MAHUBIRI YA JUMAPILI YA 4 YA PASAKA MWAKA A WA KANISA 2020/ DOMINIKA YA MCHUNGAJI MWEMA: DOMINIKA YA MIITO TAKATIFU
MAHUBIRI YA
JUMAPILI YA 4 YA PASAKA MWAKA A 2020/ DOMINIKA YA MCHUNGAJI MWEMA: DOMINIKA YA MIITO
MASOMO
Somo la kwanza: Mdo. 2: 14a, 36-41
Somo la pili: 1Pet 2: 20b-25
Injili: Yohane 10: 1-10
SALA: Ee Mungu Baba yetu Mwema, tunakushuru sana kwa kutulinda wiki nzima, kwa
kutulisha na kutuopoa katika shida mbalimbali, tunakuomba tena hasa zaidi kwa
maombezi ya mama yetu Bikira Maria katika mwezi huo wa rosari takatifu,
utuzaidie kusudi kila mmoja wetu kadiri ya uweza wa Roho Mtakatifu aweze
kutambua wito wake na awe kweli mchungaji Mwema wa Dunia nzima pia utusaidie
kulishinda hili vita litokalo katika janga la virusi vya corona. Tunaomba hayo
kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen.
UTANGULIZI
Wapendwa leo tunaadhimisha Jumapili ya 4 ya Pasaka inaofamika kama Jumapili
ya Mchungaji Mwema. Yesu leo anatupa tena picha nyingine ya ukombozi wake
akijionesha kwetu kuwa Mchungaji Mwema ambaye anayefahamu kondoo wake huku
anawaita, anawalisha, kuwaongoza na kuwalinda. Basi kama Yeye ambaye ni Kichwa
la Kanisa letu Ndiye Mchungaji wetu Mwema, Kanisa inatupa nafasi leo ya
kuombea miito Duniani ili tupate wachungaji wema.
UFAFANUZI
Wapendwa imani ya Petro na wenzeka na pia inao tuunganisha wewe na
mimi leo na kuitwa tena wateule wa Mungu ni TUKIO YA UFUFUKO WA YESU.
Mungu kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu alimfufua Yesu katika wafu na Roho Huyu huyu
anawafanya Mitume leo kuwa kweli mashaidi wa habari njema, habari ya wokovu
ambaye ni Yesu Kristo Mwenyewe. Basi ndugu zangu
ufufuko wa Yesu ni mwanzo wa maisha mapya ambao kwa njia ya ubatizo wetu
tumejaliwa neema tena ya kuitwa na Yesu kusudi tuingiye katika zizi lake,
kulishwa pia kuongozwa na Yeye Mwenyewe ambaye tunamshuhudia leo kuwa Mchangaji
wetu Mwema pia kwa njia ya Ubatizo na Kipaimara tunajaliwa utakaso na vipaji
vya Roho Mtakatifu na tunaalikwa na mama Kanisa kuwa mashaidi wa ufufuko huo na
kuwa tayari kuhuburi injili kwa mataifa yote kama Mitume.
Ndio maana katika somo
la kwanza mtume Petro na wale kumi na mmoja siku ya Pentecoste mara baada ya
kupokea Roho Mtakatifu walisimama Imara na kuwahubiria watu kuusu habari ya
Wokovu ambayo itokalo kwa Yesu Kristu Mchungaji wetu Mwema: Petro aliwataka
watubu pia wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo, kusudi wapate ondoleo la dhambi ili
wapate kipawa cha Roho Mtakatifu. Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao na
kuonesha nia ya kubadilisha maisha yao basi kwa neema ya Mungu walibatizwa na
siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Basi wapendwa mimi na wewe leo ni vizuri mahubiri ya Petro na wale kumi na
mmoja yachome mioyo yetu kusudi kila mmoja wetu atambuwe mapungufu yake na
aweze kutubu ili nasi pia Roho Mtakatifu ambaye tulimpokea siku ya ubatizo wetu
na kuimarishwa zaidi siku ya kipaimra azidi kukaa ndani yetu. sisi wakristo kwa
ubatizo wetu tumefanywa kuwa makuhani, wafalme, na manabii. Kama makuhani
inatupasa kumtolea Mungu sadaka na kuwatakatifuza wenzetu kwa sala zetu.
Vilevile kama wafalme tumeshirikishwa katika utawala wa Mungu ambapo Kristo
ndiye Kichwa chetu na Mchungaji wetu Mwema. Na kama manabii inatupasa
kumuhubiri Kristo Mfufuka… lakini tutambuye bila Nguvu na Msaada wa wa Roho
Mtakatifu hatutaweza chochote bali licha ya kumuhubiri huyu Kristo
tutawahubiria watu kadiri ya maslahi yetu binafsi.
Ndio sababu Katika Injili Yesu anatupa tahadhari ya kuwa tuwe makini na
kutambuwa kuwa: Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, laikini
akwea penginepo, huyu ni mwivi naye ni mnyang’anyi lakini aigiaye mlangoni ni
mchungaji wakondoo… na mwishoni wa Injili Yesu anajitambulisha kwetu
kuwa Yeye Ndiye Mlango wa Kondoo, Yeye Ndiye Mchungaji Mwema, na yeyote
ataingia kwake, atapata malisho, ulinzi na mwishoni atajaliwa wokovu yaani
Uzima tele. Wapendwa kwanza nivizuri kutambuwa kuwa katika Agano Lakale
Mchungaji ni Mungu Baba, na kondoo, ni Taifa nzima la Israeli ambalo kwa ulinzi
wa wafalme wao na manabii walimlulia Mungu katika shida Naye aliwasikiliza na
Aliwakomboa.
Lakini kupitia manabii wale wale Mungu alihahidi ujio wa Masiha ambaye
atakuja kuwakombowa watu wake wote na kutakasa tena ulimwengu na viumbe vyote:
Huyu ni Yesu ambaye Petro katika somo la kwanwa anawahubiria wana Israeli ya
kuwa: tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo… kwa kuwa
ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa Watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali,
na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu Wetu wamjie. Maana yake
atuna budi kuzurula na kuhangaika kutafuta wachungaji wengine isipokuwa Yeye
alie fufuka katika wafu. Na hiyo inadhibitishwa katika waraka kwa Waebrania
sura 1: 1-2: Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa
sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika
Mwana, aliyemweka kuwa mriithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Pili Yesu anajitambulisha kwetu
leo kuwa Yeye Ndiye Mlango wa zizi la kondoo, Yesu anasema hivyo kasababu tu
anajuwa kuwa Yeye na Babake wanaisha katika umoja usiovunjika na umoja huo ni
upendo na uzima ulio kati yao. Sisi tunaunganishwa kwa uzima huo kupitia Yesu.
Manake Yesu ni njia ambayo utuunganisha sisi wanadamu na Mungu na Yohane katika
injili yake utuonyesha wazi kwamba Yesu ni Njia, Uzima na Ukweli.
Tatu kama leo Yesu Mchunganji
Mwema anatuita sisi kwa majina yetu ni kwa sababu Mungu Baba alimpa Jina, jina
la upekee ambalo limeandikwa katika kitabu cha uzima. Na Paulo Mtume katika
waraka wake kwa Wafilipi sura 2: 9-11: Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha
mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, na kwa jina la Yesu kila koti
lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi na kila
ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana kwa utufufu wa Mungu Baba. Pia
kama Yesu leo anatualika kusikiliza sauti yake na kumfuata ni kwa sababu Yeye
kwanza alisikiliza sauti Baba na kufanya mapenzi yake.
Na mwishoni kabisa Yesu
anatuhahidi uzima wa milele na kutukomboa kwa sababu kwa Nguvu ya Roho
Mtakatifu Mungu alimtukuza kutoka katika wafu kusudi mimi na wewe leo tupata
ondoleo ya dhambi na tujaliwe uzima wa milele.
Basi ndugu zangu Dominika hii ya
leo inatualika sisi sote, kila mmoja kadiri ya utume na nafasi yake ndani ya
Kanisa na Dunia kuchunguza na kutafiti wito wake huku tukitafakari maneno ya Yesu
ambayo utuonesha wazi tofouti kati ya Mchunganji Mwema na wachungaji wengine
waovu. Kila mmoja wetu ni mchungaji, lakini
tujiulize sisi ni wachungaji wa namna gani? Kweli tunafahu kondoo zetu? Tuko
tayari kuwahudumia na kuwalinda? Ya
muhimu kwetu ni kuwa Yesu Kristo Ndiye Mchungaji wa kondoo lake sisi ni vibarua
tu amboya tumeshirikishwa na Yesu kwa upendo wake Mwenyewe. Basi tusididai mno
kuusu uchungaji tuliopewa bure bila malipo wala rushwa Lakini tutambuwe kwamba
bila Nguvu Yake Mwenyewe na Nguvu ya Roho Mtakatifu, bila chembe ya upendo,
unyenyekevu busara na uvumilivu sisi hutuwezi kuitwa wachungaji wema bali
tutawanyanyasa kondoo na ku wapoteza. Tena wito wetu tunaupata katika zizi lake
Mwenyewe yani Kanisa letu ambaye Kristo ni kichwa maana yake kusikia na kufuata
sauti ya Kristo Mchungaji Mwema ni kuwa tayari bila kujibaliza kumruhusu Roho
Mtakatifu atuvute na kutuongoza kwenye Maisha ya Kristo na mafundisho ya Kanisa
kusudi tumshe ndani yetu tamaa, furaha na ujasiri wa kujitowa wenyewe na Maisha
yetu kwa ajili ya jumuiya yetu, familia zetu na mwishoni kwaajili ya utumishi
wa Ufalme wa Mungu.
Ndio maana Katika somo pili mtume
Petro anatuasa kubaki katika imani yetu hata kama ni katika mateso makali. Tunaaswa tuvumilie mateso, na tumwamini na
kumtegemea Mungu katika shida na raha hususani janga hili la corona leo. Mateso
yasiwe chanzo cha kutufanya sisi tutende dhambi. Inatupasa tumwige Bwana wetu
Yesu Kristu ambaye pamoja na kwamba hakuwa na dhambi, alivumilia mateso makali
ili aweze kutukomboa kutoka katika utumwa wa dhambi. Hivyo Bwana wetu Yesu
Kristu ni kielelezo cha maisha yetu kinacho tuelekeza kwa Mungu.
Shemasi Bienvenu Kabeya Ngungwa Kungwa Poulain
Loquace, SDS
Commentaires