MAHUBIRI YA SHEREHE YA ASCENSION- KUPAA BWANA: DOMINIKA YA 7 YA PASAKA MWAKA A WA KANISA 2020
MAHUBIRI YA SHEREHE YA ASCENSION-
KUPAA BWANA: DOMINIKA YA 7 YA PASAKA MWAKA A WA KANISA 2020
MASOMO
Somo I: Mdo. 1:
1 – 11.
Zaburi: 47
Somo II: Efe.
1: 17 – 23.
Somo III:
Injili. Mt. 28: 16 – 20.
SALA: Ee Mungu Baba yetu, kwa nguvu na msaada wa Roho Mtakatifu,
tunakuomba uwakinge wanafunzi wote ambao wanajiandaa kurudi shule katika
kipindi hiki kiguma cha ungonjwa wa corona-Cov-19 uwazaidia pia walimu wote ili
pamoja waepushe na ungonjwa huu ambao hadi sasa hauna tiba wala chanjo.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
UTANGULIZI
Wapendwa Taifa la Mungu, SHALOOM! Ndungu zangu, kwanzia
Jumamosi Kuu ya Pasaka katika Misa ya usiku ambamo mama Kanisa alihadimisha
sikukuu ya KUFUFUKA Bwana Wetu Yesu Kristu katika wafu hadi leo: Tunahesabu
siku 40 ambao ki liturgia na ki theologia ni Hitimisho ya katika kazi ya ukombozi wa Mungu.
Ndio maana kwa namna ya pekke, leo tunaadhimisha sherehe ya Kupaa Mbinguni
Bwana Wetu Yesu Kristo. Sherehe hii huadhimishwa siku ya arobaini tangu
kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristo, yaani PASAKA. Hivi leo ni siku ya
arobaini tangu Pasaka. Katika sherehe hii ya kupaa Bwana wetu Yesu Kristo mbinguni, tunasherehekea kule kuingia katika utukufu wa Mungu na kujichukulia
cheo cha juu, juu kabisa katika utukufu huo. Na pia tunaimarishwa na kupewa pia
matumaini ya kushiriki utukufu wa Mungu mwisho wa safari ya Maisha yetu hapa
duniani.
UFAFANUZI
Wapendwa katika Kanuni ya imani(Credo) yetu tunakiri kama
ifatavyo: Na sadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba
wa Mbingu na dunia. Na kwa YESU KRISTO, mwanaye wa pekee, Bwana wetu,
aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa...
akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimuni siku ya tatu akafufuka katika
wafu, akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi... wapendwa
kila mara tunapo kiri imani yetu, tunasadiki kazi ya ukombozi ya UTATU
MTAKATIFU katika safari ya wokovu wetu ambao Kristu yeye aliekuwa Mungu
alikubali kwa hiari yake Mwenyewe kuchukua ubinadamu wetu kusudi katika umoja wa
Baba na Roho Mtakatifu, mimi na wewe leo tusafishwe na kupewa neema tena ya
kuishi katika utukufu.
Basi tunapo sherekeya kupaa kwa Bwana wetu Yesu Kristo
tunasherekeya Umungu na Utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristu ambaye kwa kitendo
cha kupaa huitimisha kazi ya ukombozi wetu. Kwanza tunaweza kujiuliza: ni Yesu
peke yake ambaye katika safari ya mwanadamu alipaa kwenda mbinguni? Jibu ni
ndio. Hakuna mtu mwingine katika Biblia alipaa kama Yesu Kristo na kwenda
mbinguni. Kwa hiyo Henoko na nabi Elia hawakufa, lakini kwa mapenzi yake Mungu
na kwa imani yao walipelekwa mbinguni. Tusome Waebrania (Hebrew) sura 11: 5-6: kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala
hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha. Maana kabla ya kuhamishwa alikuwa
ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Lakini pasipo imani haiwezekani
kumpendeza... Tena mafundisho ya Kanisa leo hushuhudia kwamba Bikira
Maria Mama wa Mungu, alipalizwa mbinguni mwili na Roho.
Basi kitendo cha kupaa Bwana wetu Yesu Kristo utuonesha
wazi tukio la pekee la kimungu ambao udhihirisha Mwisho na pia Mwanzo. Ni
mwisho na hitimisho wa utume wa Yesu na vile vile tena ni mwanzo wa utume wa
mitume ambao utaimarishwa zaidi ya kazi ya Roho Mtakatifu katika kazi ya
kulijenga ao kisimika Kanisa na kutangaza ufalme wa Mungu kwa mataifa yote:
huku wakitumaini na kusadiki uwepo wa Yesu kati yao kila siku ya maisha yao.
Hayo tunayasoma katika injili ya Mathayo sura ya 28: 18-20: Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka
yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa
wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo nanyi
sikuzote, hata ukamilifu wa dahari. Kwa hiyo wapendwa, masomo yetu
ya leo utuonesha wazi simulizi ya kupaa kwa Bwana wetu yetu Yesu Kristu na
kuingia katika utukufu na kukaa katika upande wa kuume wa Mungu.
Basi kibiblia kupaa maana yake
nini? Kibiblia neno kupaa lina maana ya kuhama kwa mwili wa ufufuko
wenye utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo, kutoka duniani na kuingia Mbinguni. Na
maana nyingine ya kupaa ni hali ile ya kutukuzwa kwa Yesu ili apate kuwa mkuu
na mmiliki wa vyote duniani na mbinguni. Hivyo basi Kupaa ni tendo au hali ya
kurudia utukufu aliokuwa nao kabla hajachukua mwili kwa mama Maria yaani
umwilisho. Yesu amepaa
mbinguni kwanza, ili apokee tuzo kwa kazi nzuri alliyoifanya duniani,yaani kutukomboa
sisi wanadamu kutoka utumwa wa dhambi na mauti. Amekwenda kuvikwa taji ya ushindi. Kristo ni mshindi ameshinda dhambi
ambayo hupelekea kwenye mauti. Amepaa
kupewa taji aliloandaliwa baada ya ushindi huo mkubwa ambao kwa kupitia huo tumepewa uwezo wa kwenda kwa Baba.(rejea injili ya Marko sura16:19).
Pili tunaweza kujiuliza
ni lini Bwana wetu Yesu Kristo alipaa? Wapendwa, katika simulizi ya ufufuko wa Yesu, mwenjili
Yohane utuanikia kama ifatafyo. Tusome injili ya Yoane sura ya 20: 16-18: Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia, kwa
kiebrania, Raboni.(yaani mwalimu wangu) Yesu akamwambia, usinishike, kwa maana
sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndungu zangu ukawaambie, Ninapaa
kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Mariamu
Magdelene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya
kwamba amemwambia hayo.
Kwa maneno ya mwinjili Yohane, Bwana wetu Yesu Kristo, kwa kufufuka
kwake,aliingia katika utukufu yaani siku
hiyo hiyo ya kufufuka kwake, Kristo alipaa mbinguni. Hivyo hakukuwa na wakati
fulani uliopita kutoka ufufuko mpaka kupaa. Ndio maana mwinjili Luka katika
injili yake sura 23: 39-43 udhihirisha kama ifatavyo: Na mmoja wa wale
wahalifu waliotungikwa pamoja na Yesu alimtukana,akisema, Je wewe si Kristo?
Jiokoe nafsi yako na sisi. Lakini yule wa pili akamjibu, akamkemea, akisema,
wewe hamwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Nayo ni haki kwetu
sisi... kisha akasema, “Ee Yesu nikumbuke utakapoingia katika ufalme
wako,” Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia
, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”
Tunajifunza nini? Bwana wetu Yesu
Kristo alipaa mbinguni siku ya ufufuko wake lakini alijitokeza mara
nyingi kwa wafuasi wake na mitume kwa
muda wa siku arobaini, na leo ndio
siku arobaini tangu ufufuko wake,ili
wapate kuamini kuwa amefufuka. Mitume walipaswa kuamini kwanza
wao habari za ufufuko ili baadaye waweze kuwatangazia wengine juu ya
ufufuko wa Yesu, ambao ndio ulikuwa msingi wa matumaini na imani yao pia
ya imani na matumaini yangu na wewe utakae somo homelia hii. Mtume Paulo katika
waraka wake wa kwanza kwa Wakorinto sura ya 15:14 usema hivi: Tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na
imani yetu ni bure. Pia
aliendelea kuwatokea kwa lengo la
kuwaimarisha katika imani yao
dhaifu kabla hajawatumia
Roho Mtakatifu. Ndugu zangu katika Kristo, kwamaneno mengine siku arobaini zinamaanisha muda wa kutosha wa
maandalizi kumpokea Roho Mteakatifu siku ya Pentekoste.
Ndio maana katika somo la kwanza kutoka katika Metendo ya Mitume sura ya
1:11-11: Yesu anawahadia upeo wa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua, wale
aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya
kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu
ufalme wa Mungu... tena Yesu akawaambia mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu
yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yeruzalemu, na katika
Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Katika somo la kwanza tunaambiwa pia, watu wawili
walionekana wamesimama karibu nao wenye
mavazi meupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona
mmesimama mkitazama mbinguni? Atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake
mbinguni (Rejea. Mdo. 1:
11). Watu wa Galilaya ndio mimi na wewe leo. Ndio Kanisa. Kwa ubatizo
wetu tunashirikishwa katika umungu na kuzaliwa tena katika famila takatifu na
kupewa jikumu ya kumshuhudia na kumuhuburi Kristo kwa mataifa yote. Tena kwa
sakramenti ya Kipaimara(confirmation) tunaimarishwa na Yesu na tunajaliwa
vipaja vya Roho Mtakatifu ambao vinatufanya sisi kuwa askari hodari wa injili
takatifu kwa hiyo kazi yetu sio kusimama tu na kutazama juu na
kushangaashangaa, bali ni kutekeleza agizo la Yesu Katika injili yetu ya leo Mathayo
sura 28:19: Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote
kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho
Mtakatifu.
Maana yake Kanuni hii ya
ubatizo ilivyoandikwa na mwinjili Mathayo, inaonesha kuwa yeyote anayebatizwa anashiriki
maisha ya Mungu, ambaye ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hivyo, kila
mbatizwa lazima amwite Mungu Abba, yaani Baba. Kama ishara ya heshima na upendo
na kujiweka chini ya ulinzi wa Mungu, kama watoto wake. Kristo anatuahidia
atakuwa nasi mpaka utimilifu wa dahari. Hivyo basi, tujitahidi kufuata na
kutenda kama alivyotupa agizo la kanuni ya ubatizo ili tuwe naye mbinguni, na
kushiriki utukufu wa Mungu ambao utafikia utimilifu wake wote katika ujio wake
wa pili Kristo atakapokuja kwa utukufu.
Pia Yesu mwenyewe
alisema, “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi;
kama isingekuwa hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni
nafasi.” (Rejea Yn. 14:2). Kwa hiyo basi, kupaa mbinguni hapa utuonesha
njia ambao mimi na wewe leo tunatakiwa kupita kusudi sote tushirika utukufu wa
Mungu siku ya mwisho wa maisha yetu. Kama vile Yesu anavyoingia katika utukufu wa Babake,
ndivyo wafuasi wake na wale wote watakaotimiza mapenzi ya Baba yake ndivyo nao
watakavyoushiriki utukufu huo. Na nafasi ya kushiriki utukufu huo iko wazi kwa
kila mmoja wetu hapa: watoto, vijana, wazee-wake kwa waume, matajiri kwa
maskini; kila mtu ana nafasi ya kushiriki utukufu huo ambao leo Bwana wetu Yesu
Kristo tunamshangilia kwa kujinyakulia utukufu huo. Basi
tufanye nini kusudi tushiriki ufalme wa mbinguni?
Tukisoma injili ya Mathayo sura ya 16: 24-25 tutasikia
maneno ya Yesu ambao utuonesha masharti ya kumfuata: wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu yeyote akitaka kunifuata,
na ajikane mwenyewe, ajitikwe msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa
nafsi yake, ataipoteza, na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu,
ataiona. Basi wapendwa wangu, Yesu anataka kutuambia leo kuwa kila
mmoja anajaliwa baraka na neema ya kushiriku umungu na utakatifu ila
ajichukulie mwenyewe msalaba wake na kuupeleka kwa Yesu ambao kwa mti wa
msalaba wake sisi tunakombolewa. Msalaba waako ni yupi? labda msalaba wako ni
mume wako ambaye anashindwa kuteekeleza majikumu yake kama baba na kichwa cha
familia, ni mke wako ambaye kwa tabia yake mbaya unashindwa kuona furaha na
raha ya ndoa yako, ni maisha magumu ambao unakata tamaa na kupoteza matumaini,
ni magonjwa kama corona-Cov-19 leo ambao leo tunaogopa na kuheshimu
masharti(conditions) ya wahudumu wa afya kuliko hata amri ya Mungu, ni watoto
wako ambao wamenaswa na furaha na anasa ya dunia hadi kupoteza utu wao, ni
familia yako ambao kila siku uishi katika fujo, migogoro na ugonvi, ni tabia
yako ya usharati, ya uchoyo, ya wivi na ukorofi, ya chuki na tamaa, labda ni
uwongo na umbea wako... basi kila mmoja wetu anamsalaba wake basi Yesu
anakumbia leo usiogope wala usihofu njoo kwangu na msalaba wako nitakupa
faraja, uponyanji, furaha, ukombozi, utajiri wa mwili na roho na utashiriki
utukufu wa Mungu.
SHALOOM!
SHEMASI BIENVENU KABEYA NGUNGWA KUNGWA POULAIN
LOQUACE, SDS
Commentaires