na mara nyingi somo hili
linasomwa wakati wa upadirisho wa mashemasi basi pia leo tuwaombeye mashemasi
wetu wa mpito ao wakudumu wote kusudi Mungu azidi kuwaimarisha katika kazi ya
huduma wao.
Wapendwa somo hili utuonyesha
wazi changamoto tunazo kutana nazo katika vikanisa vyetu. Leo viongozi wengi wa
vikanisa vyetu, wanajenga imani na matumaini yao katika hela na mali ya dunia
na kuwahudumaza waamini yao na mbaya zaidi kuwagawanya wakristu matajiri juu ya
masikini na kusau kulihubiri habari njema ambaye ni Kristo Mwenyewe. Leo hii
tunafundishwa na wachunganji waovu kwamba pale ambapo unatoa kiasi kikubwa cha
hela basi utabarikiwa zaidi na Mungu... kumbukeni kwamba dominika ya 4 ya Pasaka
Yesu alituharifu tuwe makini kwani wachungaji waongo wapo na
wanatupotosha(Jn10:1-10) kwa hiyo wapendwa, wewe ambaye utusoma mahubiri haya
tambuwa kwamba Kanisa letu litastawi pale ambapo kila mmoja wetu atajitambuwa
kuwa jiwe lijengalo Kanisa ambalo Kristo Mwenyewe Ndiye Jiwe la Msingi.
Ndio maana katika somo letu la
pili, Mtume Petro utualika tumwendee Yesu, Jiwe lililo hai na uzima... Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmjengwa mwe nyumba ya
Roho, ukuhani mtkatifu, mtoe sadaka za roho, zinazokubaliwa na Mungu, ka njia
ya Yesu Kristo. Basi ndugu zangu, mimi na wewe tunaalikwa kwanza
kusafisha mioyo yetu na kuitoa kama sadaka kwa Yesu. Tambuwa, utajiri wako sio
funguo ya ufalme wa mbinguni pia vile vile umasikini wako sio funguo ya uzima
wa milele lakini utayari wako wa kumfuata Yesu na Kumwamini ni mwanzo wa wokovu
wako. Hata katika maisha ya ndoa: utajiri ao umasikini sio ufunguo wa kuwa na
ndoa nzuri ama wa kuishi kwa amani na furaha katika ndoa bali masikilizano,
uvumilivu, ukweli, huruma, kujali na kumwamini mwenza wako ni mwanzo wa kuishi
maisha ya raha katika ndoa yenu... hayo yote yatakuwa kwetu somo pale tu
tutampa Yesu nafasi apenye mioyo yetu.
Ndio sababu Injili yetu ya leo
kutoka kwa Yohane sura ya 14:1-12 utuonyesha wazi kwamba Yesu-Kristo Ndiye: Njia-Ukweli-Uzima: sura hii ya 14 ya injili ya
Yohane inatanguliwa na mafundisho ya Yesu ambao aliyatoa katika adhimisho ya
Karamu yake ya Mwisho tusomavyo katika sura ya 13 ya injili ya Yohane: Yesu
baada ya kutambuwa kwamba saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu
kwenda kwa Baba, aliwapa mafundisho kuusu upendo, na kuwaambia
yatakayompata yaani mmoja wao atamsaliti, habari ya kuondoka kwake na utabiri
wake kuwa Petro atamkana, wanafunzi wake wanajawa na wasiwasi na kujiuliza
maswali mengi. Lakini Yesu baada ya kuwafundisha
alitambuwa kwamba wanafunzi wake walishikwa na hofu na wasiwasi ili kuwaondoa
wanafunzi wake wasiwasi na kuwaimarisha katika imani Yesu anawaambia
wasifadhaike:kwa sababu mnamwamini Mungu, niamini
na Mimi. Yesu aliwaambia hivi kwa sababu alijua kuwa yuko njiani
kuelekea nyumbani mwa Baba ambomo mna makao mengi na ni Yeye Peke yake ambaye
utuandalia mahali, basi Tomaso anapata mashaka juu ya njia ya kufika huko
aendako Bwana, ndipo yesu anasema “Mimi Ndimi Njia, Ukweli na Uzima; mtu
haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi”. Filipo pia akamwambia, Bwana
utuonyesha Baba, Yatutosha. Yesu akamwambia: “Mimi nimekuwapo pamoja
nanyi siku hizi sote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona Mimi amemwona Baba...
Wapendwa mimi na wewe leo tunao
sababu ya kumshukuru Mungu kwa sababu uwepo wa Yesu kati yetu, mateso, kifo na
kufufuka kwake ndiyo habari njema na ya furaha inayotupa amani, imani, utulivu
na matumaini katika mioyo yetu na pia inatupa nguvu na ujasiri wa kuendelea
kukabiliana na changamoto na magumu katika kumfuata Kristo aliye Njia, Ukweli
na Uzima.
Kwanza tutambuwe kwamba Mitume
walipata shida namna ya kuyaelewa mafundisho ya Yesu kwani fumbo kuu la kifo na
ufufuko wake lilikuwa halijatimia. Ndio maana baada ya kushudia ufufuo wa Yesu
Mitume walisimama imara na kuhubiri bila woga. Sisi leo hatupaswi kuwa na
wasiwasi Yesu anasema kuwa ni Njia ambao Yeye mwenyewe kwanza alipita kwa
mateso, kifo hadi ufufuko wake. Pili Yesu anasema Yeye ni Ukweli kwa sababu
uwepo wake kati yetu ni baraka tosha, ni uponyaji, ni utajiri, mwangaza... na
tatu Yesu anasema yeye ni uzima kwa sababu Yeye alishinda mauti na Kufufuka
katika wafu. Yesu ni Alpha na Omega, Yesu ni Mzima jana leo na kesho na kwa
njia ya ubatizo wetu sisi sote tunaonyeshwa njia na ukweli na tumekimiriwa
uzima wa milele, pia kwa neema na huruma ya Mungu tonapoamua kumfuata kwa
ukweli na uhuru tunafunguliwa njia na kujaliwa uzima na ukweli na mwisho tunatumaini
kuingia katika utukufu wa milele ambaye Yesu Kristo uenda kutuandalia mahali.
Kwani sasa tunahangaika
na kutafuta njia za mkato? Kwa nini tunatafuta ukweli utokalo kwa wanadamu kama
sisi? Kwa nini tunatafuta uzima wa mda mfupi? Kwa nini tunaamini maneno na
mafundisho ya uwongo?
Tuliambiwa kupitia mitandao ya
kijamii(facebook, whatsapp…audio zikizunguka apa na pale) kwamba kuanzia tarehe
8 hadi 11 ya Mwezi huo wa Tano mwaka 2020 kutakuwa na giza kubwa: ma mashetani
watazunguuka na kutafuna watu wa Mungu... na tukaambiwa tununuwe chakula,
mishumaa na mkaa kwa sababu giza itakuwa kubwa mno zaidi...chakushangaza
wakristu wengi waliogopa na kuanza kujiuliza na kutafuta msaada kwa wale
wachungaji waovu... leo ni tarehe 9 bado mimi sijaona giza wala wale mashetani....
sasa ndugu zangu jenga imani yako katika Yesu-Kristo epukana na mafundisho ya
upotovu, umupe nafasi leo Yesu Kristo apenye roho yako, ndoa yako, shida yako, mchumba
wako, watoto wako, mahangaiko yako, mateso, furaha, magumu na kazalika
utaonyeshwa njia ya kweli, utajaliwa kutambuwa ukweli na kukirimiwa uzima.
Tusitafute miujuza itokalo
kwa watu wanao tuvizia kiimani kusudi watajirike... leo corona-cov-19 inaweza
kutupa fundisho kubwa kwa sababu wale walijidai kuwafufua watu leo mujiulize
kwa nini wanashindwa kuwaponya wangonjwa wa corona na kutupatia dawa lakini wanabalisha
misemo eti Mungu amekasirika, Mungu ametupiga, Mungu ametuazibu.... huku
wakiwadai sadaka na michango kusudi Mungu atuhurumie.... Hayo yote ni UWONGO na WIZI. Tutambue kwamba Mungu wetu anatupenda na
bado yuko nasi kila siku katika Maisha Yetu: Upendo wake na Uponyaji wake kwetu
ni Uwepo wa Yesu Kristo kati yetu ambaye alishinda Mauti na kutuonyesha Njia
sahihi ya Kwenda kwa Baba Aliye Ukweli na Uzima.
Magumu, matatizo, shida na mateso
ni sehemu ya maisha yetu ya kikristo kwani yeye Aliye Njia, Ukweli na Uzima
alipambana nayo hata akakubali kufa msalabani ili mapenzi ya Baba yatimie. Tusiwe
na mashaka wala wasiwasi tunapopata magumu au mateso hayo na kuona kama
tumepotea njia bali tujitahidi kuyaweka yote katika Kristo na kujiaminisha
kwake Yeye Aliye Njia, Ukweli na Uzima.
SHALOOM
SHEMASI BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN
LOQUACE, SDS
Commentaires