MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 12 YA MWAKA A WA KANISA KIPINDI CHA KAWAIDA


MAHUBIRI YA DOMINIKA YA 12 YA MWAKA A WA KANISA KIPINDI CHA KAWAIDA
MASOMO
SOMO I: Yer.20: 10-13
SOMO II: Rom.5: 12-15
INJILI: Mt.10: 26-33
SALA: Ee Mungu Baba yetu, tunakusifu na tunakushukuru kwa sababu ya ulinzi wako kadiri ya juma nzima. Tunakuja mbele yako kuomba tena msaada wa wiki hii ili kwa nguvu ya Mungu Roho Mtakatifu tuepushwe na ungonjwa wa Corona pia uwasaidie wote ambao hadi sasa wanapambana na ugonjwa huu na uwarudishiye afya wale wote waliopata ugonjwa huo. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amen.
UTANGULIZI
Taifa la Mungu SHALOOM, TUMSIFU YESU KRISTU. Wapendwa baada ya Sherehe ya Pasaka, tulisherekeya sherehe ya Pentecost, Utatu Mtakatifu, Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristu na mwisho kabisa tulisherekeya sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu(sherehe hii ya Moyo Mtakatifu wa Yesu inaweza pia kuadimishwa Jumapili kwa wale ambao viongozi yaani maskofu waliamua hiadimishwe Jumapili lakini kwetu sisi tulisherekeya sherehe hii ijuma (Friday or Vendredi) ya wiki hii. sherehe zote izi inne utupa nafasi ya kutafakari kwa kina Upendo na Umoja wa Mungu katika kazi nzima ya uumbaji na ukombozi wetu pia utufunza kusudi tudumishe upendo na umoja huu kati ya Mungu sisi na pia kati yetu sisi kwa sisi kama wanadamu. Basi leo tunaendelea na Dominika ya 12 ya Mwaka A wa Kanisa katika kipindi cha kawaida. Wapendwa masomo yetu ya leo inatualika kuwa na nadhamira kama ifatavyo: tusiwaogope wauao mwili lakini ni afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum(enfer). Tumuombe Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu tubaki imara katika Imani yetu.
UFAFANUZI
Wapendwa mara nyingi katika Maisha yetu tunakutana na changamoto nyingi ambao inatufanya tukate tamaa apa na pale: kuna baadhi kati yetu wanakutana labda na Maisha magumu, wengine ni ndoa ambao inasumbua mume ao mke aeleweki, wengine ni Watoto ambao wanashindwa kuishi kadiri ya malezi ya wazazi na kumcha Mungu tena wengine ni shule, mangonjwa kama corona na menginevyo, wengine kutokupata mume ao mtoto… lakini tukiangalia kiuwalisia ya Maisha yetu, changamoto ni sehemu ya Maisha ya mwanadamu, kupambana na kujaribu kuvumilia na kutatua hizi shida ni mwanzo wa mafanyikio yetu asa Zaidi sisi tunao weka matumaini yetu kwa Yesu Kristu ambaye utusimamia Pamoja na Roho Mtakatifu katika Maisha yetu. Ndio maana katika somo la kwanza nabii Yeremia anakutana na changamoto ambao inahatarisha hata maisha yake, nabii anakata tamaa na kulia. Wapendwa  tukisoma Yeremia 1: 1-9: tutasikia simulizi ya wito wa nabii huu: Mungu katika neno lake lilimjia Yeremia na Kusema: kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa…. 
Lakini Yeremia akamwambia Bwana, tazama siwezi kusema, maana mimi ni mtoto lakini Bwana akamwambia: Usiseme, Mimi ni mtoto maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru kwake, …. Usiogope kwa sababu ya hao, maana mimi nipo Pamoja nawe nikuokoe. Lakini Yeremia baada ya kukutana na changamoto: yakutokukubaliwa na wana wa yuda, wanamkataa na wanatafuta kumuua nabii anaogopa na kulia hakishikwa na hofu. Yeremia aliishi katika wakati mgumu saana ambao waisraali walikutana na vita, hekalu likabomolewa hadi kupelekwa utumwani tena wa Babiloni… kwa izi shida zote ziliwafanya waisraeli kukataa maneno ya Yeremia yaani maneno ya Mungu na kutaka kumuua. Wapendwa nilazima kutambua kwamba kazi ya Mungu pia inachangamoto nyingi: unaweza kusemwa na wenzio kwamba huyu hana kazi ndio maana yupo kanisani, ao ni umaskini ndio maana amejifanya kuwa mkristu, hana wito huyu ni njaa tu ao unapo shuhudia ukweli leo katika ulimwengu wetu huu wa kisasa, unaweza kuonekana kama kero mbele ya watu hadi kutengwa nao… lakini usikate tamaa bali tambua kuwa Bwana Mungu yu nawe kila upande, Yesu anakutetea kila sehemu usichoke wala kubadilisha kahuli lako lakini baki katika Imani yako.
Ndio maana katika Injili Yesu anawapa wanafunzi wake tahadhari ya kuwa wasiogope nguvu za dunia wala kushindana na furaha ya dunia hii lakini ni lazima kumwogopa Mungu ambaye anaweza kuangamiza mwili pia na roho: Yesu alitaka kuwaambia wanafunzi wake na kutuambia mimi na wewe leo kwamba: kwanza Mungu awe chaguo letu kabla ya vitu vingine viote: Mungu awezi kulinganishwa na wafalme wa kidunia. Injili hii ya Mathayo inatuonesha wazi namna gani wakristu wa kwanza walikuna na changamoto ya nguvu ya Mfalme wa Roma ambaye alitawala wakati ule na kunyanyasa watu ili wamwabudu kama Mungu: wakristu wengi walichinjwa, kupigwa na kunyanganywa vitu vyo licha tu walikataa kumwabudu Mfalme. Basi mimi na wewe leo tujiulize Mfalme wangu ni nani? Labda ni feza ambao unatafuta kila siku, usiku na mchana hadi kutumia njia isiofaa kusudi upate hela hadi kuhisau siku takatifu ya Mungu, labda wewe Mfalme wako ni tabia ya uzinzi, ya wizi na unyanyazaji, labda ni ukorofi, labda ni uwongo na umbeya ambao usababisha watu waishi katika vita na matengano… 
Yesu anakwambia leo wala usikate tamaa na kujilaumu lakini piga hatua moja mbele na kumfuata kusudi upate kupona. Tena Yesu anasema kwamba: kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele ya Baba aliye mbinguni. Bali, kila mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Kwa hiyo Yesu ndiye Mwamuzi na Msaada wetu katika furaha ao katika shida tumuelekeye kila siku ya Maisha yetu tambua bila Yesu katika Maisha yako, ndoa yako, masomo yako, kazi yako ni bure lakini ukimweka mbele kuliko kila kitu atakwambia: usiogope kwa maana kwake Yeye hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa, ambalo halitajulikana. Basi tikifanya mapenzi ya Mungu tutafananishwa na Yesu ambaye alishinda mauti ya kifo na kutukomboa sisi katika utumwa wa dhambi bali kinyume chake yaani tukizingatia mapenzi yetu kuliko Mungu, tutafananishwa na Adamu ambaye kwa kutomtii Mungu alitenda dhambi na kuharibisha ulimwengu kwa kifo. Basi tuwe waaminifu katika Imani yetu ya Kumfuata Mungu.

SHALOOM
SHEMASI BIENVENU KABEYA KUNGWA NGUNGWA POULAIN LOQUACE SDS


Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

MAHUBIRI YA SHEREHE YA PENTEKOSTE MWAKA A WAKANISA: ROHO MTAKATIFU HULITAKATIFUZA KANISA

MAHUBIRI YA SHEREHE YA UTATU MTAKATIFU MWAKA A WA KANISA: ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU, MUNGU AMBAYE YUPO, ALIYEKUWAKO, NA ATAKAYEKUJA

MAHUBIRI YA ADHIMISHO YA ALHAMISI KUU TAKATIFU : EKARISTI NI ALAMA YA UPENDO NA UMOJA